Pamoja na faida kubwa mabenki ya Kenya, mikopo chechefu yatishia uimara wake. Benki zetu kubwa mbili hazifanani nao?

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,822
Taasisi ya Moody's inayohusika kutoa muono kwenye soko la mikopo na madeni imebadilisha maoni yake kuhusu hali ya mabenki ya Kenya kutoka imara mpaka hasi ikitoa tahadhari juu ya kiwango kikubwa cha mikopo chechefu na isiyofanya vizuri pamoja na faida kubwa na mtaji imara ambacho mabenki ya Kenya yamerekodi.

Kiwango cha mikopo chechefu nchini Kenya kimepanda kwa dola 890.7m na kufikia $ bilioni 4.1 ndani ya miezi 12 sawa 14.8% ya mikopo yote iliyotolewa.

Hali ya uongezekaji wa mikopo chechefu unaakisi hali ya kiuchumi nchini Kenya kutokana na wakopaji wengi kupata changamoto za kiuchumi ikiwemo viwango vikubwa vya riba, mfumuko wa bei, upungufu wa hela ya kigeni, Serikali kubana matumizi ya manununuzi na kucheleweshamalipo pia kushuka kwa mauzo ya bidhaa na huduma kwa ujumla.

Nchini, benki za NMB na CRDB wametengeneza faida ya trilioni 1 huku NMB ikivunja rekodi yake yenyewe na kufikia faida ya bilioni 542 mwaka 2023.

Hali za kiuchumi Kenya na Tanzania hazijaachana sana ikiwemo upatikaji wa fedha za kigeni. Magwiji hawa wawili wakae mguu sawa? Mabenki ya Marekani yalirekodi faida kuu kwa kuwakopesha mikopo ya nyumba wakopaji waliowalegezea sifa na kuwaletea anguko la uchumi la mwaka 2008 na kusababisha janga kwa dunia nzima.
 
Back
Top Bottom