Osaka Raha, Bukoba to Dar siyo gari la kupanda

Unachosema ni kweli,mwaka Jana nilisafiri nalo,wakasimamisha gari kama saa 5 wakashuka wenyewe kwenda kunywa chai bila kuwatarifu abiria.
 
Kuna Osaka nyingine ya Dar kwenda Musoma, siku ya tar 9/1/2016 nilipanda kutokea ubungo kwenda mwanza. Kuna kondakta kijana mweupe kwa mbali, alikuwa anawajibu watu vibaya sana alafu kauli za mikato. Kuna abiria alishuka nzega nusura wapigane kwenye gari; eti kisa yule abiria alimuomba konda awe anataja vituo maana ilikuwa usiku. Dah roho iliniuma sana, nusura ninunue ile kesi. Gari zao hazisumbui njiani lakini makondakta wao ni shida tupu, kuna mdada anakatisha mle ubungo na huwa anashukia kibaha, yule mdada ni bora angekuwa anafika mpaka mwisho wa safari. Naona yule ndio kidogo ana kauli nzuri kwa abiria
 
Nimecopy na kutuma ujumbe wa kwa Jafari nina hakika ataufanyia kazi. Jamaa ni mtu mstaarabu sana sema ndio ivyo unawekeza pesa nyingi unaajir mtu asiye na uchungu na pesa zako anakuharibia biashara.

Duc in Altum
 
mkuu thanx kwa info aiseeh sipandi hilo gari..!! gari yangu huwa OTTA, nikikosa hiyo basi hata princess muro..!! maana wengine kirusha ngumi ni sekunde
 
Sikia, siku nyingine kamata konda tia ngeta la maana.. Konda lazima atakuja juu/atajaa upepo.. Hapo ndio utakapo mfundisha adabu na heshima.
 
Kwa kweli wangewapasua vibofu vya haja ndogo maana kuna mji kidogo mingi kutoka Kahama -Singida mgeweza kujisaidia. Kuna kagongwa,Isaka,Tinde,Nzega,Nziba,Ibologelo, Igunga &Sheluwi kabla ya kupandisha Sekenke.
Kweli mkuu wametuonea sana ndo maana nikaleta uzi hapa ili kukemea huu unyanyasaji
 
Nimecopy na kutuma ujumbe wa kwa Jafari nina hakika ataufanyia kazi. Jamaa ni mtu mstaarabu sana sema ndio ivyo unawekeza pesa nyingi unaajir mtu asiye na uchungu na pesa zako anakuharibia biashara.

Duc in Altum
Umefanya vyema Mkuu lengo ni kurekebisha tabia za hao watu wasiojali biashara za watu
 
MABOYA NYIE,MPO ZAIDI YA 60VIJEBA VI 4VINAWAZIMISHA??NTALIPANDA NIWAONESHE MBWA HAO
 
Hao jamaa ndo tabia zao.Ila kama sikosei ITV kuna fulani huwa wanaitoa kwa ajili ya abiri wanaopatwa na shuruba kama hizo.
 
Bahati mbaya sana mtoa mada umetoa habari yako kwa ushabiki zaidi kuliko kuleta mada ili iweze kusaidia wasafiri;

1. Nilitegemea ungeweka namba za gari husika; maana ubaya wa Osaka Raha moja siyo ubaya wa Osaka Raha jingine
2. Umelalamika kutokupata fursa ya kuchimba dawa Kahama - Singida;je, magari mengine ya route hiyo hiyo kama OTTA, Murro, Mohamed, RS, Falcon yenyewe yalisimama njiani abiria wake wakachimba dawa?
3. Magari ya Mwanza - Dar huchimba dawa Shinyanga na dawa nyingine huchimba pale Singida; halafu Dodoma huku mbelembele hadi UBT; sasa Kahama - Singida tu imekuwa shida wakati gari linaenda kwa ratiba?
4. Pole hawakukuoa stakabadhi ya mzigo; ila mabasi karibu yote hutoa stakabadhi ya excess mzigo.

Hata hivyo Jafari, Hamza, Shahibu wamekusikia.

NB - Ujifunze kutokulakula na kunywakunywa unapokuwa kwenye safari ndefu.
 
Naona povu linakutoka kama dereva wa gari vile
1. Sikuweka namba za gari lakini ni Osaka Raha Hit man.. imeeleweka
2. 3. Magari yote uliyoyataja yalikuwa yanasimama kuwapa fursa abiria kuchimba dawa nimeshuhudia kwa macho yangu mwenyewe na wala si mara yangu ya kwanza kusafiri nisijue ni baada ya mda gani abiria wanatakiwa kupewa nafasi ya kuchimba dawa.
4. Kutotoa stakabadhi ya Malipo ya mizigo ni kati ya wizi walioufanya na kunisukuma kuleta uzi hapa.

NB: Haja haziletwi na kulakula hovyo ni involuntary actions za mwili na huwezi kuzuia abiria kula kisa safari na mbona wenye gari wanatoa vyakula na vinywaji? Ni vya nini kama kula ni kubaya? Na wao mbona wanakula na wanaenda haja na kuwaacha abiria. Mnapewa kazi za watu mnaleta masihara watu wanalalamika mnakuja juu. Mmenikera sana
 
Back
Top Bottom