Kyodowe
JF-Expert Member
- Mar 6, 2013
- 1,242
- 1,378
Kati ya mambo yaliyowahi kutia fora enzi za ukoloni na historia ya kuanzishwa kwa koloni la Tanganyika, ni ile mikataba feki iliyotengenezwa na Karl Peters na kisha kusainiwa na machifu bila hata wao kujua ni nini kilichoandikwa. Kuna uthibitisho usioukwa na shaka kuwa, machifu hawakuelewa walichofanya wakati wakisaini karatasi hizo. Wao walifikiri kuwa wameahidiwa ulinzi kutoka kwa mtawala wa mbali ambaye labda siku moja atakuwa na faida kwao lakini hawakuelewa kwamba wametoa kibali kwa mgeni kutawala nchi. Na ili kuonyesha kuwa Karl Peters alikuwa na "good faith" kabla ya kusainiwa mkataba aliwaandalia mvinyo wa kijerumani na kuwapongeza kwa zawadi za dhahabu, manukato n.k. Hatimaye Tanganyika ilijikuta ni koloni la Wajerumani.
Anyway, ni takribani miaka isiyopungua 120 na sasa Karl Peters mwingine maarufu kama Professor John L. Thornton ameandika historia nyingine kwa style ile ile ya 'good faith'.
Labda sitashangaa kwa kuwa wahenga waliwahi kunena 'What goes around comes around'. Kutoka kudai nyumba ($ 190 billioni) hadi kupewa tofali ($300 milioni).