Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!"

Pasco bana, unakuwa kama yule jamaa anayesema "Kwa Mbinde......."

Swali- Mzigo walipakua lakini?

Jibu- kwa mbinde, waulize wale vijana, mie ni SOJA.

Swali- Sasa ulipindishwa saba?

Jibu- kwa mbinde nimekuambia. Waliniinamisha nikasimama, mara ya pili-nikasimama, mara ya tatu, wakashindilia.

Zitto hapa mnampa ujiko kuwa kashindwa "KWA MBINDE."

Kwa nini kasubiri hadi Jaji Mziray kamtenda, na yeye ndiyo kuja kujifanya ANANG'ATUKA? Yale yale ya PM aliyeng'atuka.

Dah kweli kama una stress njoo JF! Mkuu nimecheka sana!
 
Hili swali hakuna Bavicha yeyote anaweza kulijibu saidi ya kuleta porojo.

Mbunge wa Wawi toka Pemba anaingia hadi sasa bungeni licha ya kiwamba CUF alishafukuzwa kama nani kama si kinga ya mahakama aambayo Zitto imemtema tokana na kiherehere chake?

Nilishawahi mara kadhaa kusema Zitto hajakomaa, anakiherehere, hana busara, vijana wana motomoto na umri wake ndio rika ya madikteta wengi waliowahi kuchukua madara kwa nguvu katika mchi mbalimbali duniani na kusababisha maafa kama Hittla wa Ujerumani na yule kijana wa kule Liberia. Hali kadhalika Idd Amini wa Uganda.

View attachment 236342
Mtaka cha uvunguni sharti ainame, historia inajieleza jinsi Kikwete alivyopitia mikwara kadhaa na aliposhindwa Dodoma kwa Mzee Nkapa akapokea kwa busara ushauri wa Nyerere, asingekupali hilo leo ingebaki historia kama ya akina Kaburu wa Kigoma na Zitto Kabwe. Akina Masumbuko Lamwai wa NCCR Mageuzi kiherehere hicho hicho na tamaa kwa kudanganywa na CCM walishajichimbia kaburi kisiasa kwa kujiingiza kichwakichwa kama bungo zao hazifanyi kazi vile.

:msela: MTAKA CHA UVUNGUNI SHARTI AINAME :msela:​
 
Pasco anazidi kujidhalilisha hapa, ninaanza kuamini hata yote aliyokuwa akimsemea lowassa ni ya uongo,

Ni nani asie juwa kuwa Zitto katimuliwa Chadema?..

Pasco ana mahaba ya wazi na zitto, sio kosa lakini uwandishi wako una hidhalilisha.
 
Ushindi wa Zitto kwenye hili ni nini?

Kutumia media coverage kulalamikia katiba ya Chadema na katiba ya nchi ati zinamkandamiza?

Juzi kwenye kipindi cha dk 45 nimemfuatilia kwa makini ili nisikie maelezo yake ya kwa nini alienda mahakamani huku akijua fika kama atashindwa atakuwa amejifukuzisha mwenyewe. Bahati mbaya sikusikia chochote licha ya kuulizwa swali hili na muongoza kipindi.
 
The Road ahead for Zitto....

kuna kitu ambacho naona Zitto anakiweza sana kuliko yoyote ndani ya CHADEMA
nacho ni ku court attention all the time.....
naamini hiki ni moja ya vitu ambavyo wapo watu ndani ya CHADEMA vina wa irritate sana

waliamini wakimfukuza watamfukuza kama mbwa and its done
badala yake kawachezesha ngoma halafu anaondoka in style...

maradona wa siasa za Tanzania for sure....
now October kuna 'world cup'

lets wait and see
 
BREAKING NEWS;Halima mdee sasa siku zake za hesabika
ndani ya chadema.taarifa zilizopo ni kwamba kutokana na
tuhuma za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na zitto kabwe
sasa kukubalika kwake ndani ya chama kuna mashaka
makubwa,tuhuma hizo alisomewa leo na mwanasheria wa
chadema tundu lisu wakati wa kikao cha dharura baada ya
mapumziko ya bunge kikao ambacho kilivurugika baada ya
halima mdee kummwagia matusi ya nguoni Mh.tundu lisu
na kumtaka akaimbe taarabu kama anapenda umbea na
mambo ya kuzua.hata ivyo wakati wakiendelea kurushiana
maneno inasemekana Mh.halima alimtupia chupa ya maji
Mh tundu lisu kwa bahati ilimpiga katika bega lake la kulia
kabla ya wabunge wenzao kuamulia ugomvi huo,hata ivyo
tundu lisu amemtaka mbunge huyo ambaye ni mwenyekiti
wa bawacha kujiandaa kwa majibu ambayo alikuwa
anazungumza na zito siku ya jumapili kabla ya kikao cha
usiku wa siku hiyo.
Duh! Movie ndo kazi inaanza,lets wait and see.
 
Baada ya Kisa, Mkasa, na Baada ya Chanzo Kitendo!,

Sakata la Zitto Kabwe na Chadema limekuwa na visa na mikasa, vyanzo na vitendo na hatimaye leo, limekwisha rasmi, it is now a history!.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe, amefanya historia kwa kuwa mbunge wa kwanza kungatuka rasmi ubunge kwa kuaga rasmi kwa kulihutubia Bunge!.

Hatua hii, sio tuu inamfanya Zitto kuendelea kuwa shujaa, bali pia kwa hatua hiyo, ameipiga Chadema bao la kisigino, kwa sababu sasa ni Zitto ndio ameiacha Chadema na sio Chadema imemfukuza!.

Uuanachama hauombwi kwa maelezo na haufukuzwi kwa maelezo na press conferences!.

Ama kweli Zitto ni shujaa sijaona mfanowe!.

Hili ni angalizo kwa Chadema na wapenzi wake, msishangilie sana hadi mkajisahau, wekini akibakidogo kwa sababu, kujiuzulu kwa Zitto, kunaweza kusiwe ndio mwisho bali ukawa ndio mwanzo wa series za 'karma' effects ambazo ama zitamtandika Zitto mwenyewe kama kweli ni msaliti, ama zitaindandika Chadema, kama haikumtendea haki!.

Kwa mnaoijua 'karma', shangilieni kwa kiasi tuu, msimbeze, msimehihaki wala msimtukne kwa sababu hakuna mkamilifu.

Pasco.

Note to mode: This is opinion article na sio reportage!

Kwa hiyo ndio kung'atuka huku.

zitto.jpg
 
Hili swali hakuna Bavicha yeyote anaweza kulijibu saidi ya kuleta porojo.

Alikuwa anaingia kwa hisani ya waliokuwa wanamtuma kuhujumu chama chake, mbona iko wazi mkuu? Ndo maana tumesikia kauli za bunge na tume zikipishana na khjichanganya.
 
Juzi kwenye kipindi cha dk 45 nimemfuatilia kwa makini ili nisikie maelezo yake ya kwa nini alienda mahakamani huku akijua fika kama atashindwa atakuwa amejifukuzisha mwenyewe. Bahati mbaya sikusikia chochote licha ya kuulizwa swali hili na muongoza kipindi.
Hivi kweli nyie watu mna tatizo la kusahau au mnafanya kusudi. Kitila na wenzake wote walifukuzwa uongozi na uanachama na wakapinga hatua hiyo wakitaka baraza kuu ndilo lipewe mamlaka hayo. Na huwezi kusajili kesi (rufaa) pasipo kupitia Ofisi ya katibu mkuu ambaye aliwakatalia. Tumeyasoma matukio yote haya humu humu JF, leo mtu anauliza kwa nini Zitto alikwenda mahakamani?

Halafu kwa ujinga wa watoa taarifa wa Chadema wanasema ati Zitto kwenda mahakamani kajifukuza ilihali walimfukuza hadi uanachama toka mwanzo. Mbona Prof. Kitila alikuwa pia mjumbe wa kamati kuu na alifukuzwa hata uanachama? Je, kuna tofauti yoyote! Kwa kutumia kifungu gani cha sheria kamati kuu inaweza kumfukuza kiongozi aliyechaguliwa uanachama! na bado kina Kitila wametukanwa weee japo walikubali yaishe. Hata hivyo mkuu, jibu lako lipo ktk waraka aloandika Zitto ambao alikuwa ausome leo bungeni. Soma vizuri kisha jiulize mwenyewe..
 
Pasco

Nikuulize tu kitu kidogo

Hivi ule mkutano ulioitishwa na Tundu Lisu yeye na waandishi wa habari ilikuwa ya nini???
1. Tundu Lisu aliongea nini kuhusu Zitto???
2. Bila Tundu Lisu kuongea na waandishi wa habari kuhusu kufukuzwa uanachama Zitto, Je Zitto leo angeaga bunge???
3. Katiba ya Chadema liko wazi na Zitto analijua hilo na ndio maana alikimbilia mahakamani, baada ya kuona ameshindwa akawa anajua kabisa kuwa amejifukuzisha uanachama hata kama asingeambiwa na Lissu.

Jamani Watanzania tuachane na maneno ya uongo au ya kumsifia mtu pasipo sababu, hapa hakuna cha ushindi wala mshindwa kilichopo ni kuwa Zitto aliteleza kwenye chama chake na chama chake kimemchukulia hatua za kinidhamu.

Kweli Pasco kwa akili yako na kidogo uelewa wako wote ndio hapo ulipofikia, kweli Tanzania mna safari ndefu. Ndio mana mpaka leo mnamwita Lowassa Waziri mkuu mstaafu wakati alifukuzwa kwa kashfa.

Mwisho kama Zitto angekuwa shujaa labda niseme kama angeondoka ile siku ya kwanza walipoondoka wenzake Kitila na Mwigamba. Kulikuwa hakuna maana kwenda mahakamani, hii ya kwenda bungeni na kusema/kuaga ni danganya toto ya kuwadanganya watanzania kama akina Pasco.

Lakini kinachojulikana Zitto alifukuzwa/alijifukuzisha Chadema tangu mwaka jana alipofungua kesi mahakamani.

Tanzania ya sasa sio ya mwalimu, yani nchi imejaa watu waongo,wezi, wabinafsi si serikali si raia. Yani hakuna neno ambalo unaweza kuliamini, maneno yanazushwa,uongo kila sehemu na serikali imekaa kimya bila hata kufanya chochote. leo mtu anazusha rais,waziri,mama nyerere kafa serikali kimya wala hawachukuliwi hatua tunaenda wapi??

INATAKIWA SERIKALI IMARA YENYE KUSIMAMIA WATU WAKE KWA HAKI NA UAMINIFU. ILI KILA RAIA AFUATE SHERIA NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE BILA KUJALI HUYU NI MTOTO WA WAZIRI AU MTOTO WA KOVA. HII ITAONDOA UONGO NA UZUSHI

kama wewe unatumia akili,na unakubali zito alishafukuzwa uanachama,katiba ya JMT inasema ubunge unapotea,kwanini Zitto aliingia bungeni km mbunge,na juz alishangia mswada wa ajira kwa wageni,pia Jana katangaza kung,atuka.si amefukuzwa uanachama,km ilo linawezakana MTU ambaye si mbunge akaingia bungeni,na akaa katika kitu cha ubunge aende padr slaa,tuone kama hataruhusiwa kukaa viti vya ubunge,naunga mkono hoja ya Pasco
 
Last edited by a moderator:
Baada ya Kisa, Mkasa, na Baada ya Chanzo Kitendo!,

Sakata la Zitto Kabwe na Chadema limekuwa na visa na mikasa, vyanzo na vitendo na hatimaye leo, limekwisha rasmi, it is now a history!.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe, amefanya historia kwa kuwa mbunge wa kwanza kungatuka rasmi ubunge kwa kuaga rasmi kwa kulihutubia Bunge!.

Hatua hii, sio tuu inamfanya Zitto kuendelea kuwa shujaa, bali pia kwa hatua hiyo, ameipiga Chadema bao la kisigino, kwa sababu sasa ni Zitto ndio ameiacha Chadema na sio Chadema imemfukuza!.

Uuanachama hauombwi kwa maelezo na haufukuzwi kwa maelezo na press conferences!.

Ama kweli Zitto ni shujaa sijaona mfanowe!.

Hili ni angalizo kwa Chadema na wapenzi wake, msishangilie sana hadi mkajisahau, wekini akibakidogo kwa sababu, kujiuzulu kwa Zitto, kunaweza kusiwe ndio mwisho bali ukawa ndio mwanzo wa series za 'karma' effects ambazo ama zitamtandika Zitto mwenyewe kama kweli ni msaliti, ama zitaindandika Chadema, kama haikumtendea haki!.

Kwa mnaoijua 'karma', shangilieni kwa kiasi tuu, msimbeze, msimehihaki wala msimtukne kwa sababu hakuna mkamilifu.

Pasco.

Note to mode: This is opinion article na sio reportage!

Zitto alishafukizwa toka alipokimbilia mahakamani.wewe pasco.endelea kuganga njaa labda utapata chenji kama andrea
Cordes . Unajifanya great thinker kumbe unatumia tumbo kufikiri chenji za mafisadi na nyama choma za mondoli juu zinakutoa ufaham shwein wahhid
 
Amechelewa sana, mahakama imemshtukiza akiwa off-guard, chadema wamepiga za ukweli, asi nawe usiturubuni, zitto kafukuzwa chamani.

Nasema ni mjinga, ndio ni mjinga!!! Yeye badala kupigana akiona adui ana nguvu zaidi yake, akimbie ili ajipange, yeye anajiingiza kwenye ROBA ya JOHN CENA kinyesi kimemtoka, anajitetea eti " nilikalia maji"

Nguvu alizodhani na kutumainishwa kuwa zipo za ccm masikini siku hizi hazipo, yamebaki maigizo tu, wameshindwa kumlindia hadhi yake,

Kinachofuata sasa atabwabwaja kama mwanamke aliyetalikiwa, oh! Kwanza we mwanaume gani hata kazi huwezi n.k

Nasi tutamkumbusha mwanamke huyu alivyokuwa akijifunga kibwebwe kuwatimua wanawake wanyemelezi, tutamkumbusha maneno aliyokuwa akiwasimulia mashosti wake kuhusu mumewe anavyonoga.
("Chadema imenilea na kunifikisha hapa nilipo")
Akisema chadema ni mbaya basi itakuwa imempa malezi ya yeye kuwa mbaya zaidi kuliko mlezi wake.

Maskini zitto tulikupenda, lakini wajinga wamekupenda zaidi na wamekumaliza!!!!!

Pasco upo hapo, wapelekee lumumba haka kakaratasi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom