Orodha ya Utalii ya nyumba za malazi kwenye GN 823 ya 2.10.2020 ina mapungufu

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,460
1,444
Serikali kwa kupitia Wizara ya Utalii na Maliasili iltoa orodha ya mahoteli yanayopswa kulipia vitanda siku nchi nzima na kumkabidhi Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Mhede kuifanyia kazi.

Orodha hiyo ya mahoteli na nyumba za kulala wageni imo kwenye GN No 823 ya tarehe 2.10.2020. Orodha hiyo inapaswa ipitiwe tena kwa vile ina mapungufu mengi kama baadhi ya mahoteli makubwa hayamo kwenye orodha hiyo na mengine yametokea mara mbili kwenye orodha. Mahoteli mengine baadhi ya mikoa hayapo yamefungwa kwa sasa au yamebadilisha majina baada ya kuuzwa.

Hivyo Waziri mwenye dhamana atoe idhini marekebisho yafanyike ili kutoa orodha sahihi na kuchapisha nyongeza kwenye gazeti la serikali kwa mujibu wa Sheria kwa ajili ya tozo/mapato sahihi kama ilivyokusudiwa.
 
...Kulipia vitanda? Kwani unapolipia chumba hotelini hayo malipo ni ya nini? Ya kwenda kusimama chumbani? Sijaelewa.
 
Back
Top Bottom