Pajue Iringa kwa kupitia picha


Sasa tutoke kidogo kati kati ya mji sasa tusogee pembeni kidogo ya mji,, hapa nipo mtaa wa kijiweni ,, na hivi ndivyo iringa CBD inavyoonekana ukiwa huku kijiweni
 
Natamani kupajua vizuri Kilolo. Hali ya hewa, shughuli za uchumi na mzunguko wa pesa
 
Kwa tako sijapaona nimekula Ice cream pale sana nikiwa mtoto. I wish pia kuiona Tosamaganga kwasasa inafananaje. Huu mkoa nina historia nao sana. Nimesoma na kuishi Iringa. Ahsante Mkuu, vipi na mmea mnalima?
Zile keki na Juice za mapera hukunywa?

Tunakumbuka Ice Cream na Mtindi kwa keki!
 
Kwa wastani range ya bei ya kiwanja 20m kwa 20m kwa maeneo ya kando ya mji ni kiasi Gani? Vp mashamba pia ni bei Gani kwa wastani?
Ukiwa na 4 au 3.5 unapata katika maenro ya kitasengwa dk 15 toka katikati ya mji kwa bajaji
 
Imebarikiwa kwa upande wa hali ya hewa na udongo unayo- support kilimo cha mazao mbali mbali lakini pia uwepo wa misitu mikubwa kama sao hills inapelekea mkoa kuwa na mvua zisizo sua sua ,, so ukiangalia hivi ndiyo watu huvitafsiri kama baraka
Pia mji una hali bora sana ya usafi nadhani Iringa. Cbd ndio mji msafi kuliko yote Tanzania
 
Kuna maisha rahisi sana huko...nyumba rahisi za tofali za kuchoma.
 
"Cha mafinga" kinapatikana wapi?
 
Mkuu vipi waganga wa huko?
Nasikia wapo vizuri
 
Natamani kupajua vizuri Kilolo. Hali ya hewa, shughuli za uchumi na mzunguko wa pesa
Hali ya hewa ni baridi sana ,, kwani kadri unavyoiacha iringa mjini kuelekea kilolo mwinuko wake huongezeka na kufanya wilaya ya kilolo kuwa na baridi zaidi ukilinganisha na iringa mjini

Shughuli kuu kwa kilolo ni kilimo ,, kilolo wanafanya kilimo cha miti kama vile pine kwa ajili ya mbao , gyms kwa ajili ya mbao na nguzo za umeme , milunda kwa ajili ya kusupport issue za ujenzi kama vile kutengenezea majukwaa na nk

Kilimo cha mazao , kama vile mahindi na maharage pia vinafanyika kwa wingi katika wilaya ya kilolo .

Pia Unaweza fanya kilimo cha matunda kama vile apples , pindigesi na mapeasi kwani hali ya hewa ya ubaridi ni very favourable kwa aina hizo za matunda .

Lakini pia shughuli za ufugaji pia zina fanyika kwa kiwango kikubwa tu ndani ya wilaya ya kilolo ,, kuna ufugaji wa ng'ombe wa maziwa mbuzi , kondoo na nk

Muzunguko wa pesa ni mzuri kwa kiasi chake ukichangizwa na biashara ya mbao iliyotamadadi kuanzia wilaya ya kilolo kuelekea ndani ndani mpaka kidabaga ,, kwani biashara ya mbao imekuwa ikiwavuta wafanya biashara wengi wanaofanya shughuli za ulanguzi wa mbao toka pande mbali mbali za nchi na kuchochea mzunguko wa pesa ndani ya kilolo lakini pia biashara mahindi , maharage na usafirishaji ni miongoni mwa biashara zinazochochea mzunguko wa pesa kuwa mkubwa ndani ya kilolo .

Asante natumaini nimejibu kwa namna fulani swali lako
 
Kigonzile huwezi kupakumbuka Tena ht kiwanja hupati🤣

Ila nimerudi nimekuta kumevafirika iringa imekua sana aisee
 
Pia omba msaada kwa akina sie ili mambo yaende sawa. Kilolo ni kubwa na tamu sana. Kuazia Bomalang'ombe, kidabaga, lulanzi,kitowo, pomerini, njoo iringa yenyewe. Pawaga, kidamali, magubike. Kalenga, Ifunda, kiponzero,. Malangali, Nkororo, Kate huko kuna hela siyo mchezo. Ndala inguluvi ya tumatite lunofu. Kamwene iringa yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…