Kwanini nguvu kubwa inayotumika kumtafuta "Mo" isitumike kuwatafuta Ben, Azory na waliotaka kumuua Lissu?

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
201
1,534
Na Malisa GJ

Kuna mambo mawili ningependa kueleza kuhusu hili tukio la kutekwa MO.

#Mosi; nipongeze mshikamano uliooneshwa na taifa baada ya taarifa za kutekwa kutolewa. Pamoja na kwamba bado hajapatikana lakini taifa zima limeshikamana pamoja. Mshikamano huu ungeoneshwa kwa Ben Saanane, kwa Tundu Lissu, kwa Azory Gwanda na wengineo pengine leo yasingefika kwa MO.

Lakini kwa kuwa tuliona la Lissu na Ben Saanane ni matukio ya kisiasa tukawaachia wanasiasa wenzie wahangaike nao, la Azory tukawaachia waandishi wenzie wahangaike nae, la Roma Mkatoliki tukawaachia wasanii wenzie wahangaike nae. Hii ndio changamoto iliyotufikisha hapa. Kujiona upo salama just because 'hujaguswa'.

Kwa kuwa wewe si CHADEMA ukaona ya Lissu hayakuhusu, kwa kuwa wewe si Mwandishi ukadhani ya Azory hayakuhusu, kwa kuwa wewe si msanii ukadhani ya Roma hayakuhusu, kwa kuwa wewe si Mwanasiasa ukaona ya Ben hayakuhusu. Usidhani upo salama kiasi hicho. Zamu yako ikifika wengine nao wataona ya kwako hayawahusu.

Mchungaji Rev.Martin Niemöller alipata kusema "Walianza na wajamaa, sikuwatetea kwa sababu sikua mjamaa. Kisha wakaenda kwa wafanyakazi, sikuzungunza kwa sababu sikua mfanyakazi. Baadae wakaja kwa wayahudi, sikuwatetea kwa sababu sikuwa Myahudi. Mwishowe wakaja kwangu, na hapakuwepo na aliyesalia kunitetea"

Tungeonesha hasira zetu kana taifa, kushikamana kwa pamoja na kuchukua hatua lilipotokea tukio la Ben, la Lissu, au la Azzory pengine leo MO asingetekwa. But who cares?

Nimeshangaa nana kuona taarifa ya January Makamba akisema kuwa MO ana familia (mke na watoto) na hivyo tumuombee apatikane. Lakini je Ben, Anzory Lissu etc hawakua na familia na watoto?

Kwahiyo kama MO asingekuwa na familia tungemuacha apotee? Hiki ndicho January anachotaka kutueleza?

Nadhani hii hoja ya Makamba sio sahihi. Kuwa na familia au kutokuwa na familia kisiwe kigezo cha kulaani utekaji. Tulaani utekaji kwa sababu ni kitendo cha kinyama, cha kikatili, cha hovyo na kinachokiuka misingi ya haki za binadamu. Mtu awe na familia au asiwe nayo, hastahili kutekwa, na ikitokea hivyo basi anapaswa kutafutwa kwa nguvu zote.

#Pili; RC Makonda amesema tukio hili ni 'jipya' na si la kawaida katika mkoa wa Dar. Yani ameshangaa mtu anawezaje kutekwa Dar? Nadhani atakuwa amesahau. Ngoja nimkumbushe kidogo.

Kijana wa kitanzania Ben Saanane aliyekuwa mwanafunzi wa shahada ya uzamivu (PhD), Chuo kikuu cha Maastrich huko Uholanzi anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake Tabata usiku wa tar.16/11/2016. Hadi leo hajapatikana hata mfupa wake, licha ya juhudu mbalimbali zilizofanywa na UTG, LHRC, CHRCC, na vyomba mbalimbali vya habari. Tukio hili lilitokea Dar, wakati huo Makonda akiwa Mkuu wa mkoa. It seems amesahau. Akumbushwe.!

Kijana Erick Raphael Msyaliha, anayeishi Sinza (Mugabe) usiku wa tar.13/03/2017 alifuatwa nyumbani kwake na watu waliojitambulisha kuwa ni Askari Polisi ambao walimchukua wakihitaji maelezo kutoka kwake. Majirani wanasema tangu Erick achukuliwe na watu hao hadi sasa hajarejea. Ndugu zake hawajui alipo licha ya juhudi mbalimbali za kumtafuta. Habari ya kupotea kwa Erick iliandikwa na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari. Tukio hili lilitokea Dar, wakati huo Makonda akiwa Mkuu wa mkoa. It seems amesahau. Akumbushwe.

Msanii wa Ibrahimu Mussa maarufu kama Roma Mkatoliki, akiwa na wenzie wawili walivamiwa na kutekwa na watu wasiojulikana katika studio za Tongwe Records Kinondoni. Baada ya kelele nyingi za vyombo vya habari, wanaharakati na wasanii wenzake, walitupwa katika ufukwe wa Ununio na kutelekezwa huko. Tukio hili lilitokea Dar, wakati huo Makonda akiwa Mkuu wa mkoa. It seems amesahau. Akumbushwe.

Haya ni machache lakini yapo matukio mengi ya watu kutekwa na kupotea katika jiji la Dar na maeneo mbalimbali ya nchi. Hili si tukio la kwanza kama RC anavyotaka kutuaminisha. Wala si 'tukio jipya' kama anavyodai. Watu wengi wamepoteza ndugu zao kwa matukio kama lililotokea kwa MO leo.

Swali ambalo watanzania wanajiuliza ni kwanini vyombo vyetu havikuchukulia kwa uzito matukio ya kutekwa na kupotea kwa watu wengine kama ilivyokua kwa MO? Waliompiga risasi Tundu Lissu wako wapi? Waliomteka mwandishi Azory Gwanda nani anawajua? Waliomteka Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibondo, Bw.Simon Kanguye ni kina nani? Kwanini hawa wengine haikutumika nguvu kubwa kiasi hiki? Au labda watekaji wao 'wanajulikana?'
_
Kama kweli tunataka kuifanya Tanzania kuwa mahali salama pa kuishi tuache 'double standards'. Sio anapotea MO, nchi nzima inazizima hadi DCI anatoka ofisini kwenda 'field' lakini akina Ben kupotea na Lissu kupigwa risasi, hakuna hata OCS aliyeenda kwenye eneo la tukio. Tujisahihishe. Hakuna raia nusu na raia kamili. Sote ni raia wa Tanzania na sote tuna haki ya kuthaminiwa utu wetu na kupata haki ya ulinzi.!
 
Bwana wee hapo ndio tunashangaa yani hii nguvu ingetumika hata kipindi tundu lisu kapigwa risasi, au kipindi Ben sanane kapotea na watu wengi wanaoripotiwa hakika,jeshi la polisi lingepata sifa tele

Ukakasi upo nimeona bashite akihojiwa TBC mda wa darubini saa sita Leo hii anasema inaonekana waliomteka MO ni wageni swali kajuaje Kama wageni?
 
labda kwa sababu yule mo anatulisha na kutunywesha na kutuburudisha kwa club ya msimbazi.
Tangu nizaliwe sijawahi kusikia bilionea katekwa bongo yetu. Ila leo nimeelewa kwa nini mchungaji kama gwajima anatembea na mabodegadi badala ya Malaika, Sijui sisi wagalatia tujilindeje!!!!!
 
Ni kweli jipya Bwana Malissa GJ kwa SBB:

1. Labda kwa kuwa yeye na kikosi chake (i.e DAB) cha "wasiojulikana" hawajahusika. Sasa anashangaa ni kina nani hao wafanye kitu hiki bila kutumwa na yeye? ....... Jipya hili!

2................................
 
Siku zote ukicheka na nyani utavuna mabua, wakati watu wakitishiwa kwa risasi hadharani kuna watu walikuwa wakiona kawaida tu lakini haya mambo yataleta madhara makubwa sana kwani hata wale waliokuwa wanaogopa wataona kawaida tu kuteka na kutumia silaha za moto.
 
Nyie wapangusa viatu vya Mbowe badala ya kutumia nguvu kubwa kujadili jinsi chadema ilivyokimbiwa na mbunge wa Ukerewe ,sasa hivi mko bize kutumia nguvu kubwa kugeuza tukio la uhalifu alilofanyiwa Dewji kutafuta kiki za kisiasa!!

Aliyewabatiza nyumbu aliona mbali
Naona kila sehemu unahangaika na comment ya namna hii!
Itakuwa imekuuma sana watu kulipa uzito suala la MO na kuachana na upuuzi wa usajili wa malaya wa kisiasa!!!!

Hahaaaaa,tuko busy kumsaka Mo!Mwambie polepole hamna kiki ya huyo jamaa kujiunga ccm!
Kiufupi imebuma,period!
 
Bwana wee hapo ndio tunashangaa yani hii nguvu ingetumika hata kipindi tundu lisu kapigwa risasi, au kipindi Ben sanane kapotea na watu wengi wanaoripotiwa hakika,jeshi la polisi lingepata sifa tele

Ukakasi upo nimeona bashite akihojiwa TBC mda wa darubini saa sita Leo hii anasema inaonekana waliomteka MO ni wageni swali kajuaje Kama wageni?

MKUU walikuwa wageni out ya wale wengine wasiojulikana
ani nadhani anamanisha waliomteka hajatoka kundi lao
 
Ni kweli jipya Bwana Malissa GJ kwa SBB:

1. Labda kwa kuwa yeye na kikosi chake (i.e DAB) cha "wasiojulikana" hawajahusika. Sasa anashangaa ni kina nani hao wafanye kitu hiki bila kutumwa na yeye? ....... Jipya hili!

2................................

yaah sahihi nadhani wapo wanaulizana imekuaje tena??
mbona amri haijatoka Ndani yetu
 
Back
Top Bottom