Pamba Soccer Team

Pamba.jpg
 
Halafu hii picha chanzo chake ndo mimi, nina hardcopy yake, kuna mshikaji aliiomba mwaka jana mara ghafla bin vuu ikatapakaa kila mahali kwenye internet. Dang, shoulda copywritten it!!
Kuna mshikaji alikuwa anauza magazeti pembeni ya Tivoli sinema alikua anaitwa Philipo, kwa walioishi Mwanza kipindi hicho early 90s, nadhani ndio nilinunua kwake hii picha.
 
Wana Mwanza wote. Turudisheni timu yetu ya Pamba kwenye Super League. Je, tuanzie wapi?
Tunaweza kuirudisha Pamba. Tunaweza kuanzaia humu humu kwa sababu kukutana wote itakuwa ngumu. Harakati zinaweza kuanzia hapa kisha tukapata mwakilishi akajaribu kuongea na wahusika. Kwa mkoa wa Mwanza na 'diaspora' yake tunaweza kabisa kufanikisha kuifufua timu. Nashauri tuchague siku na muda mwafaka tukutane humu JF, tujaribu kujadiliana jinsi ya kuweza kuifufua Pamba. Najua hatuwezi kubeba mzigo wote wa kuendesha timu lakini tunaweza kuwa chanzo/catalyst ya kuhamasisha wana Mwanza kuifufua hii timu.
 
TP LINDANDA WANAKAWEKAMO, WANA KISHAMASHAMAPANDA. napendekeza J.mosi tukutane humu. inaniuma sana kuona timu ambayo mwaka 1990 nilikimbia kwa miguu kutoka Pasiansi hadi CCM Kirumba tukisindikiza timu yetu ikitoka Uganda.
 
Wanakishamapanda ni Toto Africans mkuu...
Pamba ndio walikuwa Tout Puisant Kawekamo......R.I.P Domonick Chilambo
 
Zungumzeni na mkuu wa mkoa muanzishe account maalum halafu mnaandaa mpango wa kuchangia tigo pesa, mpesa etc tutawachangia
Mkuu wa mkoa ni mtu wa kupita, unaweza kuzungumza naye leo kesho akahamishwa.Inatakiwa jitihada za wananchi wa kawaida tu, naamini tupo wengi wenye kupenda kuona hadhi ya Pamba ikirudi.
 
Hii Picha imenitoa Machozi
nauhakika katika mechi hii nilikuwa ndani ya nyumba, jukwaa kuu.
kuanzia kuchoto kwenda kulia waliosimama
Madata Lubugisa
Rajabu Musoma
Beya Simba
Nteze John
Kitwana Suleiman
Fumo Felician
Nimemsahau (naomba nikumbushwe)
Paul Rwechungura

Waliokaa kuanzia kushoto
George Gole
Khalfani Ngasa
Ali Bushiri
Nimemsahau (Naomba nikumbushwe)
Mao Mkami
Salehe Mohamed
Nimemsahau (Naomba Nikumbushwe)
Niko Bambaga.
 
Mkuu wa mkoa ni mtu wa kupita, unaweza kuzungumza naye leo kesho akahamishwa.Inatakiwa jitihada za wananchi wa kawaida tu, naamini tupo wengi wenye kupenda kuona hadhi ya Pamba ikirudi.

Hiyo timu iko chini ya akina nani siku hizi? Niko tayari kushiriki kwenye kuifufua.
 
Hiyo timu iko chini ya akina nani siku hizi? Niko tayari kushiriki kwenye kuifufua.
Sijui iko chini ya nani. Tuchagueni siku na muda tukae humu tujadili kisha tunaweza kupata wawakilishi wa kwenda kuwasaka wahusika na kuongea nao. Kampeni inaweza kuanzia humu, tusiishie tu kutaja majina ya wachezaji wa zamani. Njia bora ya kuwaenzi hao nyota wa zamani ni kuifufua timu na kuhakikisha inarudisha hadhi yake na hadhi ya mkoa.
 
Naomba umoderate hicho kikao
kifanyike weekend
tuma matangazo ya kikao majukwaa yote kama inawezekana.
 
kipindi hicho napiga kitangiri primary nilikuwa sikosi mechi hadi matizi ya pamba.... ila nilikoma na stik za bubu
 
OK. Mimi ndio Mleta Mada hii. Kwanza kabisa niwashukuru wote mliochangia kwa kutoa maoni na kuonyesha upendo na hamu kubwa ya kuirejesha timu yetu ya Pamba. Nafikiri JUMAMOSI HII, KUANZIA SAA NNE ASUBUHI TUKUTANE WOTE HAPA JF ILI TUJADILI HILI SUALA. Pia wataarifu Wananzengo wote na wale wote wanaopenda soka lenye kiwango cha kimataifa wawasiri kikaoni bila kukosa. Kama unamawasiliano na wachezaji wa Pamba Soccer Team wa zamani (walio Hai), basi wape taarifa. Mimi binafsi naanza na rafiki wangu Nteze John Lyungu ambae anaishu USA kwa sasa hivi. Nia tunayo, Uwezo tunao, na sababu tunayo ya Kuirudisha Timu yetu na heshima ya mkoa wetu. TAHADHARI... HAKUNA ULAJI HAPA. NGUVU YA WANANZENGO IPO IMARA KUHAKIKISHA TUNAJITOLEA KIMAWAZO, KIFIKIRA, NA HATA KIFEDHA IKIBIDI. Lakini sharia mkononi...PERIOD
 
Asante sana, saa nne kamili ntakuwa ndani ya nyumba.
 
Tuko pamoja wananzengo...nimekumbuka miaka hiyo nilikuwa na rafiki yangu Zuberi Msuya mitaa ya Mecco, Nyakato, kila Pamba walipokuwa wanacheza alikuja na redio yake tunakaa kwenye msingi na kufuatilia mpambano kupitia Radio Tanzania Dar es Salaam wakati huo
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom