Padre amwagiwa Tindikali huko Zanzibar

Padre amwagiwa Tindikali huko Zanzibar

Status
Not open for further replies.
Wale mabinti wa kizungu walivaa vimini ikasemwa ndio sababu ya kuwamwagia - Sasa huyu Padre nae amevaa nini???
Waislam tuache ujinga wa kushikiliwa vichwa kwa manufaa ya wachache......huu si ubinadamu hata kidogo wala hakuna thawabu kwa matendo haya ya kinyama
Haya mambo yatatugharimu sana hata kwa vizazi vijavyo
 
...znz ni kisiwa cha udini...!
 
Noma sana!! tusihusishe na uislam,huo ni ushenzi, ugaidi na uoga,kama kwingine tu.mboni watu tunachanganyika vizuri tu.
 
Huu ni ushamba na ujuha, they need to be civilized...poor zanzibaris ------
 
Padri wa kanisa
Katoliki Parokia ya Cheju
Zanzibar,Joseph Mwangamba
amemwagiwa tindikali na kujeruhiwa
usoni na kifuani
source..East Africa Radio.


Hapo ktk red umekosea, anaitwa Ancelmo Mwang'amba

SOURCE: ITV - Farouq Karim
 
Hii mbaya sana jamani!

Bado tunasema kuna AMANI kwa namna hii.

Mbaya sana hii!
 
hatari ni hatari lakini salamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Wale mabinti wa kizungu walivaa vimini ikasemwa ndio sababu ya kuwamwagia - Sasa huyu Padre nae amevaa nini???
Waislam tuache ujinga wa kushikiliwa vichwa kwa manufaa ya wachache......huu si ubinadamu hata kidogo wala hakuna thawabu kwa matendo haya ya kinyama
Haya mambo yatatugharimu sana hata kwa vizazi vijavyo


Nimeipenda sana post yako mama D
 
Last edited by a moderator:
hiyo ndo zanzibar bwana,kisiwa kinachoharibiwa sifa zake za amani na utulivu na wapumbavu wachache na serikali dhaifu na legelege ya kisiwani inashindwa kuwafanya lolote,hadi wamwagiwe tindikali mama zao ndio washtuke,kisiwa hchi kinapoelekea siko kabisa
 
Kumwagiwa acid ni issue,lakini kuna wengine hapa wakimwagiwa wengine acid wanakuaga na maneno mabovu sana,
 
Tunasubiri matmko makali na ahadi kem kem kutoka kwa jk na serikali ya CCM as usual.
 
sitakanyaga tena Zanzibar hata kama watakuwa wanagawa hela , potelea mbali !
 
Nina mashaka na Mungu anayeabudiwa na Waislamu. Sithani kama ni Mungu yule tuaminiye ndo Muumba Mbingu na Dunia. Nadhani hawa jamaa wana Mungu wao
mkuu; ishu hapa si waislam wala wakristo, Ishu hapa ni makundi ya uhalifu ambayo hayajadhibitiwa. Ikumbukwe kwamba uhalifu hufanywa na watu na watu hawa wanaweza kuwa na dini zao ila sio dini hizo zinazowatuma watu kufanya uhalifu.Muhalifu bila kujali dini yake ni muhalifu tu na anayedhuriwa bila kujali dini yake ni lazma atetewe.Binafsi naamini watu wanaoyahusisha matukia haya na dini fulani (yoyote iwayo) ni wale wale wanaoyafanya matukio husika ambao mimi naamini lengo lao ni kuchochea migogoro ya kidini.Kwa hiyo wanapomdhuru kiongozi hivyo halafu wakawa wanachochea "watakuwa ni watu wa dini fulani", na siku nyingine anadhuriwa kiongozi wa dini nyengine; basi utasikia tena wanachochea "Watakuwa ni wale wa dini nyengine" basi mgogoro unakuwa na muhalifu anakuwa kafikia lengo.Nadhani sisi tujaribu kujiepusha kuwa sehemu ya kumfanya muhalifu kufikia lengo la kuichonganisha jamii. ANAYEFANYA UHALIFU ABEBE MSALABA WAKE MWENYEWE.
 
Padri mmoja mjini Zanzibar amemwgiwa tindikali sehemu za usoni na kifuani..source rfa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom