Orodha ya wadaiwa sugu HESLB yaibua mapya

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205



Kwa ufupi
Pia, yapo majina ya watu ambao hawajawahi kuomba mkopo na wengine walisoma nje ya nchi.



By Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Orodha ya wadaiwa sugu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), imedaiwa kuwataja wanufaika ambao baadhi walishamaliza kulipa madeni yao.

Pia, yapo majina ya watu ambao hawajawahi kuomba mkopo na wengine walisoma nje ya nchi.

Mapema wiki hii Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru, alitaja kiasi cha fedha wanazodaiwa wanufaika hao 142,470 kuwa ni Sh2.39 bilioni. Hata hivyo, baadhi ya majina yaliyotolewa katika tovuti ya HESLB ikidai kuwa ni wadaiwa sugu, wametajwa kimakosa.
 
hao bod ya mikopo ni sawa nyoka aliyepigwa mshale sasa anamaumivu..ana hasira kila aliye mbele yake anamgonga!!.
 
Rais alisema deni ni trillioni tatu, nyie mnasema bil 2.7 jingine lilipwa lini?
 
Nangoja wanifuate maana tangu nimalize chuo sijawahi kuajiliwa naendesha shughuli zangu..kunipata wafanye kazi ya ziada
 
Wazee wa comedy hiyo bodi ya mikopo imejaa wajinga tupu,kuna mtu alimaliza mwaka 90 ila leo wamemtoa kwenye list yao.
Mkopo ulianza mwaka 94 kma sikosei sasa huyo wa 1990 anadaiwa mkopo upi
 
tatizo la awamu hii watu wanamuogopa magu wanafanya mambo mengine bila kutumia utashi wanamdangaya ilimradi tu wawepo kazini hivi mdeni anafungwa? wanapoteza muda a

Badala ya kulipwa madeni watajikuta wanaburuzwa mahakamani kwa kudhalilisha watu ambao hawana makosa.
 
Wengine wanalipa kama bodi inavyotaka cha ajabu nao wamo. Sijajua hawa jamaa kazi zao huwa wanafanya vipi
 
Walivyosema kuwashitaki wadaiwa nilicheka sana, maana nilifikiria jinsi Mzee Mrema anavyojitahidi kupunguza msomngamano magerezani huku upande wa pili mtu mwingie anataka kuingiza wafungwa zaidi ya 300,000!
Alafu mtu kusema eti kwa vile wazazi wako walikuwa na pesa mwaka 2000 ni lazima waendelee kuwa nazo mwaka 2016 wakati mnatwambia wazi kuwa waliokuwa wakiishi kama malaika mnawageuza kuishi kama mashetani.
 
Raha sana kuzaliwa Tanzania
1479373992004.png
 
Back
Top Bottom