DOKEZO Organized Crime(?): Nani wapo nyuma ya Ramla Said Ahmed?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Matunda yameshaanza kuonekana Ramla Said keshakamatwa kwa utakatishaji fedha kupitia ununuzi wa dhahabu through black market. Mumewe amejitoa katika sakata hili na wengi wa viongozi waliopigiwa simu za kisiri wamegoma kutoa msaada katika kumnasua.

Ila mpaka sasa amebadirishiwa mashtaka inavyoonesha tayari kuna mrungula umetolewa kulainisha case.

Wapo wazalendo wa kweli ila ni wachache
 
Picha please, tumuone mmoja wa watu anaeifanya Tanzania kuendelea kuwa Masikini.

Dodoma hadi leo barabra za katikati ya Jiji pale mjini ni za vumbi, barabsra za toka mjini kuelekea nane nane hadi Mtumba ni nyembamba sana foleni muda wote tumeshindwa kutanua na kujenga barabara nzuuuri sababu najua hakuna hela, Ila pembeni kuna wanaosababisha haya.

Ndio maana mioyo yetu inamlilia sana Mzalendo wa kweli JPM
 
Nakubaliana nawe mkuu, ndiomana ilifikia kipindi rate MG alikuwa akimpa vijembe JK lakini kutokana na uwelewa mdogo wa watu walikuwa walimchukulia ni kama chuki za kisiasa tu kumbe Kuna makubwa katika kulea utoroshaji wa rasilimali za nchi.
Fbme bank ilikua dili zao kupitia madalali wa kizungu..

Wazungu walikua wanakuja hapa kujifanya Wananunua madini kumbe ni madalali wa FBME bank.
 
Kipimo cha utu uzima na kujitambua nikuona kiongozi anaongea alafu wewe u akasirikia mazungumzo yake wakati upo sebleni kwako, jua hapo umekuwa mtu mzima.

Sasa ishu kama hizi ukizisoma na kuzikia unasonya peke yako jua sasa umekuwa mtu mzima na kujitambua.
 
Hakika mkuu kuna muda mtu unatamani ungekuwa na mamlaka makubwa ili urekebishe mambo lakini ndio hivyo. Tunaletewa mpaka yaliyowazi sasa ya DP World ni jinsi gani tunaonekana watanzania tumelala katika ulimwengu huu.
RIP Magufuri, japo alichofeli ni kuua demokrasia kwa kutulea bunge la ovyo na kutesa watu.
 
uchaguzi umeingiaje hapa. tunza heshima yako
Acha upumbavu,haya ndio matokeo ya wengi humu kutokujua how to read to understand, hii issue ni mwendelezo wa uchunguzi ule wa to smuggling cigarettes from Zimbabwe to south africa, then malipo Dubai, watu weusi ni shida dunia hii maana ni corrupted, greedy na washenzi,(only Botswana kuna uafadhali wa hili na corruption its almost ni zero)
 

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila Bongo haitajwi kabisa au sisi ni kunguru?
Madini yetu yanapita jirani ama
Nimeisoma hii ila kama ni ujambazi viongozi wa Africa wanaongoza duniani kwa upumbavu

Bora hata kama wangeendeleza nchi zao ila huwa wanaishia kuwa na Ranch za ng'ombe tu pumbavu kabisa
 
Huyu ni Mmiliki wa Sharjah Trading (nitaeleza kwa undani kuhusu hii kampuni).

Miaka michache iliyopita wakati wa utawala wa Magufuli alikamatwa, akafunguliwa kesi ya utakatishaji fedha akafanya plea bargaining, ikakubaliwa - akalipa faini na kuachiwa.

Ramla alikamatwa juma lililopita, siku ya Alhamisi akawa anashikiliwa Cetral Police Mwanza.

Anamiliki Bureau De Change pale Mwanza ila anafanya biashara zake hadi mkoa wa Geita.

Hadi anakamatwa, alikuwa na pesa nyingi za kigeni ambazo hakuwa amezibadilisha na alikuwa anazitumia kununua madini aina ya dhahabu katika ‘black market’ kisha yeye analipwa 2-4% katika kila manunuzi.

Katika kuhangaika kwake ili ajinasue akawasiliana na Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini. Wao kwa kuanzia wakamkatalia. Wakasema kwakuwa tayari lipo katika mikono ya kikosi maalumu (task force) kinachoshughulikia haya masuala basi wao wanashindwa kuweka mkono.

Wakajaribu kumwona RC Shigella awasaidie. Akakataa ila Jumatatu ya wiki hii akawapigia, akawaambia anaweza kuwasaidia lakini ‘lazima wafanye jambo’ (PCCB fuatilieni, maafisa wenu wana taarifa).

Wakawa wanahaha waweze kumwona kijana mmoja mtoto wa Kigogo mkubwa ambaye walielekezwa na Waziri mmoja kuwa wafanye hivyo, akiwaaminisha ndio pekee anayeweza kuwasaidia ndugu yao akaachiwa ila kwa kijana huyo wakagonga mwamba.

Sasa, leo vyanzo vyangu vinaonyesha Ramla kapewa shitaka la kununua dhahabu bila kufuata utaratibu. Kashapelekwa Geita na ana simu anawasiliana na watu wake.

Kuna kila dalili hela imetolewa katika mchakato huu.

Mumewe amegoma kutoa hela zake akisema zitumike za mtuhumiwa mwenyewe na katoa msimamo kuwa hata akifungwa yeye hajali. Watoto ndio wanahaha kumtoa mama yao.

Swali: Kina nani wako nyuma ya mama huyu?
tunaomba picha plz
 
Back
Top Bottom