Palma Msumbiji, kitovu cha mafuta na gesi haipo tena

Genecandy

JF-Expert Member
Dec 13, 2017
491
882
Waasi wameamua kumaliza kabisa sasa washaingia wilaya ya Palma ambapo ndo kitovu cha mafuta na Gas toka Juzi mpka sasa washachoma kila kitu cha serikali kambi ya jeshi ipo mikononi mwao kituo cha polisi pia hospital na offic zote za serikali zimetiwa moto

Raia ambao hawakuwahi kukimbia wamechinjwa na kama kawaida yao wakiingia sehemu cha kwanza ni kuangusha mitambo ya mawasiliano wanapiga bomu mitandao inakata ndio wanaanza shughuli zao za kikatili hvyo toka juzi hakuna mawasiliano Palma!!

Watoa habari wanatumia WI-FI Ya kampuni kwenye ma camp yao ambayo bado hayajapatwa dhahama yoyote na wananchi wote washakimbilia huko kwenye macamp ya wazungu kupata hifadhi!!

Hivyo mpaka sasa boda ya Mtwara imefungwa hakuna namna ya kuingia Msumbiji kwa kupitia Mtwara labda kuzungukia Masasi na Songea au Malawi maana boda zote zilizokuwa nyepesi kupita hao mbwa washazifanyia maasi kama kuteka magari na kuua Raia!!

Hali ni tete sana kwa majirani zetu kwa huo mkoa wa Cabo del Gado Mmarekani + Mfaransa ndio wawekezaji hapo japo Mmarekani ambaye alijiita ANADARKO anajifanya kujitoa na kusema kazi kamuuzia mfaransa ambaye ni TOTAL ndio mmiliki kwa sasa!!

Kuna voice note zinasambaa watu wakiomba msaada maana serikali bado haijatoa neno mpaka sasa japo wanaongea kireno ntajaribu kuzi attach kama zitakubali!!

Nimeshindwa kuziweka hizo audio anaeweza anifate inbobo nimtumie aje aziweke!! Tuombee nchi yetu na majirani zetu jamani hali ni tete!! Asanteni

 
Yaani ukiwasikiliza marais/ viongozi wa nchi fulani wanavyoongea wakiwa nchi za wenzao utadhani nchini kwao wanakunywa maziwa bombani wakioga asali mtoni.

Hali ya Msumbiji na hicho kikundi kinasikitisha na kufikirisha sana. Yaani bado kuna watu wanafanya mambo yale yale ya kikoloni kwa waafrika wenzao!
 
Umeweza ku attach video, umeshindwa ku attach audio🤔🤔🤔⁉️⁉️⁉️⁉️
 
Back
Top Bottom