Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,417
Kuna wakati unaweza kumuomba mwanamke mtoko (dates) kwa ajili ya kufahamiana zaidi na kubadilishana mawazo au uzoefu halafu anakwambia "sorry I'm in a relationship" lakini hataishia hapo atakwenda kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii (Social Media) na kuweka ujumbe kama ...."in a relationship or Engaged" na mbaya zaidi mapicha picha ya huyo mwanaume ambaye hata hawajafikia hatua ya kupanga mipango ya ndoa yatakuwa yakibadilishwa kila muda kwenye ukurasa wake wa ujumbe.
Wakati mwingine nabaki nikijiuliza hivi hawa dada zangu wamelogwa au wanaumwa ugonjwa gani.
Naomba niwaambie dada zangu mnaosoma hapa amkeni msiwe wajinga kiasi hicho. Ukweli ni kwamba ni Mpaka pale mwanaume utakapofunga naye ndoa ndiyo unaweza kusema ni wa kwako. Mwanaume kabla ya kufunga ndoa hata kama kakuvisha pete ya mamilioni bado hajakuwa wa kwako. Unapojifunganisha naye na kujitangaza kwamba uko na mtu tayari, mwenzako yuko available na bado anadodosa kutafuta mwenye vigezo kukuzidi na huenda Bahati hiyo ikamuangukia mwingine.
Hamjawahi kusikia wanawake wenzenu waliochwa na pete za uchumba na pete za ndoa wakavishwa wengine, achilia mbali wale walioachwa kanisani au majumbani mwao wakisubiri Bwana aje wafunge ndoa na asionekane mazima.
Kama uko na mwanaume uaminifu ni lazima lakini haikunyimi nafasi ya kukutana na wanaume wengine na kuzungumza nao kwani wakati yule anauweka usiku wapo ambao wako serious na wameshakuona una meet vigezo vyao na wanachotaka ni kupata nafasi ya kusikilizwa.
Ushauri wengu kwenu dada zangu ni kuwaomba kupunguza mbwembwe za mitandaoni. Kujifunganisha na mwanaume ambaye hata kwenu hajulikani ni kujitia mikosi, wanaume siyo wa kuaminika kiasi hicho. Kufanya hivyo ni kujizibia nafasi yako ya kuonekana na wanaume wengine walio na nia njema na wewe.
Mwenye masikio na asikie….