PostGE2025 Padri Kitima: Ninaweza kuuawa hata leo, baada ya taarifa hii

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
"Tulifanya kikao hapa tuliwashauri serikali tarehe 30 mwezi wa nne usiku wake ambapo waliamua kuniua mimi, ndiyo tulipitisha yale maazimio na uzuri yamekabidhiwa serikalini mwezi wa nane tarehe 27. Pamoja na kwamba ilikuwa tuyakabidhi siku iliyofuata wakataka kuniua Mungu bariki nikapona, najua naweza nikauawa leo baada ya taarifa hii."

"Tulisema haya yasipozingatiwa nchi haitakaa salama tunaelekea pabaya. Tuliongea taifa linaelekea pabaya tulishaona, lakini kupuuza viongozi wa dini ni hatari sana kwa sababu viongozi wa dini hawana maslahi binafsi kwenye taarifa zinazohusu uhai wa mtu.

Kwahiyo kusema watu wamenunuliwa si kweli, kuna matatizo yanayoendelea ya msingi ya nchi ambayo hayajashughulikiwa, watu wanatekwa, wanapotezwa, wanauawa."

Padre Charles Kitima, Katibu mkuu wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 01, 2025.
 
Walijua nini wanapanga, haishangazi kilichotokea
Ndiyo maana wamesema waliouawa wako mbinguni maana wamepigana vita vya msalaba
We nae upumzike sasa!!

Yaani upo kama fisi unadanga na kuzurura jf Kila mtaa ili mradi tu kutafuta nyuzi zinazoikosoa serikali ili uandike mashudu.

Au dau lako huko Rumumba ni kubwa siyo kama wenzio wa buku 7?
 
Lumumba*
 
Uchawa hadi jina likikosewa unalisafisha.

Ibaki Rumumba hivyo hivyo. Hutaki kumbatia transfoma.
Huo mtaa wa Lumumba zilipo ofisi za CCM ulipewa jina hiloekumuenzi aliyekua waziri mkuu wa DRC Patrice Lumumba
 
Padri anajua kwamba nchi inaongozwa na Human Life Rangers. Hawa wanakaribiana na wale wildlife rangers wa wanyama pori. Wale Wildlife rangers ni wema sana, wanawinda wanayama wanatupa kitoweo. Je hawa wanaowinda binadamu wanapeleka wapi watu wetu waliokufa?
 
Walikuwepo wenzie wengi sana humu Wala yeye hawezi kuwa wa kwanza Wala wa mwisho.

Huyu gallow bird Namwonea huruma anakula kwa shida sana kama Hela yenyewe ndiyo anaipata kwa kuwatetea Hawa madhalimu wa sisiem.
Kijana,mimi mkulima,sina dhiki,nimeajiri watu watatu na Wana familia
Mimi nipo kwa maslahi ya nchi
Vijana wanatumika na wapuuzi kwa agenda zao chafu
 
"Tulifanya kikao hapa tuliwashauri serikali tarehe 30 mwezi wa nne usiku wake ambapo waliamua kuniua mimi, ndiyo tulipitisha yale maazimio na uzuri yamekabidhiwa serikalini mwezi wa nane tarehe 27. Pamoja na kwamba ilikuwa tuyakabidhi siku iliyofuata wakataka kuniua Mungu bariki nikapona, najua naweza nikauawa leo baada ya taarifa hii."
"Tulisema haya yasipozingatiwa nchi haitakaa salama tunaelekea pabaya. Tuliongea taifa linaelekea pabaya tulishaona, lakini kupuuza viongozi wa dini ni hatari sana kwa sababu viongozi wa dini hawana maslahi binafsi kwenye taarifa zinazohusu uhai wa mtu.
Kwahiyo kusema watu wamenunuliwa si kweli, kuna matatizo yanayoendelea ya msingi ya nchi ambayo hayajashughulikiwa, watu wanatekwa, wanapotezwa, wanauawa."

Padre Charles Kitima, Katibu mkuu wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 01, 2025.
Mbaya zaidi, Serikali bado inaendelea kuteka na kupoteza watu kama kawaida!
 
Back
Top Bottom