Pichani hapa ni Kevin Holland akiwa na Saddam Hussein, muda mfupi baada ya kukamatwa kwake.
Holland ndiye anayejulikana kuwa mwanajeshi pekee aliyewahi kuhudumu katika vitengo viwili vya siri vya kiwango cha juu zaidi nchini Marekani—kwanza katika kitengo maalum cha Jeshi la Wanamaji (
Navy SMU), na baadaye katika kitengo maalum cha Jeshi la Nchi Kavu (
Army SMU).
Alihitimu shule ya West Wilkes High School huko North Carolina mwaka 1988, kisha akajiunga na Jeshi la Wanamaji. Akiwa na umri wa karibu miaka 20 tu, alishiriki Vita vya Ghuba (
Desert Storm) akiwa kama SEAL, akifanya upelelezi wa kina deep reconnaissance akisaidiana na mlenga shabaha sniper maalum kaskazini mwa Iraq. Baadaye alishiriki katika Operesheni kadhaa ukiwemo
Provide Comfort na
Uphold Democracy.
Akiwa miongoni mwa asilimia moja ya SEAL bora zaidi, Holland alichaguliwa kujiunga na Navy SMU. Aliondoka jeshini mwaka 1997 na kuwa afisa wa wanyamapori huko North Carolina. Lakini baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001, alirejea jeshini na baadaye akahamia Jeshi la Nchi Kavu, ambako alichaguliwa pia kujiunga na Army SMU.
Tarehe 13 Desemba 2003, Holland alikuwa Ad-Dawr, Iraq, akiwa sehemu ya Task Force 121 iliyokuwa ikimtafuta Saddam Hussein. Kikosi hicho kiligundua shimo dogo lililofichwa chini ya mabaki ya uchafu.
Holland alikuwa miongoni mwa waliomtoa Saddam Hussein ndani ya tundu hilo, wakimvuta kwa nywele na ndevu. Huku Holland akimuelekezea bunduki kifuani mwa Saddam, ikiwa tayari kwa matumizi, hadi alipothibitisha kuwa hakuwa na silaha.
Saddam Hussein, aliyekuwa akitafutwa kwa jina la “Ace of Spades,” alikuwa amekamatwa rasmi.
Mwaka 2011, huyu bwana Holland alipata jeraha kubwa vitani. Alistaafu mwaka 2013 baada ya miaka 25 ya utumishi.