Panapo kipato hakuna mwanamke mwenye dharau

Miyeyusho

Member
Aug 14, 2020
24
36
MWAKA 2019

JAMAA: Kaka Miyeyusho habari? Naitwa Nassoro, samahani naomba unishauri. Nina mchumba wangu nampenda ila yeye anipendi, mara kadhaa ameniambia tuachane ila nambembeleza tunarudiana. Ila sasa naona kawa kweli na maamuzi yake, wiki sasa kila nikimbembeleza ananiambia hanitaki.

MIMI: Ni kweli una mpenda sana tena sana?

JAMAA: Ndio kaka nampenda sana tena sana na nipo tayari kufanya lolote kwaajili yake.

MIMI: Kama kweli unampenda kweli, muache kwanza kwa muda. Muondoe kichwani. Tafuta pesa, tumia muda mwingi sana Kutafuta Pesa.

JAMAA: Sawa kaka.

Mwaka 2021

JAMAA: Kaka mambo vp? Unanikumbuka ni mimi Nassoro nilikuombaga ushauri mwaka 2019(akanitumia screenshot ya maongezi yetu kipindi iko).

MIMI: Yes, nassoro nakukumbuka kaka. Vp unaendeleaje?

JAMAA: Salama kaka, nimekutafuta nikushukuru kaka. Ushauri wako niliufanyia kazi na nashukuru sasa nimepiga hatua kwenye maisha yangu, kipato sasa hakiyumbi. Najitosheleza kimahitaji na kuhudumia familia.

MIMI: Asante sana nasoro, Mungu akuzidishie zaidi ya hapo. Vipi shemej yangu bado mnawasiliana?

JAMAA: Kaka sitaki ata kumsikia, baada ya miaka miwili alikua akinitafuta sana na kunisumbua turudiane. Amekua msumbufu sana tena sana. Mimi simtaki tena.

MIMI: Kwanini wakati ulikua unampenda sana?

JAMAA: Nimepata mwanamke mwingine mzuri zaidi yake na anaeniheshimu na kunisikiliza na kutambua kuwa mimi ni mwanaume.

MIMI: Sawa kaka. Panapo kipato hakuna mwanamke mwenye dharau. Zidisha kipato zaidi na zaidi udumishe mahusiano yako au ndoa yako. Mungu akubariki.


TAFUTA PESA KIJANA
 
MWAKA 2019

JAMAA: Kaka Miyeyusho habari? Naitwa Nassoro, samahani naomba unishauri. Nina mchumba wangu nampenda ila yeye anipendi, mara kadhaa ameniambia tuachane ila nambembeleza tunarudiana. Ila sasa naona kawa kweli na maamuzi yake, wiki sasa kila nikimbembeleza ananiambia hanitaki.

Mkuu kuna ukweli wa asilimia fulani hapo labda kubwa ni ile hali ukiwa na kipato unaweza pia kufanya ma chaguo kadhaa lkn pia kuna watu wana kipato na mke anashughulikiwa tu na wengine umewazidi hata kipato haya mambo huwa naona ni mkono wa muweza tu

Lkn yote kwa yote kuwa na kipato unatatua changamoto nyingi za maisha ya kisasa
 
Mkuu pata pesa halafu uwe humpelekei moto wa kumtosha mkeo/mpenzi uone majibu yake, mkuu hela ni muhimu sana ila siyo kila kitu, kuna heshima pia, hata uwe na pesa kama mwanamke wako humheshimu na kumsikiliza bado hela zako unazozitafuta zitaenda kutumika kuwajengea majumba wanaume wenzako, narudia tena mkuu, pesa ni muhimu sana lakini siyo kila kitu.
 
mkuu pata pesa halafu uwe humpelekei moto wa kumtosha mkeo/mpenzi uone majibu yake, mkuu hela ni muhimu sana ila siyo kila kitu, kuna heshima pia, hata uwe na pesa kama mwanamke wako humheshimu na kumsikiliza bado hela zako unazozitafuta zitaenda kutumika kuwajengea majumba wanaume wenzako, narudia tena mkuu, pesa ni muhimu sana lakini siyo kila kitu.
Unajiskiaje uwe na pesa mingi lakini kidubwana cha kumkuna manzi hakifanyi kazi..
 
Back
Top Bottom