Pamoja na kumtumia Mengi mikakati 14 ya Wapiganaji CCM itawaangusha

Ni mikakati gani basi ambayo hawa wapiganaji wanaweza kuitumia kuelekea na hatimaye kujiletea ushindi?

Nina Maswali kwa Wapiganaji na wale watetezi wa Wapiganaji na Mbinu Zao

1: Kwa Kuwa wao wanadai wanapambana dhidi ya Mafisadi, je ni mikakati gani wanayoweka kuhakikisha hao wanaowadhani ni Mafisadi hawarudi Mjengoni?

2: Hii inanipa shaka kwa sababu

Wapiganaji wanadai wanapambana na Mafisadi, lakini the battle ground ni katika Majimbo yao at least basi wangehamishia uwanja wa Mapambano katika kuhakikisha hao Masifadi hawarudi Mjengoni au wanadhani wapiga kura wa Kyela wana uwezo wa Kubadilisha matokeo ya Bariadi Mashariki?

3: Nimesikia katibu mwenezi Chiligai amesema wanawaunga Mkono, Chiligati huyu huyu aliwaambia Wapiganaji wanaligeuza Bunge Ze Commedy, sasa wao wanasimama wapi?

4: Je hawaoni kwamba wanapowaambia watu wapokee rushwa ni kinyume na Maadili ya Viungozi, je wamesahau kwamba “ Rushwa kwangu ni mwiko sitapokea wala kutoa Rushwa? naongezea " Wala sitahamasisha Rushwa"?

Mimi ningewaona Vidume kama wangeenda katika Majimbo ya hao wanaowaita Mafisadi na kuwaelimisha wananchi wasiwarudishe Mjengoni, vinginevyo ninawaona Waoga kama KUKU
 
Vyote hawa vita vyao ni Madaraka, narejea makala ya ndugu yangu Kishoka, Wote kama kweli wana nia ya dhati basi wahamie vyama vya Upinzani, Ndugu yangu utaona kuwa mwakani hawa jamaa hawatapewa tena kugombea ubunge na ndio utakuwa mwisho wao

- Yaaani wakajiunge na chama cha Zitto? This is incredible idea kama sio theory!

Respect.

FMEs!
 
- Yaaani wakajiunge na chama cha Zitto? This is incredible idea kama sio theory!

Respect.

FMEs!

You are Very Much Obsessed with Zitto Man Mpaka UNABOA, wapi jamaa kamtaja Zitto? Wakitajwa Wapinzani basi wewe Mpinzani unayemjua ni Zitto, come on mkuu I believe you could have done better then this
 
Kutumia katiba ya CCM katika mapambano si kosa kwani kwetu sisi heri mapambano yaende mbele atimaye tupate ukombozi.​

hawa jamaa hawatumii katiba ya CCM kwa kuwa wanaiamini isipokuwa ni janja ya kuonyesha kuwa wao ni waaminifu kwa maslahi ya chama chao. wengi wao ukiwauliza kilichomo humo ndani utaona jinsi wanavyochanganyikiwa. watakachokujibu ni lilelile jibu lao la kawaida "UMETUMWA NA MAFISADI".

Pia katika chama kama cha CCM kutumia jina la kikwete kwenye mapambano ni njia ya kupambana hili huyu jamaa asije akageuka hata yeye ataogopa kwani ataonekana haonyeshi nia ya mapambano.
Kama alivyosema PASCO, hawamsaidii, hawamheshimu na wala hawana mapenzi naye. Kwanza ni mabingwa wa kumsema chinichini. Wanachofanya ni kujaribu kuficha makucha yao mbele ya wanachama wao ambao wanajua kuwa kamwe hawatawavulia wakifika kumshutumu ama kumpiga vita mwenyekiti wao lakini pia wanatambua kuwa Kikwete amehika nguvu za dola zenye kila mabomu, halali na haramu za kumaliza unafiki wao.

Mtu kama mwakyembe ni mtu makini, ni mjanja tena wanaofikiri wataweza kumkamata au kumshinda kirahisi wanajidanganya au wanacheza mchezo wa kitoto. Huyu bwana sio wa kuenda nae pupa. Kwa makelele ya wakinamwakalinga sidhani. Waamulize kamanda mwakipesile kilichompata ni nini mpaka leo anamchukia.Ndugu zangu huyu ni mtu makini. Haliweza kuiteka kyela na kuchukua jimbo kwa muda mfupi sana. Wengi walijaribu kabla lakini waliishia kupiga mayowe tu. Aliwaambia wanakyela yeye ni mbunge wa east africa hivyo anawapa nafasi ya kumtumia hakuja na mayowe kama wanavyokuja hawa, alijua kilicho mbele yake.
Makini ni subjective lakini hata hivyo nakubaliana nawe Mwakyembe ni mjanja mno....tena sana

Kwa kifupi amewahi kujiuzulu katika menejimenti ya NBC ( kwa kinachosemekana kuwa watu wa nje wapewa mikopo kwa riba ndogo huku weusi ndio riba kama wanamfukuza kukopa).
Vinavyosemekana ni vingi mno. Ni bahati mbaya watanzania tupo tayri kuweka imani yetu kwa mambo "yanayosemekana"

Amewahi shiriki kwenye tume ya muafaka Zanzibar kipindi cha mzee Mkapa.
Sio hapo tu, hata katika kujustify mauaji ya wazanzibari/wapemba wakati ule. Hatujasahau umahiri wake wa kutetea umwagaji damu ule tena kwa mikogo nanjeuri kubwa.....

Mimi kwa mfumo anaokuja nao mwakalinga nashawishika kabisa kusema kuwa ametumwa na mafisadi. Lengo likiwa ni kupunguza mapambano dhidi yao.
Yaleyale, simple minds, easy conclusions.....

Kumtumia Mengi hakuna tatizo hawa watu ni wenye pesa.
Same was KIKWETE kuwatumia kina NYARI,ROSTAM,KARAMAGI,LOWASSA na matajiri wengine wengi......

Kuhama kutawavuruga mapambano ya kweli ni imani hivyo uwe CCM au UPINZAni mapambano ni yaleyale.
Si kweli, CCM wanapigania kulinda ulaji wao, Wapinzani wanapigania kupata ulaji wao.....all the same unfortunately

Issue ni ufisadi issue si chama.
Sasa iweje watu watumie katiba na ilani za CCM kuhalalisha issue hiyo?
Kwani kusema ni ya kwenye vyombo vya habari hawa watu wanapesa kitu cha kwanza ni kutafuta umoja wa watanzania. Kutafuta kuungwa mkono na watanzania. Njia inayotumika ni nguvu ya umma.
Hata kama wana kila dalili za unafiki, ushahidi wa ufisadi na mawazo ya kifashisti bado tu nguvu ya umma iwape uhalali wa kutuletea UFISADI MBADALA?

Hawa watu kutumia katiba ya chama ni kuwafunga mdomo wanachama ambao wanasema wanangusha chama na wao kuonekana kama hawasimamii katiba ya chama. Kusimama mabegani mwa kikwete ni njia ya kumbeba mtu hata kama hataki na kumwingiza kwenye mapambano. Kiongozi inatakiwa awe kinala wa mapambano sasa anapokuwa kimya mungizeni kama anataka akanea mwenyewe. Kujilinda kuendelea kuwepo bungeni ndio njia sahihi ya kujilinda maana wasipokuwepo bungeni watashughulikiwa mpaka wamalizwe. sasa hivi kuna mtu anafikiri CCM wanaweza kumnyanganya kadi spika? Wakiweza kufanya hilo CCM haisimami tena. Itapasuka ni mkwala tu hawawezi fanya hilo. Ukitaka wajaribu!!!
Hapa kidogo unaeleweka
 
PAMOJA NA KUMTUMIA MENGI, MIKAKATI 14 YA WAPIGANAJI ITAWAANGUSHA
(Makala hii inaweza kuchapwa na chombo chochote cha habari kwa kuzingatia jina la mtunzi linabakia lilivyo pamoja na barua pepe. Mabadiliko yoyote ya uhariri yasibadili maudhui ya makala hii.)

Na. M. M. Mwanakijiji

Pamoja na mkakati wa kumtumia mfanyabiashara maarufu nchini mzee Reginald Mengi wapiganaji walioko CCM bado watajikuta wana wakati mgumu ufikapo uchaguzi wa 2010. Katika makala yangu iliyopita nilihoji hasa ni kitu gani wapiganaji hawa wanapigania ndani ya CCM. Makala ile ni mwendelezo wa makala mbili za nyuma ambazo zote zinahusu vita hii ya ufisadi na hasa jaribio langu la kuonesha kuwa tunayo nafasi moja tu ya kubadili mwelekeo wa taifa letu.

Nilionesha katika makala za awali kuwa tukifanya kosa la kupigana vita hivi kama gizani basi mafisadi, makuwadi wao na vikaragosi vya ufisasi watapeta ufikapo uchaguzi mkuu ujao. Katika ile makala yangu ya “Ukosoaji wa wa Wazi wa Wapambanao na Ufisadi” nilieleza kwa kirefu juu ya kile kilichopo mbele yetu.

Nilijenga hoja na kusema kuwa “kwa mwendo wa sasa wa wapiganaji wetu na nikiangalia mwelekeo wa harakati za mabadiliko nashawishika kuamini kuwa vita hii ni vita ya maneno na siyo ya yenye mkakati wa ushindi.

Ni vita ya mbele ya vyombo vya habari na kwenye majukwaa ya siasa. Ni vita ya wanaharakati kulalamika kuwa "mafisadi wanataka kutunyang'anya majimbo" na kuwa "mafisadi wanamwaga fedha kwenye majimbo yetu". Sisikii kauli za wapiganaji wenye fikra za ushindi.”

Katika makala hii nitajaribu kuangalia kile nilichokiangalia katika makala ile ya Augusti 12, 2009 kwenye gazeti la Tanzania Daima lakini kwa kuangalia zaidi ni kwa sababu gani wapiganaji walioko CCM (makala ile iliwazungumzia wapiganaji kwa ujumla) wamejitengenezea mazingira ya kushindwa kwao kwani mikakati wanayotumia kupambana na ufisadi ni mkakati utakaosababisha kuanguka kwao.
Mwanakijiji kwa ufahamu wangu ni kwamba ccm haiwatumii hawa wanaojiita makamanda wa ufisadi.Nadhani hapa unakosa muunganisho wa majambo
 
Hii issue ina siri kubwa sana, hapa watu wanashindwa kkujua Mengi anampigania nani, ni ukweli uliowazi kabisa kuwa hii move yote iko supported na mzee mwenyewe JK, kwa sababu hata yeye hatima yake ya 2010 bado haijajulikana, kwa maana hakuweza kabisa kuwatetea jamaa zake hao wa Ufisadi (RA, EL nk), sasa hawa wabunge kwa kiasi fulani waliweza kuumaliza ule upinzani wao waliounzisha kwa JK baada ya kuona wamesalitiwa, hawa wabunge ni wamuhimu mno kwa kipindi kijacho cha JK na ndio maana kwenye hiyo mikutano yao yote ni lazima wammention huyo mkuu,
"Sidhani kama kuna rafiki mkubwa wa JK kama BwMengi" (naomba kurekebishwa), hao watu wameshibana mno na labda sio siri hata hizo fedha zinazogawiwa huko ni zile za kutoka kwa Jk kupitia TRL na miradi mkingine isiyokuwa na kichwa wala miguu.
 
mambo yanazidi kuwiva; political triangulation and neutralization of the opponent strategy has been adopted by CCM. It simply means that the wapiganaji watajikuta wanapigana hewani.
 
PAMOJA NA KUMTUMIA MENGI, MIKAKATI 14 YA WAPIGANAJI ITAWAANGUSHA
(Makala hii inaweza kuchapwa na chombo chochote cha habari kwa kuzingatia jina la mtunzi linabakia lilivyo pamoja na barua pepe. Mabadiliko yoyote ya uhariri yasibadili maudhui ya makala hii.)

Na. M. M. Mwanakijiji

Pamoja na mkakati wa kumtumia mfanyabiashara maarufu nchini mzee Reginald Mengi wapiganaji walioko CCM bado watajikuta wana wakati mgumu ufikapo uchaguzi wa 2010. Katika makala yangu iliyopita nilihoji hasa ni kitu gani wapiganaji hawa wanapigania ndani ya CCM. Makala ile ni mwendelezo wa makala mbili za nyuma ambazo zote zinahusu vita hii ya ufisadi na hasa jaribio langu la kuonesha kuwa tunayo nafasi moja tu ya kubadili mwelekeo wa taifa letu.

Nilionesha katika makala za awali kuwa tukifanya kosa la kupigana vita hivi kama gizani basi mafisadi, makuwadi wao na vikaragosi vya ufisasi watapeta ufikapo uchaguzi mkuu ujao. Katika ile makala yangu ya “Ukosoaji wa wa Wazi wa Wapambanao na Ufisadi” nilieleza kwa kirefu juu ya kile kilichopo mbele yetu.

Nilijenga hoja na kusema kuwa “kwa mwendo wa sasa wa wapiganaji wetu na nikiangalia mwelekeo wa harakati za mabadiliko nashawishika kuamini kuwa vita hii ni vita ya maneno na siyo ya yenye mkakati wa ushindi.

Ni vita ya mbele ya vyombo vya habari na kwenye majukwaa ya siasa. Ni vita ya wanaharakati kulalamika kuwa "mafisadi wanataka kutunyang'anya majimbo" na kuwa "mafisadi wanamwaga fedha kwenye majimbo yetu". Sisikii kauli za wapiganaji wenye fikra za ushindi.”

Katika makala hii nitajaribu kuangalia kile nilichokiangalia katika makala ile ya Augusti 12, 2009 kwenye gazeti la Tanzania Daima lakini kwa kuangalia zaidi ni kwa sababu gani wapiganaji walioko CCM (makala ile iliwazungumzia wapiganaji kwa ujumla) wamejitengenezea mazingira ya kushindwa kwao kwani mikakati wanayotumia kupambana na ufisadi ni mkakati utakaosababisha kuanguka kwao.
Mwanakijiji,
Napenda kuungana nawe asilimia mia na kwa mara nyingine umejenga hoja nzuri sana na inaweza kuwa angalizo kwa hawa wana mgambo.

Napenda kuwajulisha kuwa Makara hii kama ilivyo itatoka kwenye gazeti la TAZAMA TANZANIA linalotoka mara moja kwa juma, kwa hiyo changamkieni.

Kikubwa ambacho nimekiona kwa hawa ndg zangu ni uoga wa kisiasa, na uoga huu unatokana na kuwa hawataki kuenguliwa kwenye majimbo yao na wako tayari kuona kila ujanja unatumika ili wabakie 2010.

Kama kweli wewe unasema mafisadi wamemwaga 400M, wao walijuaje kama ni 400M? na kwa nini isiwe 100M? ina maana kwenye vikao vya kupanga mgawanyo wa hizo pesa walikuwepo?

Kibaya zaidi kwa nini hawawataji hao watu kwa majina? Leo unajiita mpambanaji sasa unapambana na nani wakati mtu unayemtuhumu unamficha? inamaana unapambana na kivuli?

Mwembe Yanga, DK. Slaa na kundi lake waliwataja mafisadi kwa majina na hata Rais wa nchi alikuwemo, hao ndio wapambanaji, leo hawa ndg zaidi wanaimba pambio ambazo ni sawa na cinema ya kihindi kwa kushupalia kitu ambacho hata wao hawakijui.

Wameshindwa kuyaendeleza majimbo yao, matokeo yake wanatapatapa kwa uoga wa kubwangwa 2010.

Wanakyela jiandaeni kusoma hoja za Mwanakijiji kupitia RAI na TAZAMA TANZANIA.
 
You are Very Much Obsessed with Zitto Man Mpaka UNABOA, wapi jamaa kamtaja Zitto? Wakitajwa Wapinzani basi wewe Mpinzani unayemjua ni Zitto, come on mkuu I believe you could have done better then this

- Unajua mkuu ni afadhali kuwa obsessed na kiongozi wa taifa, kuliko kuwa obsessed na mimi kama ulivyo, maana unatia kinyaa sana! siku moja unasema hutaki personal na mimi na kulia lia kila mahali halafu within minutes huyo unarudia matapishi yako tena na kunitafuta tena, vipi una tatizo gani mkuu nikusaidie?

- Anyways, wapiganaji soon wataishika CCM tena kichwani, dalili ziko wazi kabisaa kwa jinsi mafisadi na mawakala wao wanavyohangaika toka ile stupid NEC, wanaopigania haki za wananchi hawawezi kushindwa daima na wale wanafiki pia watashindwa!

Lakini wapiganaji wa kweli 11 watadumu na wataishika CCM kichwani tena very soon, maana wananchi wa Tanzania wanaamuka kila siku ya Mungu, na Mungu awabariki wapiganaji wadumu, katika kutuongoza kwenye mwanga wa uhuru wa kweli!

Respect.

FMEs!
 
Mkuu MM hapa umenena kweli. Hata mie nimekuwa nikijiuliza kama kweli hawa so called wapambanaji wanaweza kushinda hii vita ndani ya SISIEMU. Wale walio hodhi madaraka ndani ya SISIEMU hawaonyeshi kama wanajali kuhusu hii vita. Hii vita kikomo chake ni kuwaondoa fisadiz ndani ya SISIEMU lakini so called wapambanaji wanaweza kujikuta wanaondolewa ndani ya Chama chao in one way or another.
 
Mzee Mwanakijiji,

Hii makala yako iko kwenye gazeti la TAZAMA leo.

Huku vijijini sisi tulishaijadili vya kutosha. Nimeona majembe ya Rev. Kishoka pia, wacha nichapishe nayo na tuendelee kuelemishana huku vijijini.
 
Jitahidini kutumia kanuni ndogo tu ya fizkia ya NEWTON.Utagundua huwezi kupigana na ufisadia ukiwa ndani ya sisiemu.
 
- Kaanza Rais wa Jamhuri kwanza kukubali kuwa joto ya wapiganaji sio mchezo ndani ya CCM na taifa, then kafuatia Makamba, and then akaja Chiligati, Guninita, mwisho wote watakuwa hawana choice,

- Halafu naomba kurekebisha hapo kwamba si kweli kuwa Mengi anatumiwa na wapiganaji, isipokuwa ukweli ni kwamba Mengi ndiye kiongozi wa wapiganaji, na sasa tulipofikia hakuna kuangalia nyuma wanaotaka maneno maneno, tunawaacha nyuma, Rais amekubali, katibu wa CCM ambaye ndiye hasa kiongozi wa mafisadi, amekubali sasa nani aliyebaki?

Mungu Awatangulie Wapiganaji.

Respect.

FMEs!
 
Huyu Mengi kila ninapomfuatilia mienendo yake anaonekana kuwa mtu wa kujipendekeza kwa wenye mamlaka, mtu wa visasi, "a man of the people" n.k.

Katika vita hii dhidi ya ufisadi tabia zake hizi hasa anapojifanya kuwa swaiba wa JK (sijui tangu lini na sijui kuliko RA!!) na kutaka watz tuamini JK ni mtu safi sana na anatuonea huruma sana watz.

Vyombo vyake vya habari viko mstari wa mbele kumuandama Mkapa na akina EL. Ninachojiuliza kila siku wakati Benn yuko ikulu na EL anaiongoza sirikali Mengi angethubutu kucheza huu mchezo wake wa kinafiki anaoufanya sasa. Thubutu...! Kwani vyombo vyake vya habari havikuwa msaada kuwaweka akina Benn Magogoni!!

Sasa hivi anajifanya yuko mstari wa mbele ktk hii sanaa ya akina JK ya kilimo kwanza (ambacho mafanikio yake yako kwenye picha za video wakati wakazi wa vijiji taklibani 12 elfu vya tz wakitaabaka na ufukara uliopindukia). Tunafaham hakuna cha kilimo wala nini hapa, ni kampeni tu za 2010 kwanza. Kilimo bila viwanda vya ndani wala masoko ya uhakika uliona wapi!!

Tena najiuliza kwa madudu aliyoyafanya JK tangu awe ktk nyadhifa za kisiasa, tukiisha ipiga chini CCM, mnafiki Mengi ataendelea kutufanya kama mazuzu kwa kubeba JK kama malaika wa nuru!?

Mengi alitutajia orodha ya waarabu wa tz tena watano tu ndo tuamini ni mafisadi, this is nonsense. Hivi Mengi anayajua mateso tunayoyapata vijijini na hawa ma VEO, WEO, wenye viti wa vijiji na madiwani wa CCM na marafiki zao? Siwasafishi hawa mafisadi wa Mengi ila ni dhahiri hawa waaarabu kwa namna moja au nyingine waliwahi bugombana na Mengi kwa sababu hasa za kibiashara (biashara halali au sio halali ni swala jingine).Ni jambo baya sana TBC "kutekwa" na hawa waarabu ila hilo halihalalishi Mengi kuelekeza vyombo vyake vitumiwe na nani na nani wasituvimie kama inavyoonekana sasa.

Tabia ya Mengi kuchokoza watu alafu anakimbilia kwenye uvungu wa JK uiache. Kama kweli Mengi si mnafiki basi vita hii ipigane bila kubagua watu. Simama kama wafanyabiashara wenzako walivyosimama (muone Freeman, mzee Ndesa n.k).
 
Mkuu FMES

Na wakuu wengine naomba kuungana na Mzee Mwanakijiji kuwa watashindwa kwa kuwa mbinu wanayoitumia siyo kwa maslahi ya watanzania wote.

Waliku wapi wakati NBC inauzwa?waliku wa wapi wakati Mkapa anauza Kiwira?hawa wapiganaji feki wasiyo na tija

Kimsingi wanatumia vibaya Pesa za wavuja jasho!

wapiganaji wa kweli wataendelea kutambulika kwa michango yao ambayo ni moto,wapiganaji wa nchi kavu(ni wanajamii forums).Hatuonekanani tukijipitisha ila tunawapa watu kile kitu wanataka na watu wanangamia !

Naam ,nawambieni watashindwa!

Hivi mkuu madela wa madilu yupo wapi?miss you guys..Kada Mpinzani na wale ambaoni wapiganaji...

Gembe
 
Huyu Mengi kila ninapomfuatilia mienendo yake anaonekana kuwa mtu wa kujipendekeza kwa wenye mamlaka, mtu wa visasi, "a man of the people" n.k.

Katika vita hii dhidi ya ufisadi tabia zake hizi hasa anapojifanya kuwa swaiba wa JK (sijui tangu lini na sijui kuliko RA!!) na kutaka watz tuamini JK ni mtu safi sana na anatuonea huruma sana watz.

Vyombo vyake vya habari viko mstari wa mbele kumuandama Mkapa na akina EL. Ninachojiuliza kila siku wakati Benn yuko ikulu na EL anaiongoza sirikali Mengi angethubutu kucheza huu mchezo wake wa kinafiki anaoufanya sasa. Thubutu...! Kwani vyombo vyake vya habari havikuwa msaada kuwaweka akina Benn Magogoni!!

Sasa hivi anajifanya yuko mstari wa mbele ktk hii sanaa ya akina JK ya kilimo kwanza (ambacho mafanikio yake yako kwenye picha za video wakati wakazi wa vijiji taklibani 12 elfu vya tz wakitaabaka na ufukara uliopindukia). Tunafaham hakuna cha kilimo wala nini hapa, ni kampeni tu za 2010 kwanza. Kilimo bila viwanda vya ndani wala masoko ya uhakika uliona wapi!!

Tena najiuliza kwa madudu aliyoyafanya JK tangu awe ktk nyadhifa za kisiasa, tukiisha ipiga chini CCM, mnafiki Mengi ataendelea kutufanya kama mazuzu kwa kubeba JK kama malaika wa nuru!?

Mengi alitutajia orodha ya waarabu wa tz tena watano tu ndo tuamini ni mafisadi, this is nonsense. Hivi Mengi anayajua mateso tunayoyapata vijijini na hawa ma VEO, WEO, wenye viti wa vijiji na madiwani wa CCM na marafiki zao? Siwasafishi hawa mafisadi wa Mengi ila ni dhahiri hawa waaarabu kwa namna moja au nyingine waliwahi bugombana na Mengi kwa sababu hasa za kibiashara (biashara halali au sio halali ni swala jingine).Ni jambo baya sana TBC "kutekwa" na hawa waarabu ila hilo halihalalishi Mengi kuelekeza vyombo vyake vitumiwe na nani na nani wasituvimie kama inavyoonekana sasa.

Tabia ya Mengi kuchokoza watu alafu anakimbilia kwenye uvungu wa JK uiache. Kama kweli Mengi si mnafiki basi vita hii ipigane bila kubagua watu. Simama kama wafanyabiashara wenzako walivyosimama (muone Freeman, mzee Ndesa n.k).

Mtu mhuni ambaye hawezi kuishi na familia yake siku zote huwa anaonekana ni mnafiki..

Mie simi kabisa ila watashindwa!
 
Mkuu FMES

Na wakuu wengine naomba kuungana na Mzee Mwanakijiji kuwa watashindwa kwa kuwa mbinu wanayoitumia siyo kwa maslahi ya watanzania wote.

Waliku wapi wakati NBC inauzwa?waliku wa wapi wakati Mkapa anauza Kiwira?hawa wapiganaji feki wasiyo na tija.............

Laiti ungelijua..............hii vita si rahisi hivyo.....fuatilia rekodi ya mpiganaji kule NBC ndio utaelewa........
 
Yote yasemwayo hapa ni kweli tupu. Kitakachotokea ni kuwa hawa mabwana hawatachaguliwa ndani ya CCM yenyewe kuwa wagombea katika majimbo yao ya uchaguzi mwaka 2010. Watabwagwa vikali na watashangaa na watakuwa wameshachelewa.

Kitakachowasaidia ni kama watasoma ishara ya nyakati sasa na kubadilika kwani muda bado wanao.
 
Back
Top Bottom