Pamoja na kumtumia Mengi mikakati 14 ya Wapiganaji CCM itawaangusha

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
PAMOJA NA KUMTUMIA MENGI, MIKAKATI 14 YA WAPIGANAJI ITAWAANGUSHA
(Makala hii inaweza kuchapwa na chombo chochote cha habari kwa kuzingatia jina la mtunzi linabakia lilivyo pamoja na barua pepe. Mabadiliko yoyote ya uhariri yasibadili maudhui ya makala hii.)

Na. M. M. Mwanakijiji

Pamoja na mkakati wa kumtumia mfanyabiashara maarufu nchini mzee Reginald Mengi wapiganaji walioko CCM bado watajikuta wana wakati mgumu ufikapo uchaguzi wa 2010. Katika makala yangu iliyopita nilihoji hasa ni kitu gani wapiganaji hawa wanapigania ndani ya CCM. Makala ile ni mwendelezo wa makala mbili za nyuma ambazo zote zinahusu vita hii ya ufisadi na hasa jaribio langu la kuonesha kuwa tunayo nafasi moja tu ya kubadili mwelekeo wa taifa letu.

Nilionesha katika makala za awali kuwa tukifanya kosa la kupigana vita hivi kama gizani basi mafisadi, makuwadi wao na vikaragosi vya ufisasi watapeta ufikapo uchaguzi mkuu ujao. Katika ile makala yangu ya "Ukosoaji wa wa Wazi wa Wapambanao na Ufisadi" nilieleza kwa kirefu juu ya kile kilichopo mbele yetu.

Nilijenga hoja na kusema kuwa "kwa mwendo wa sasa wa wapiganaji wetu na nikiangalia mwelekeo wa harakati za mabadiliko nashawishika kuamini kuwa vita hii ni vita ya maneno na siyo ya yenye mkakati wa ushindi.

Ni vita ya mbele ya vyombo vya habari na kwenye majukwaa ya siasa. Ni vita ya wanaharakati kulalamika kuwa "mafisadi wanataka kutunyang'anya majimbo" na kuwa "mafisadi wanamwaga fedha kwenye majimbo yetu". Sisikii kauli za wapiganaji wenye fikra za ushindi."

Katika makala hii nitajaribu kuangalia kile nilichokiangalia katika makala ile ya Augusti 12, 2009 kwenye gazeti la Tanzania Daima lakini kwa kuangalia zaidi ni kwa sababu gani wapiganaji walioko CCM (makala ile iliwazungumzia wapiganaji kwa ujumla) wamejitengenezea mazingira ya kushindwa kwao kwani mikakati wanayotumia kupambana na ufisadi ni mkakati utakaosababisha kuanguka kwao.
 
Attachments

  • PAMOJA NA KUMTUMIA MENGI.doc
    61.5 KB · Views: 394
Nakuunga mkono, haswa pale wanapoongozwa na katiba ya CCM badala ya katiba ya nchi. Vita hii ina walakini lazima tukubali hilo. Wanaongea huku wanaangalia pembeni kwa woga JK amereact vipi. When is project X coming?
 
Nidhamu ya woga ni tatizo sugu si tu kwenye medani za kisiasa,bali hata jamii kwa ujumla...Nidhamu ya woga ni tatizo sugu sana.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu safi sana isipokuwa tu nadhani hukuwatendea haki Wapiganaji kwa sababu wewe unatazama mwisho wa sefari nzima, wakati hawa jamaa zetu bado kabisa hawajaondoka hata bandarini..
Kifupi ni kwamba Wapiganaji wanaitazama hatua kubwa ya uchaguzi ujao ambao kwanza ni lazima wapite mchekecho wa ndani ya chama ili wapate kusimama kama mgombea na chama kitaifa. Hivyo kutumia ilani ya chama ni muhimu zaidi ktk utangulizi wa mashambulizi tofauti na mtazamo wako..

Kama unakumbuka JK amebailisha mfumo mzima wa uchaguzi ndani ya chama, hivyo kujitangaza kwao ktk majimbo yao ni muhimu sana iili wapate kuyaweka majina yao ktk ushindani wa kwanza. Mkuu wangu kama unakumbuka makosa alofanya Kikwete na team yetu ya taifa ni pale alipoweka nguvu yote kwa Taifa Stars kucheza kombe la dunia pasipo kufahamu kwamba ni lazima kwanza Taifa Stars ishinde michuano ya Afrika.

