Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,482
- 40,001
PAMOJA NA KUMTUMIA MENGI, MIKAKATI 14 YA WAPIGANAJI ITAWAANGUSHA
(Makala hii inaweza kuchapwa na chombo chochote cha habari kwa kuzingatia jina la mtunzi linabakia lilivyo pamoja na barua pepe. Mabadiliko yoyote ya uhariri yasibadili maudhui ya makala hii.)
Na. M. M. Mwanakijiji
Pamoja na mkakati wa kumtumia mfanyabiashara maarufu nchini mzee Reginald Mengi wapiganaji walioko CCM bado watajikuta wana wakati mgumu ufikapo uchaguzi wa 2010. Katika makala yangu iliyopita nilihoji hasa ni kitu gani wapiganaji hawa wanapigania ndani ya CCM. Makala ile ni mwendelezo wa makala mbili za nyuma ambazo zote zinahusu vita hii ya ufisadi na hasa jaribio langu la kuonesha kuwa tunayo nafasi moja tu ya kubadili mwelekeo wa taifa letu.
Nilionesha katika makala za awali kuwa tukifanya kosa la kupigana vita hivi kama gizani basi mafisadi, makuwadi wao na vikaragosi vya ufisasi watapeta ufikapo uchaguzi mkuu ujao. Katika ile makala yangu ya "Ukosoaji wa wa Wazi wa Wapambanao na Ufisadi" nilieleza kwa kirefu juu ya kile kilichopo mbele yetu.
Nilijenga hoja na kusema kuwa "kwa mwendo wa sasa wa wapiganaji wetu na nikiangalia mwelekeo wa harakati za mabadiliko nashawishika kuamini kuwa vita hii ni vita ya maneno na siyo ya yenye mkakati wa ushindi.
Ni vita ya mbele ya vyombo vya habari na kwenye majukwaa ya siasa. Ni vita ya wanaharakati kulalamika kuwa "mafisadi wanataka kutunyang'anya majimbo" na kuwa "mafisadi wanamwaga fedha kwenye majimbo yetu". Sisikii kauli za wapiganaji wenye fikra za ushindi."
Katika makala hii nitajaribu kuangalia kile nilichokiangalia katika makala ile ya Augusti 12, 2009 kwenye gazeti la Tanzania Daima lakini kwa kuangalia zaidi ni kwa sababu gani wapiganaji walioko CCM (makala ile iliwazungumzia wapiganaji kwa ujumla) wamejitengenezea mazingira ya kushindwa kwao kwani mikakati wanayotumia kupambana na ufisadi ni mkakati utakaosababisha kuanguka kwao.