Maisha pesa
JF-Expert Member
- Nov 6, 2015
- 681
- 630
Wasalaam wanaJF kama ilivyo kawaida huwa tunapeana taarifa na habari mbalimbali zenye lengo la kujenga. Jana nilisafiri kutoka Bukoba kuja Dar na nikapanda gari la Osaka Raha niliyoyashuhudia ndiyo yamenisukuma kuleta uzi hapa.
Kiukweli ni gari mpya wala haina tatizo lolote la kiufundi au kwa lugha nyingine niseme gari haijachakaa wala haliharibiki hovyo njiani mwendo wake wa kawaida tu hamna shida.
Tatizo linakuja kwenye tabia za madereva na wafanyakazi wa hilo gari kwanza hawana ustaarabu ukishakata tiketi basi unaonekana huna maana tena wana lugha chafu kama makonda wa daladala.
Shughuli imeanza asubuhi wakati wa abiria kupanda wanalipisha mizigo kama hawana akili nzuri mzigo wako ukizidi 20kg basi wanachaji elfu moja kwa kila kilo iliyozidi na wala hawana punguzo basi abiria kakata tiketi 60,000/= analipishwa na mzigo elfu20, 15, 30. Kibaya zaidi hawatoi risiti ya hizo hela za mizigo. Mimi niliwakomalia nijue kwanza hiyo rate ya 1,000/= kwa kila kilo imepangwa na nani? Na pili nikilipa nipewe risiti lakini waligoma almanusura niachwe stendi huku nikipewa matusi ya kila aina na kuambiwa nitarudishiwa nauli ofisini wakati gari limeshaondoka nilisaidiwa na askari aliyewaamuru kama wananiacha basi wanirudishie nauli yangu kabla hawajaondoka nipande gari nyingine. Hapo wakaona pagumu kurudisha nauli ikabidi wanipakie tu kumbe walitaka wanitapeli ionekane nimechelewa gari imeniacha.
Baada ya sereka hiyo safari ikaanza kisanga kingine kikaja kwenye kuchimba dawa duh hawa jamaa ukizubaa wanakuacha na hawajali watu wanalikimbilia gari wakati linaondoka. Tumepiga mwendo kutoka Kahama hadi Singida 302km masaa matano bila kuchimba dawa wakati magari mengine tunaona wanachimba dawa sisi ni mwendo tu hadi abiria tukaomba watusaidie lakini wapi wanajidai eti wana haraka wao wakipata kinafasi kidogo cha kupakia abiria wanaenda kuchimba dawa wanatuacha sisi abiria.
Mziki ukaja pale mtoto alipolilia kujisaidia wakamshusha halafu wakampandisha kabla hajajisaidia eti wana haraka mwishoe dogo akaaharisha kwenye gari na harufu ikasambaa gari zima lakini hawakujali kama abiria tunapata shida wakaendelea na safari hadi kelele za abiria zilivyozidi ndo wakasimamisha kwa kutupa dk5 tu almanusura tuwaache baadhi ya abiria. Aisee sipandi tena hili gari.