Akaitengeneza Taifa stars kwa kuipa makocha wakubwa wakubwa hali team zetu zote daraja la juu (legue kuu) zimejaa wageni toka Kenya, Kongo, Uganda na nchi jirani.. Hivyo ktk wachezaji 22 wa timu ya Taifa waliongia michuano ya Afrika, NUSU kama sii robo tatu yake ni wachezaji waliokaa benchi mwaka mzima ktk legue ya Taifa. Hawana uzoefu kabisaaa, na uwezo wao ni mdogo kuliko hata hao wachezaji wa nje ambao huko kwao iwe Kenya au Uganda hawana nafasi ktk timu ya Taifa..Na hata wawe na nafasi haitusaidii kitu sisi ktk kuwaadaa vijana wetu kucheza michezo mikubwa wnapokuwa benchi mwaka mzima ktk legue ya ndani.

Sasa nambie ikiwa huyo Udhiambo sijui Oginga hayupo ktk timu ya Taifa ya Kenya na ndiye mchezaji mashuhuri wa legue ya Taifa unategemea nini toka mchezaji Mtanzania ambaye mwaka mzima amekaa benchi?..kweli kuna kufikiria World cup hapa au tunajidanganya sisi wenyewe!

Binafsi, nin mashaka na Wapiganaji kujinadi ktk majimbo yao..Kuhakikisha kwamba ushindi wa uchaguzi mkuu unatanguliwa na ushindi ktk majimbo yao..Sasa ikiwa kweli wanajihami badala ya kushambulia basi bila shaka ni bora mashambulizi yenyewe yahusiane na pinzani ktk jimbo lake.

Kosa kubwa niloliona mimi kutoka kwa Wapiganaji ni pale wanapo nadi nguvu na Ufisadi wa kina Rostam wakati hawa watu wanagombea kura za wananchi toka jimbo lao i.e Ukerewe..Wapiga kura siku ya siku watashindwa kuelewa uhusiano wa Rostam na Ukerewe au mgombea unayepingana naye! kisha juhudi hizi zitawakwaza hata wagombea halali, kwani wananchi (kina Ndivyo tulivyo) watafikiria mpinzani wako amewekwa na Rostam.. yale yale yanayomkuta ndugu yetu msomi wa London - Mwakalinga.

Hiyo vita ya mtu ya Mwakyembe na Mwakalinga inatisha zaidi na hakika nakubalianana na wewe kwamba Wapiganaji wanaweza kujikuta ktk wakati mgumu zaidi..Kila mbunge alokwenda ktk jimbo lake ameshindwa kueleza uhusiano wa mgombea yeyote dhidi yao pasipo kuwahussha mafisadi kwa sababu hawana ushahidi wala hawafgahamu ni nani atakuwa mgombea dhidi yao.. Hivyo siku wananchi watakapo gundua kwamba hakuna Uhusiano kati ya Mafisadi na mgombea aliyesimama dhidi ya Mpiganaji..juhudi zote hizi zitakuwa hazina matunda kwa sababu wao wameweka nguvu zote ktk uchaguzi wa taifa hali wanaopambana nao ni ktyk nchujo wa jimbo.

Kifupi mbinu ya Wapambaniaji ni hatari zaidi kwao kuliko kwa Mafisadi na sidhani kama Mafisadi wana lolo9te la kufanya isipouwa kukaa pembeni wakitafuna popcorn kutazama mchezo wa sinema baina ya wanaCCM wenyewe wakiumizana.

Ushahuri wangu mkubwa ni Wapiganaji kujikita ktk majimbo ya Mafisadi. Kujenga wagombea dhidi ya Mafisadi na kuwatangaza kwa nguvu zote badala ya kujibnadi wao ktk majimbo ambayo hayana ushindani na Mafisadi.

Mafisadi hawahitaji majimbo hayo 11, kwa sababu wajumbe 11 hawana nguvu kabisa ndani ya chama au serikali kuu ikiwa Mafisadi wataweza kushika majimbo yote yaliyobakia..mchezo utakuwa kama wa mwaka huu au uchaguzi wa mwaka 2005 ambapo Wapiganaji watalazimika kujiunga ma mafisadi ktk uchaguzi mkuu (World cup) kuunda timu moja laa sivyo nani atawapa support ya kifedha au jukwaani itakapo fika wanasimama na mgombea wa Chadema au CUF.

Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wa hawa wapiganaji kuumbuka ktk uchaguzi ndani ya chama (mfano wa Mwakyembe na Mwakalinga) na pia wakashindwa uchaguzi mkuu kwa sababu watakosa support kubwa ya wajumbe wa CCM (Mafisadi)..

Ndio maana mkuu wangu umeniona nikizungumza sana kuhusiana na Mwakalinga na kwamba mkuu wangu hakufaa kumpiga vita Mwakyembe ktk jimbo moja. Inasikitisha, haipendezi lakini ndio ukweli wenyewe kuwa Simba (animal instict) ktk mawindo humchagua mnyama dhaifu au yule aliyejitenga na kundi kubwa..Na Mwakalinga kaiona nafasi hiyo, Mwakyembe ni dhaifu, ndama ambaye bado hajaweza kuwa na kasi za kumshinda duma bila fadhila za mafisadi (mabeberu), uwezekano wa kumshinda ni mkubwa.
 
Last edited:

12. Walikuwa wapi tulipoibua kashfa mbalimbali?
Yawezekana wapiganaji wetu wamechelewa kuja lakini wengine tunawauliza walikuwa wapi tulipoibua kashfa mbalimbali ambazo leo zinajulikana kuwa ni za kweli? Kuanzia kashfa ya wanafunzi walioachwa Ukraine, ubadhirifu na uongozi mbovu kule ATCL, mambo ya Meremeta n.k kwanini wapiganaji wetu hawajasimama kuyavalia njuga? Leo hii kama vile nchi ya mazezeta tunaanza kuburuzana tena kwenye suala la shirika la reli wakati tuliyaandika toka mwanzo kuhusu suala hilo? Leo hii sheria ya madini imeendelea kuzungushwa na sheria ya Usalama wa taifa hata kuangaliwa haiangaliwi wapiganaji wetu mbona wako kimya? Siyo kwamba wanachotaka wao ni ubunge tu na siyo kile kinachokuja na nafasi hiyo?

Mzee Mkjj

Nakuunga mkono kwenye hoja zote 14 isipokuwa hioja hapo juu nambari 12.

Sioni kama kuna ulazima wa wapiganaji kuangushwa kwenye kampeni yao iwapo ushiriki wao kwenye kashfa za nyuma ulikuwa dhaifu. Mimi naamini hilo walishaliona na ndio maana wakaamua kutumia nguvu ya Umoja. Ndani ya timu yao wapo wakina Mwakyembe ambao wanajulikana kwa kukemea Richmond, nio la Umoja wao ni kutumia nguvu za wana timu wengine kuzima mapngo kwenye udhaifu wa wenzao. Kwa hili wana nafasi kubwa ya kufanikiwa.

Iwapo watajirekebisha kikamilifu katika hoja zingine 13, nina uhakika muda uko upande wao kabla ya uchaguzi 2010.
 
Mzee Mwanakijiji,

Wacha nikaichape hii habari yako na kuisambaza maana ujumbe wako ndio huo huo ambao tumekuwa tukiongea wengine huku wilayani.

Mtu unasema wameleta milioni mia 400 kuniangusha na chukueni, baada ya mkutano na wewe unatoa pesa tena kwa wajumbe wale wale uliokuwa unawaambia rushwa ni mbaya.

Hapa Kyela juzi kulikuwa na kongamano iliandaliwa na mbunge wetu pamoja na mbunge wa viti maalumu mama Ngowi. Waalikwa walikuwa wanawake, eti kujifunza ujailiamali. Hakukuwa na kitu chochote kinachohusu ujasiliamalina mwisho wa mkutano kila mama akapewa 5,000 na kanga. Walipotoka hapo hao akina mama wakaanza kutukana kwamba katupotezea siku nzima ili atupe kanga tu?

Kwa mtu anayepigana na ufisadi toka moyoni mwake hatakiwi kufanya hayo.

Kuna mengine mbunge kwa mfano kwenye mkutano mmoja na wapambe anasema Mwakalinga kapewa pesa nyingi sana na mafisadi. Siku nyingine na wapambe hao hao anasema Mwakalinga hana pesa hata huko Ulaya ni kibarua tu ndio maana hata wapambe wake hapa njaa kali. Yeye anafikiri ni vijembe kumbe ni messages mbili zinazojichanganya.

Mengi hajawahi kusaidia Kyela toka mimi naanza kuishi hapa, ghafla leo anakuja na kumwaga mapesa, wananchi sio wajinga, watayachukua lakini pia watajua ni siasa. Alikuwa wapi miaka yote?

Hii makala yako itakuwa kwenye vijiwe vyote hapa mjini ili tuijadili kwa undani.
 
Hivi kweli mkiwaangalia kwa MAKINI kabisa mnawaona wote ni "wapambanaji"? Kundi hilo kwa kuliangalia harakaharaka utaona kuna vikundi vidogo vifuatavyo:
1. Wale wanaodhani walistahili kupewa vyeo kama Uwaziri, Unaibu Waziri au hata Uwaziri Mkuu;
2. Wale ambao hawakutaka JK awe Rais wa TZ;
3. WAle ambao wamekosa MGAO wao "halali" kwenye huu ufisadi uliopita;
4.Walipaji visasi katika dhahma mbalimbali;
5.Wanaotumwa kuwachunguza wenzao ndani ya kundi hilo.
Ni vigumu mno mtu kuwa ndani ya CCM halafu akapinga ufisadi.
 
Vyote hawa vita vyao ni Madaraka, narejea makala ya ndugu yangu Kishoka, Wote kama kweli wana nia ya dhati basi wahamie vyama vya Upinzani, Ndugu yangu utaona kuwa mwakani hawa jamaa hawatapewa tena kugombea ubunge na ndio utakuwa mwisho wao
 
At last MM umenena! huko nyuma wengine tulichangia juu juu bila uchambuzi yakinifu kama huu ambao MM umeufanya, hongera sana personal naungana sana na wachangiaji wengine naweza toa mifano ya wazi juu ya madai mengi kama yachangiwavyo na wadau. kikubwa ni chuki, fitina, visasi, wasi wasi wa kuendelea kuwepo mjengoni na mengine mengi bila kusahau interest za 2015
 
Asante Mzee Mwanakijiji kwa Mada hii, nami nakuunga mkono na kuna maeneo ninatofautiana na wewe kama ifuatavyo.1. wanapigana kwa kujihamiNi kweli wanajihami kwa kupiga kelele za pesa pesa zinamwagwa ili watutoe huko nao wakizimwaga za kwa na kuchanganya na za Mangi anayewahami.2-13 kwenye attachment14. Na mwisho mimi siamini kama wanamtegemea JK, kuanzia huyo mfadhili wao, kumtajataja JK ni kumpaka tuu mafuta kwa mgongo wa chupa. Time will tell.
 
Attachments

  • PAMOJA NA KUMTUMIA MENGI.doc
    35 KB · Views: 112
Last edited by a moderator:

Mzee Mkjj

Nakuunga mkono kwenye hoja zote 14 isipokuwa hioja hapo juu nambari 12.

Sioni kama kuna ulazima wa wapiganaji kuangushwa kwenye kampeni yao iwapo ushiriki wao kwenye kashfa za nyuma ulikuwa dhaifu. Mimi naamini hilo walishaliona na ndio maana wakaamua kutumia nguvu ya Umoja. Ndani ya timu yao wapo wakina Mwakyembe ambao wanajulikana kwa kukemea Richmond, nio la Umoja wao ni kutumia nguvu za wana timu wengine kuzima mapngo kwenye udhaifu wa wenzao. Kwa hili wana nafasi kubwa ya kufanikiwa.

Iwapo watajirekebisha kikamilifu katika hoja zingine 13, nina uhakika muda uko upande wao kabla ya uchaguzi 2010.

YeboYebo,

Kama CCM ingekuwa na nia ya kusawazisha suala la Richmond, ingeliamkia mapema na si kuchelewa mpaka Taifa kufikia kuingia hasara kiasi hivho.

Kilichotokea ni wao CCM kupokonya tonge kutoka Upinzani baada ya Upinzani kuanza kurembeka na kashfa ya EPA
 
Jamanni mapambano ya ufisadi hayana itikadi ya chama, hatuwezi kuwaona wapambanaji ni wasanii kwa sababu tu et wapo CCM. Siku moja niliuzulia mkutano wa mwakyembe katika kiwanja cha siasa pale Kyela. Kuna baadhi ya watu wakamuomba ahamie chama cha upinzani ili apambane vizuri. Jibu alilotoa akasema ni heri CCM ninaweza kusema na nikawa bado mwanachama. Alitoa mifano mingi jinsi vyama vingine ambapo wakitofautiana kidogo tu basi watu wanafukuzwa uanachama. Hili la Chadema lilikuwa bado halijatokea kumbe hata vyama vya upinzani vinaweza kutatua tofauti yao kwa amani bila ya kufukuzana hili ni somo kwa vyama vingine vya siasa.​
Kutumia katiba ya CCM katika mapambano si kosa kwani kwetu sisi heri mapambano yaende mbele atimaye tupate ukombozi. Pia katika chama kama cha CCM kutumia jina la kikwete kwenye mapambano ni njia ya kupambana hili huyu jamaa asije akageuka hata yeye ataogopa kwani ataonekana haonyeshi nia ya mapambano.
Mafisadi ni watu makini tena leo wanajifanya wao eti hawasumbuliwi na mapambano hiyo ni njia ya kutaka kuhadaa umma. NDUgu zangu hawa watu hawalali hila wanajifanya wana amani ili mapambano yaonekane hayawaumizi ili yapoe. Dawa yao ni moto mpaka kieleweke.
Mtu kama mwakyembe ni mtu makini, ni mjanja tena wanaofikiri wataweza kumkamata au kumshinda kirahisi wanajidanganya au wanacheza mchezo wa kitoto. Huyu bwana sio wa kuenda nae pupa. Kwa makelele ya wakinamwakalinga sidhani. Waamulize kamanda mwakipesile kilichompata ni nini mpaka leo anamchukia.Ndugu zangu huyu ni mtu makini. Haliweza kuiteka kyela na kuchukua jimbo kwa muda mfupi sana. Wengi walijaribu kabla lakini waliishia kupiga mayowe tu. Aliwaambia wanakyela yeye ni mbunge wa east africa hivyo anawapa nafasi ya kumtumia hakuja na mayowe kama wanavyokuja hawa, alijua kilicho mbele yake. Kwa kifupi amewahi kujiuzulu katika menejimenti ya NBC ( kwa kinachosemekana kuwa watu wa nje wapewa mikopo kwa riba ndogo huku weusi ndio riba kama wanamfukuza kukopa). Amewahi shiriki kwenye tume ya muafaka Zanzibar kipindi cha mzee Mkapa.
Mimi kwa mfumo anaokuja nao mwakalinga nashawishika kabisa kusema kuwa ametumwa na mafisadi. Lengo likiwa ni kupunguza mapambano dhidi yao. Hata ukiwa unakula, paka anakusumbua anataka nae kula kupunguza usumbufu mpe chakula chake pembeni utapata ahueni. Hii mbinu inatumika sana hata tanzania mambo yanapo kuwa hot wanapeleka mtuhumiwa wa epa mahakamani. Hapo ndio wanapata muda wa ahueni wa kujadili mambo yao na kujipanga. Kwani watanzania wote waanza kujadili mambo ya EPA. Sasa hapa wanachojaribu ni kumfanya mwakyembe aanze kudili na mwakalinga wao wale kiulaini. Wapate haueni.
Kama kweli mwakalinga ana nia ya kuchukua jimbo hawezi kupambana na mtu makini kama mwakyembe kwa makelele kiasi hichi. Huyu mtu anahitaji umakini sana. Mpaka sasa sina mashaka mwakalinga ameshindwa. Huo ndio ukweli hata kama atapinga.
Kumtumia Mengi hakuna tatizo hawa watu ni wenye pesa. Sasa watu maskini kupambana na kikundi cha watu wenye pesa kunahitaji umoja. Lakini kuwepo kwa mengi kati yao basi kunawapa ahueni kwa upande wa mapesa. Hivi mnajua kuwa simba akitaka kukamata mnyama anatishia kwanza halafu yule mnyama atakae kimbia peke yake, basi ndio atakula naye sahani moja amkamate. Hivyo muungano wa wapiganaji ni mzuri kwa muda huu. Tena sio muda wa kuhama CCM. Kuhama kutawavuruga mapambano ya kweli ni imani hivyo uwe CCM au UPINZAni mapambano ni yaleyale. Issue ni ufisadi issue si chama.
Mimi sina matatizo na msimamo wa mzee mwakijiji ila imani yangu ni kuwa mapambano yatashinda. Kwani kusema ni ya kwenye vyombo vya habari hawa watu wanapesa kitu cha kwanza ni kutafuta umoja wa watanzania. Kutafuta kuungwa mkono na watanzania. Njia inayotumika ni nguvu ya umma.

Hawa watu kutumia katiba ya chama ni kuwafunga mdomo wanachama ambao wanasema wanangusha chama na wao kuonekana kama hawasimamii katiba ya chama. Kusimama mabegani mwa kikwete ni njia ya kumbeba mtu hata kama hataki na kumwingiza kwenye mapambano. Kiongozi inatakiwa awe kinala wa mapambano sasa anapokuwa kimya mungizeni kama anataka akanea mwenyewe. Kujilinda kuendelea kuwepo bungeni ndio njia sahihi ya kujilinda maana wasipokuwepo bungeni watashughulikiwa mpaka wamalizwe. sasa hivi kuna mtu anafikiri CCM wanaweza kumnyanganya kadi spika? Wakiweza kufanya hilo CCM haisimami tena. Itapasuka ni mkwala tu hawawezi fanya hilo. Ukitaka wajaribu!!!
. TUWAUNGE MKONO WAPIGANAJI TUTASHINDA!!!
 
Fikra za wapiganaji wengi ni kuwa ni ngumu kwao kupigana nje ya CCM. Suala la wagombea huru lingekuwa na msaada mkubwa katika mazingira haya kwasababu, kama inaonekana ngumu kutafuta chama mbadala basi ingekuwa rahisi kujiuza kama mtanzania. Ndo maana hata ule waraka wa kanisa ambao pamoja na mambo mengine umeliongelea suala la wagombea huru, umekuwa kama mwiba kwenye masikio ya wanasiasa wakubwa.
 
Hawa jamaa wanasoma tu alama za nyakati na hakuna kingine hapa, Kama kweli wanataka kupigana wawaseme mafisadi ni wakina nani?? Hoja ya ufisadi siyo ya CCM na pia mimi napenda kama wote wale makamanda wavuliwe uachama CCM
 
Jamanni mapambano ya ufisadi hayana itikadi ya chama, hatuwezi kuwaona wapambanaji ni wasanii kwa sababu tu et wapo CCM. Siku moja niliuzulia mkutano wa mwakyembe katika kiwanja cha siasa pale Kyela. Kuna baadhi ya watu wakamuomba ahamie chama cha upinzani ili apambane vizuri. Jibu alilotoa akasema ni heri CCM ninaweza kusema na nikawa bado mwanachama. Alitoa mifano mingi jinsi vyama vingine ambapo wakitofautiana kidogo tu basi watu wanafukuzwa uanachama. Hili la Chadema lilikuwa bado halijatokea kumbe hata vyama vya upinzani vinaweza kutatua tofauti yao kwa amani bila ya kufukuzana hili ni somo kwa vyama vingine vya siasa.​

Kutumia katiba ya CCM katika mapambano si kosa kwani kwetu sisi heri mapambano yaende mbele atimaye tupate ukombozi. Pia katika chama kama cha CCM kutumia jina la kikwete kwenye mapambano ni njia ya kupambana hili huyu jamaa asije akageuka hata yeye ataogopa kwani ataonekana haonyeshi nia ya mapambano.
Mafisadi ni watu makini tena leo wanajifanya wao eti hawasumbuliwi na mapambano hiyo ni njia ya kutaka kuhadaa umma. NDUgu zangu hawa watu hawalali hila wanajifanya wana amani ili mapambano yaonekane hayawaumizi ili yapoe. Dawa yao ni moto mpaka kieleweke.
Mtu kama mwakyembe ni mtu makini, ni mjanja tena wanaofikiri wataweza kumkamata au kumshinda kirahisi wanajidanganya au wanacheza mchezo wa kitoto. Huyu bwana sio wa kuenda nae pupa. Kwa makelele ya wakinamwakalinga sidhani. Waamulize kamanda mwakipesile kilichompata ni nini mpaka leo anamchukia.Ndugu zangu huyu ni mtu makini. Haliweza kuiteka kyela na kuchukua jimbo kwa muda mfupi sana. Wengi walijaribu kabla lakini waliishia kupiga mayowe tu. Aliwaambia wanakyela yeye ni mbunge wa east africa hivyo anawapa nafasi ya kumtumia hakuja na mayowe kama wanavyokuja hawa, alijua kilicho mbele yake. Kwa kifupi amewahi kujiuzulu katika menejimenti ya NBC ( kwa kinachosemekana kuwa watu wa nje wapewa mikopo kwa riba ndogo huku weusi ndio riba kama wanamfukuza kukopa). Amewahi shiriki kwenye tume ya muafaka Zanzibar kipindi cha mzee Mkapa.
Mimi kwa mfumo anaokuja nao mwakalinga nashawishika kabisa kusema kuwa ametumwa na mafisadi. Lengo likiwa ni kupunguza mapambano dhidi yao. Hata ukiwa unakula, paka anakusumbua anataka nae kula kupunguza usumbufu mpe chakula chake pembeni utapata ahueni. Hii mbinu inatumika sana hata tanzania mambo yanapo kuwa hot wanapeleka mtuhumiwa wa epa mahakamani. Hapo ndio wanapata muda wa ahueni wa kujadili mambo yao na kujipanga. Kwani watanzania wote waanza kujadili mambo ya EPA. Sasa hapa wanachojaribu ni kumfanya mwakyembe aanze kudili na mwakalinga wao wale kiulaini. Wapate haueni.
Kama kweli mwakalinga ana nia ya kuchukua jimbo hawezi kupambana na mtu makini kama mwakyembe kwa makelele kiasi hichi. Huyu mtu anahitaji umakini sana. Mpaka sasa sina mashaka mwakalinga ameshindwa. Huo ndio ukweli hata kama atapinga.
Kumtumia Mengi hakuna tatizo hawa watu ni wenye pesa. Sasa watu maskini kupambana na kikundi cha watu wenye pesa kunahitaji umoja. Lakini kuwepo kwa mengi kati yao basi kunawapa ahueni kwa upande wa mapesa. Hivi mnajua kuwa simba akitaka kukamata mnyama anatishia kwanza halafu yule mnyama atakae kimbia peke yake, basi ndio atakula naye sahani moja amkamate. Hivyo muungano wa wapiganaji ni mzuri kwa muda huu. Tena sio muda wa kuhama CCM. Kuhama kutawavuruga mapambano ya kweli ni imani hivyo uwe CCM au UPINZAni mapambano ni yaleyale. Issue ni ufisadi issue si chama.
Mimi sina matatizo na msimamo wa mzee mwakijiji ila imani yangu ni kuwa mapambano yatashinda. Kwani kusema ni ya kwenye vyombo vya habari hawa watu wanapesa kitu cha kwanza ni kutafuta umoja wa watanzania. Kutafuta kuungwa mkono na watanzania. Njia inayotumika ni nguvu ya umma.

Hawa watu kutumia katiba ya chama ni kuwafunga mdomo wanachama ambao wanasema wanangusha chama na wao kuonekana kama hawasimamii katiba ya chama. Kusimama mabegani mwa kikwete ni njia ya kumbeba mtu hata kama hataki na kumwingiza kwenye mapambano. Kiongozi inatakiwa awe kinala wa mapambano sasa anapokuwa kimya mungizeni kama anataka akanea mwenyewe. Kujilinda kuendelea kuwepo bungeni ndio njia sahihi ya kujilinda maana wasipokuwepo bungeni watashughulikiwa mpaka wamalizwe. sasa hivi kuna mtu anafikiri CCM wanaweza kumnyanganya kadi spika? Wakiweza kufanya hilo CCM haisimami tena. Itapasuka ni mkwala tu hawawezi fanya hilo. Ukitaka wajaribu!!!
. TUWAUNGE MKONO WAPIGANAJI TUTASHINDA!!!

Wapambe njaa au wa kutumwa utawaona tu. Hii thread ni kuhusu wapiganaji na wala sio Mwakalinga. Kuna thread ya Mwakalinga kule na unaweza kwenda kutukana utakavyo.

Kama Mwakyembe ni makini kwanini apate kiwewe cha kuanza kuropoka kuhusu huyo Mwakalinga? Mara milioni 400, mara wanataka kuniua, mara Mwakalinga anauza unga Ulaya, mara Mwakalinga kakamatwa na polisi, mara Mwakalinga kajitoa. Hayo sio maneno ya mtu makini, ni maneno ya mtu mwenye wasiwasi na anayetaka aonewe huruma.

Mwakalinga kajitambulisha tena wiki moja, wewe unaanza kusema makelele kiasi hiki, lini umemsikia Mwakalinga anaongea?

Ukisoma magazeti ya Mengi utafikiri Mwakyembe anaandamwa kumbe yeye ndiye anaongoza kuandama kila anayetaka kumpinga. Alianza na Mwanjala sasa kahamia kwa Mwakalinga.

Uzuri Kyela tumemjua na kama anafaa taifa asi amwambie JK ampe ubunge wa taifa. Sisi huku vijijini tunataka mtu wa kushirikiana naye kusogeza maendeleo ya Kyela mbele.

Njoo Kyela umsaidia mpiganaji wako, kura zitapigwa huku wilayani na wala sio JF. Kama Mwakalinga kashindwa si anzeni kufurahi? Mbona mnahaha huku na huku wakati hata kampeni yenyewe haijaanz?
 
This guy has been denounced with Mr Mwakalinga! Anapoteza muda wala msimsome ....
 
This guy has been denounced with Mr Mwakalinga! Anapoteza muda wala msimsome ....

Masanilo aka Ze Comedy,

Wewe Mshamba wa Marekani ondoa ujuha wako. Ukiweza rudi kawasaidie ndugu zako wasukuma.

Mimi sio mwakilishi wa Mwakalinga. Mbona unaanza kujilegeza kwa Mwakalinga, vipi umeambiwa anapenda .....
 
Ni mikakati gani basi ambayo hawa wapiganaji wanaweza kuitumia kuelekea na hatimaye kujiletea ushindi?
 
Njia pekee ya kweli ni kuiga mfano wa Mrema, na kurekebisha kasoro ambazo zimemfanya Mrema apoteze mwelekeo. Nia ni kujenga sio kujitukuza. Kama ubinafsi ukiachwa na vyama vikajengwa kama taasisi future itakuwepo.Tatizo naloliona sasa ni kuwa ni CCM tu inayoendeshwa kama taasisi yenye structures na uhuru atleast unaoheshimiwa, ingawa wanawalinda wale wanaodhani ni "wao" bila kujari inawagharimu nini.
Vyama vingi vinaoperate kama NGO za watu au vinaonyesha kuwa bila watu fulani fulani basi navyo havipo.
 
Mzee Mwanakijiji,

Wacha nikaichape hii habari yako na kuisambaza maana ujumbe wako ndio huo huo ambao tumekuwa tukiongea wengine huku wilayani.

Mtu unasema wameleta milioni mia 400 kuniangusha na chukueni, baada ya mkutano na wewe unatoa pesa tena kwa wajumbe wale wale uliokuwa unawaambia rushwa ni mbaya.

Hapa Kyela juzi kulikuwa na kongamano iliandaliwa na mbunge wetu pamoja na mbunge wa viti maalumu mama Ngowi. Waalikwa walikuwa wanawake, eti kujifunza ujailiamali. Hakukuwa na kitu chochote kinachohusu ujasiliamalina mwisho wa mkutano kila mama akapewa 5,000 na kanga. Walipotoka hapo hao akina mama wakaanza kutukana kwamba katupotezea siku nzima ili atupe kanga tu?

Kwa mtu anayepigana na ufisadi toka moyoni mwake hatakiwi kufanya hayo.

Kuna mengine mbunge kwa mfano kwenye mkutano mmoja na wapambe anasema Mwakalinga kapewa pesa nyingi sana na mafisadi. Siku nyingine na wapambe hao hao anasema Mwakalinga hana pesa hata huko Ulaya ni kibarua tu ndio maana hata wapambe wake hapa njaa kali. Yeye anafikiri ni vijembe kumbe ni messages mbili zinazojichanganya.

Mengi hajawahi kusaidia Kyela toka mimi naanza kuishi hapa, ghafla leo anakuja na kumwaga mapesa, wananchi sio wajinga, watayachukua lakini pia watajua ni siasa. Alikuwa wapi miaka yote?

Hii makala yako itakuwa kwenye vijiwe vyote hapa mjini ili tuijadili kwa undani.

You are totally wrong! Mwanakijiji ana message tofauti kabisa ya utazamo wako. Wewe umejikita kwenye ushabiki kati ya Mwakyembe na Mwakalinga wakati Mwanakijiji anaangalia mbali zaidi ya mambo hayo ya uhasama/mashindano kati ya mtu na mtu! Mwanakijiji ana mstakabali wa TAIFA ndani ya moyo na maneno aliyoyaandika.
 
Back
Top Bottom