Pablo aletewa kocha mpya Simba

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,786
4,421
1645604990763.png

Picha: Arno Buitenweg akisalimiana na mwenzake

KIKOSI cha Simba kilichokuwa uwanjani mjini Niamey, nchini Niger usiku wa Feb 20 ilipokuwa ikimalizana na US Gendermarie, kinajiandaa kuanza safari kuifuata RS Berkane ya Morocco, huku kocha mkuu wake, Pablo Franco akimleta fundi mpya.

Mbali na kuleta fundi mpya kutoka Hispania anayejua soka la tiki-taka kama linalopigwa Manchester City ya Pep Guardiola, lakini kocha huyo ameanza mapema kuisoma RS Berkane ya Morocco watakayovaana nayo Jumapili hii katika mfululizo wa mechi za makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tuanzie hapa! Kocha Pablo amependekeza kuboreshwa kwa benchi la ufundi la kikosi hicho kwa kuongeza nguvu ya makocha wengine wawili watakaofanya kazi kwenye maeneo mbalimbali.

Kocha huyo kwanza ametaka aletewe kocha msaidizi mwingine, pia akipendekeza Mkurugenzi wa Michezo wa kuja kuongeza nguvu kikosini pamoja timu za vijana na ile ya wanawake ya Simba Queens.

Na habari za uhakika kutoka ndani ya Simba ambazo Mwanaspoti imezinasa ni kwamba katika eneo la Mkurugenzi wa Michezo, Pablo amempendekeza, Arno Buitenweg aliyewahi kufanya kazi katika timu mbalimbali kwa nafasi tofauti.

Mtaalam huyo aliyebobea kwenye soka la vijana anatajwa ni fundi wa soka la pasi nyingi maarufu kule Hispania kama tiki-taka huku akifundisha timu kutoka nchini kwao Uholanzi, Hispania ikiwamo Real Mallorca pamoja na Uarabuni.

Taarifa hiyo inaeleza Pablo amemtaka Arno kwa ajili ya kushauri na kushirikiana katika masuala ya kiufundi kwa timu ya wakubwa pamoja na kuwekeza nguvu Simba Queens na ile ya vijana ili kuzalisha wachezaji bora watakaopata nafasi katika timu ya wakubwa au kuuzwa.

Inaelezwa mabosi wa Simba baada ya kukubaliana na ombi hilo la kumleta Arno, lakini waliamua kwanza kuzungumza naye ikiwemo kumtumia majukumu atakayotakiwa kuyafanya akija nchini na kukubaliana masilahi watakayomlipa.

Japo haijawekwa wazi walipofikia, lakini kama Arno atakubaliana na majukumu hayo pamoja na maslahi atakayopata Simba atawasili nchini muda wowote kuanzia leo ili kusaini mkataba kabla ya kuanza kazi Machi Mosi 2022.

Kocha huyo aliyewahi kuinoa timu ya Ajax Amsterdam na Al Arabi SC ya Qatar na kufanya kazi na kituo cha kimataifa cha kukuza soka cha Aspire Academy, ana leseni za AFC Pro na UEFA Leseni A akifanya kazi kama kocha na Mkurugenzi wa Ufundi kwa baadhi ya timu barani Ulaya na Asia.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alipoulizwa kuhusu jambo hilo alisema uongozi upo tayari kuwapatia kila wanachohitaji benchi la ufundi ili kuhakikisha wanafanya vizuri na kufikia malengo ya klabu.

“Simba tuna malengo ya muda mrefu na kufanya vizuri katika kila mashindano tutakayokuwepo, hivyo tumejipanga kuboresha katika maeneo yote ikiwemo kusikiliza benchi la ufundi linahitaji vitu gani,” alisema Barbara mwenye kiu kubwa msimu huu kuona Simba inafika mbali katika michuano ya Shirikisho Afrika ambayo jana ilikuwa ikimalizana na USGN ya Niger kabla ya kuifuata Berkane ya Morocco.

Kocha Pablo kwa ajili ya mchezo huo ameanza maandalizi mapema ya kuwasoma Morocco hata kabla ya kuwafuata, lengo likiwa kujua ubora na udhaifu wake akimtumia zaidi Clatous Chama waliyesafiri naye licha ya hawezi kutumika katika michuano ya CAF sababu alishacheza msimu huu akiwa na Berkane.

MDACHI ALIVYO
Arno aliwahi kuwa mkufunzi wa makocha katik Shirikisho la Soka visiwa vya Balearic kisha akaajiriwa kama kocha wa Al-Arabi na kuteuliwa kocha wa timu ya taifa ya Qatar.
 
Yes that's SIMBA FC with long term strategies We want to see achieving big goals in Africa.
 
Hata Pablo naye alipokuja mlimpamba hivi hivi! Ila mwisho ndiyo hivyo tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom