Kwenye picha hizi hapa chini ni Master Chief Britt K. Slabinski, mpokeaji wa Nishani ya Heshima ya Juu kabisa ya Jeshi la Marekani (Medal of Honor), alikuwa mtu muhimu sana kwenye moja ya usiku wenye utata na changamoto kubwa zaidi katika historia ya kisasa ya SEALs—Vita vya Takur Ghar, vinavyojulikana pia kama Roberts Ridge.
Slabinski alitamani jambo moja tangu alipojiunga na Jeshi la Wanamaji mwaka 1988 ya kuwa mwanajeshi wa navy SEAL. Alifanikiwa kupata Trident yake baada ya kumaliza mafunzo ya BUD/S, kwenye Darasa la 164, Januari 1990. Baadaye alikamilisha safari tisa za kikazi nje ya Marekani na safari 15 za kivita, ikiwemo operesheni ya kumwokoa Private Jessica Lynch wa Jeshi la Marekani mwaka 2003.
Sasa Usiku wa kuamkia tarehe 3 hadi 4 Machi 2002, Slabinski aliongoza kikosi cha upelelezi kuelekea Mlima wa Takur Ghar, kilele chenye urefu wa takribani futi 10,000, kilichofunikwa na theluji katika Bonde la Shahi-Kot nchini Afghanistan.
Helikopta yao ilipokaribia eneo hilo, ilipigwa na RPG, iliyosababisha Petty Officer Neil Roberts kuanguka kutoka kwenye helikopta na kutua katika eneo lililokuwa limeimarishwa na wapiganaji wa Taliban chini ya milima hiyo.
Slabinski aliamua kugeuza kikosi chake na kurudi moja kwa moja mlimani kumtafuta Roberts. Walipanda tena kuelekea eneo hilo na kushambulia pamoja na kusafisha ngome ya adui huku wakikabiliwa na mashambulizi makali.
Katika vurugu zilizofuata, Combat Controller John Chapman alijeruhiwa vibaya. Kwa kuamini kwamba Chapman alikuwa tayari amekufa, Slabinski aliamuru kikosi kijiondoe pamoja na mwanajeshi mwingine aliyekuwa amejeruhiwa vibaya.
Lakini kulikuwa na jambo ambalo hakuna aliyelijua wakati huo.
Miaka kadhaa baadaye, baada ya picha za video zilizorekodiwa na ndege isiyo na rubani (drone) kuchunguzwa upya, ilibainika kwamba alikuwa amerudiwa na fahamu na alikuwa akipigana peke yake kwa karibu saa nzima. Hatimaye, alipambana huku akivuta mashambulizi ya adui kuelekea kwake na hivyo kusaidia kuondoa presha kutoka kwa kikosi cha Rangers kilichokuwa kinakuja kuwaokoa, kabla na hatimaye kuuawa.
Tofauti hiyo kati ya kile Slabinski alichoamini wakati huo na kile kilichokuwa kimetokea
na Chapman wote walitunukiwa Medal of Honor.
Tuzo ya Slabinski ilikuwa kupandishwa hadhi kutoka kwenye Navy Cross aliyokuwa tayari amepokea.
Baadhi ya watu katika jumuiya ya operesheni maalum pamoja na baadhi ya waandishi wa habari walidai kwamba uamuzi wa kumuacha Chapman ulikuwa kosa na kwamba haukupaswa kupewa tuzo. Wengine, akiwemo viongozi waandamizi wa kijeshi, waliutetea uamuzi huo wakisema kwamba kwa taarifa ambazo Slabinski alikuwa nazo wakati huo, katikati ya mapambano makali, usiku, kwenye mlima, huku akiamini mwanajeshi wake tayari amefariki, huo ulikuwa uamuzi wa busara zaidi ambao kamanda angeweza kufanya.
Katika mapambano mapana ya Takur Ghar, Wamarekani saba waliuawa, huku Rangers na wanajeshi wa anga pia wakipoteza maisha katika mapigano yaliyofuata.
Huyu mwamba alikiri kwamba heshima hiyo aliyopewa si yake peke yake Bali ni ya kikosi kizima.