Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,222
- 157,411
Nã Malisa GJ
Kijana Erick Raphael Msyaliha, anayeishi Sinza (Mugabe) usiku wa tar.13/03/2017 alifuatwa nyumbani kwake na watu wanaodhaniwa kuwa Polisi ambao walimchukua wakihitaji maelezo kutoka kwake. Majirani wanasema tangu Erick achukuliwe na watu hao hadi sasa hajarejea.
Ndugu zake hawajui alipo licha ya juhudi mbalimbali za kumtafuta. Simu zake hazipatikani na hajaonekana popote wiki ya 3 sasa.
Jeshi la Polisi limekanusha kumshililia kijana huyo, kama lilivyokanusha kumshikilia Ben, na kama linavyokanusha kumshililia Roma. Familia ya Erick inaomba yeyote atakayepata taarifa za kuwepo kwake akiwa hai au maiti awasiliane na familia kwa namba 0718 105959.
Hapa ndipo nchi yetu ilipofikia. Binadamu wanapotea na serikali haioneshi kujali, ila Faru anapotea serikali inatumia Mil.700 kumtafuta. Matukio tuliyokua tukiyaona Rwanda, Congo, Sudan na Somalia sasa yanatokea kwetu. Si hadithi ni kweli. Ila Mungu yupo.!!