Operesheni KIMBUNGA yaanza rasmi

Tatizo ni pale oparesheni inapoendeshwa kwa kuangalia sura za watu. Kuna hakimu mkazi huko Kagera kapata kichapo kwa kuwa tu ana sura ya kitusi. Kwa utaratibu huu tutajikuta wahamiaji haramu hasa wenye asili ya kihutu wakiachwa bila kuguswa huku watanzania wenye asili ya kitusi wakiswagwa kwenda mahali wasipopafahamu. Zoezi linaendeshwa mechanically.
Kwa nini wahutu wabaki halafu waondoke watusi tu?
 
Tatizo ni pale oparesheni inapoendeshwa kwa kuangalia sura za watu. Kuna hakimu mkazi huko Kagera kapata kichapo kwa kuwa tu ana sura ya kitusi. Kwa utaratibu huu tutajikuta wahamiaji haramu hasa wenye asili ya kihutu wakiachwa bila kuguswa huku watanzania wenye asili ya kitusi wakiswagwa kwenda mahali wasipopafahamu. Zoezi linaendeshwa mechanically.
Mkuu zoezi hili haliwezi kuwa na efficiency ya 100% na kesi za watu wawili watatu haziwezi kuonesha kuwa zoezi halikwenda kihalali...

Hapa kinachofanywa ni propaganda tu za kitusi na hasa kutoka RWANDA, mbona wahutu wanarudishwa na hatusikii kelele??

Kwa nini watusi tu???
 
Kwani kabla ya mgogoro na Rwanda jk ulikua wapi kufanya hiyo opareshen?
 
Zoezi hili /Operation hii isiishie kwa Wahamiaji haramu kutoka Rwanda, Burundi na Uganda tu. Liendelezwe kwa Wahamiaji haramu wote kutoka China, Somalia, Kenya, DRC na nchi nyingine yoyote ile. Zoezi hili likilenga makundi machache litakuwa la kibaguzi. Tunataka wahamiaji haramu wote watimuliwe bila kujali nchi wanazotokea.
 
Jeshi la Polisi, Jeshi la Kujenga Taifa, Usalama wa Taifa na pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania. HAKIKISHENI hakuna MTUTSI YOYOTE ANAEBAKI, mara 100 akabaki Mrundi au Mkongo kuliko hawa Watutsi. Huko DRC walianza hivi hivi ila leo dunia nzima inaona nini kinachoendelea kufanywa na Watutsi kupitia M23. Wakizaliana sana Ipo siku Watataka Kagera, Geita n.k kuwa hayo maeneo ni yao na wapewe hifadhi ya kudumu. Damu ya Kitutsi haibebeki, 1994 wakati wanachinjana kwao Rwanda wengi walikimbilia Congo na wengine wakaja hapa. Na hao hao ndio waliomtukana Rais Kikwete. Damu za Wakongo Milioni 3 walizozimwaga DRC ni lazima ziwalilie kila waendapo.
 
sikushiriki kwa namna yoyote kutetea ubaguzi na uvunjaji wowote wa haki za binadamu.
 
hawaangalii sura tu mkuu!!kuna mambo mengi sn ya kiinteligensia yanachunguzwa,wanaulizwa maswali na team za watu ambao ni professionals,hivyo hakuna atakae onewa!!!!sura na lafudhi ni moja tu ya items za uchambuzi unaotumika kuwatambua!!!
I know you're joking. Huyo hakimu aliyeshambuliwa alitendewa haki?
 
Mkuu zoezi hili haliwezi kuwa na efficiency ya 100% na kesi za watu wawili watatu haziwezi kuonesha kuwa zoezi halikwenda kihalali...

Hapa kinachofanywa ni propaganda tu za kitusi na hasa kutoka RWANDA, mbona wahutu wanarudishwa na hatusikii kelele??

Kwa nini watusi tu???
Talk about the efficiency of a corrupt bureaucracy. Jamaa zako hawa kila kinachokatiza mbele yao wanaona ni fursa ya utajirisho.
 
Tatizo ni pale oparesheni inapoendeshwa kwa kuangalia sura za watu. Kuna hakimu mkazi huko Kagera kapata kichapo kwa kuwa tu ana sura ya kitusi. Kwa utaratibu huu tutajikuta wahamiaji haramu hasa wenye asili ya kihutu wakiachwa bila kuguswa huku watanzania wenye asili ya kitusi wakiswagwa kwenda mahali wasipopafahamu. Zoezi linaendeshwa mechanically.
Hekima na busara isipotumika katika zoezi hili halitaleta tija kwa taifa.
 
Swali la kufikirisha.

Enzi za uhai wake Mwl Julius K. Nyerere alisema tukianza na ubaguzi wa huyu Mtanganyika na yule Mzanzibar mjue haitaishia hapo, kesho mtaanza huyu mmakonde wa rufiji na yule mmakonde wa musumbiji, na hii imeshaota mizizi leo hii sio kitu cha kushangaza kuwaona wasukuma au wamasaii wakichomewa nyumba zao moto eti tu kwa vile wako kusini mwa TZ au kwingineko eti nao ni wahamiaji / wafugaji haramu.P/se tuwe makini natukifanyacho.
 
katika
hali isiyo ya kawaida wiki hii ni mshike mshike wa kujificha kwa
wahamiaji haram; ambao wengi wao ni wanamziki wa kikongo: matapeli wa
kinajeria; mabaa medi na mahotelia wa kikenya wengi wakiwa katika hali
ya taharuki; kwa ufupi watanzania wengi wamepata nafuu hasa kwa ndugu
zetu wakongo ambao tunawapigania wapate utulivu wafaidi madini yao
yanayochukuliwa na m23 na ukoo wa pk. Watanzania mbali na kuwa punda wa
makada wa chama fulani ; wakipata fedha zao uishia kuwapa wakongoman
ambao kwa kawaida uitwa mario au defender au TRA kwani wana mbinu
nyingi za kukusanya mapato toka wa Tz kwa njia ya kuwasifia na
kuwaimba. Mtz akiitwa papa mukru ya pamba uota mapembe ghafla na kumwaga
maela utafikiri katoka machimbo kumbe sembe imemtoa. Sasa kinondoni
magomeni na msasani hapakaliki wale wakina mpe mruke hawapo tena
 
Zoezi hilo lisiishea kuwatimua wahamiaji haramu katika mashamba na mapori ya akiba wanakulisha ngombe na mifugo yao bali liingia pia kuwarudisha makwao wageni haramu walio Serikalini na katika majeshi yetu. Mweshimiwa Rais Kikwete fungua macho uone wapo wengi sana ndani ya Serikali yako na katika majeshi yetu nao waondolewe.
 
Mhe. Kiwete amekuja na operation timua timua ya wakimbizi na wote wanaoishi hapa nchini TZ kinyume na sheria. Lakini wakati wanaingia hapa nchini sheria hizo zilikuwepo na hazikufuatwa namna ya kuwaangalia wasije wakahesabika kuwa ni raia wa Tz.

Inasikitisha kwa jinsi suala hili linavyochukuliwa na vyombo vya Serikali imeonekana kuwa ni 'dili' kwa baadhi ya maafisa Uhamiaji na vyombo vya usalama.

Sasa kinachoonekana hata kama unafanana na Wanyarwanda au Mzaire tu una hatari ya kukamatwa na kulazimishwa kusipokuwa kwenu.

Jana imejitokeza kabisa kwa rafiki yangu walimshikiria kwa muda hapa kanda ya ziwa , hali ilikuwa mbaya maana wanasema hauna hati ya uraia.

Hivi jamani Hati inayotambulika kwa sasa ni kitambulisho cha mpiga kura ambacho wengi tunavitumia pia kama vitambulish vya uraia maana mchakato wa Vitambulisho vya uraia upo slow sana. Ok jamaa alikuwa na kitambulisho cha mpiga kura na kitambulisho cha kazi na pia passport ya TZ.

Na hizi documents hata wale wakimbizi na wanaoishi nchini kinyume na sheria wengi wanavyo, linapokuja suala la kuwarudisha kule wanaposema kwao linakuwa gumu mwisho wa siku watarudishwa watanzania na kuacha wakimbizi hapa nchini.

Na kwa hali hii operation hii imeanza kufeli kabisa. Maana wanaoishi humu isivyo halali na si watanzania wanaachwa wanakamatabtu watanzania wenzetu kwa kufananisha tu na Wazaire au wanyarwanda.

Ningeomba wote vyombo vya usalama liangalie namna ingine ya kushughulikia suala hili siyo tu kuvamia guest house , mahotelini usiku ha hata bus terminals na kuleta usumbufu kwa raia wa Tanzania.

Just imagine leo umekata ticket upo Ubungo unajiandaa kuja Mwanza na ni raia halali wa Tz then unakamatwa , unapoteza nauli na. Usumbufu mwingine na mwisho wa siku wanakuachia baada ya kuthibitika kuwa wewe ni raia wa Tanzania bila kulipwa usumbufu uliojitokeza. Jamani nchi hii inaelekea pabaya sana.

Kama waliwaruhusu kuingia na wakashindwa kuwahudumia kufuata sheria inakuwaje leo raia tunyanyaswe hivi????
nawasilisha.
 
Hivi kwanini nyie mnaojiunga JF siku za karibuni huwa mnasumbua sana? Ndivyo kagame alivowatuma? Kwenu kurudi mtarudi tu.
 
Na Theonestina Juma, KAGERA


OPERESHENI kimbunga ya kuwarejesha wahamiaji
haramu makwao katika Mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma imeanza rasmi ambapo ndani ya siku mbili tu, wahamiaji hamu 1851 na ng'ombe 10763 wamekamatwa.

Hayo yamebainishwa jana (leo) na Mkuu Operesheni nchini,Simon Sirro ambaye pia ni Mkuu Msaidizi wa operesheni kmbunga katika mkutano na Waandishi wa habari kuhusiana na operesheni ulioanza rasmi Septemba 6, mwaka huu kufuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete alilotoa akiwa ziarani Mkoani Kagera mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.

DSC09011.JPG

Mkuu wa Mkoa Kagera Kanal Massawe akiwa na Mkuu wa operesheni nchini na Mkuu wa operesheno Kimbunga Kamanda Simon Sirro ambaye pia ni kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Kamanda Sirro amewataka wananchi wote kutoa ushirikiano katika zoezi zima ambalo amesema halina mwisho mpaka hapo watakaporidhika.



Alisema katika mkoa wa Kigoma wamekamatwa wahamiaji haramu 855, short gun moja, gobole moja na ng'ombe 200, Mkoa wa Geita wahamiaji haramu 246 wamepatikana, gobole tatu na ng'ombe 240, sare ya jeshi moja na kibuyu cha maji cha JWTZ moja.

Halikadhalika Mkoa wa Kagera Wahamiaji 750 wamekamatwa, short gun moja, gobole sita, ng'ombe 1,323, ambapo ng'ombe 200 walikamatwa ndani ya pori la akiba la Moyovosi Kigoma na wengine 200 wamekamatwa katika pori la akiba la Burigi mkoani Kagera.
Alisema ng'ombe 1,123 wamekamatwa wilaya za Karagwe na Kyerwa na 240 kutoka maeneo mbali mbali mkoani Geita.

Alisema miongoni hao wahamiaji haramu 750 waliokamatwa mkoani Kagera, 26 wamekatwa katika Manispaa ya Bukoba.
Kamanda Sirro alisema katika zoezi hilo, wahamiaji hao wanawapakia kwenye malori na kuwapeleka hadi mipakani wa Tanzania nan chi husika na kuwakabidhi kwa viongozi wan chi husika.

"Katika harakati za kutekeleza zoezi hili, suala la haki za binadamu tunazingatia sana, kwani wahamiaji haramu tunawaondoa kwa upole na utaratibu unaotakiwa"alisema

Alisema katika utekelezaji wa zoezi hilo, ametoa onyo kali kwa mtu yeyote ambaye watawarushia risasi maofisa wao, hawatakuwa na mchezo nao, tuko tayari kupambana na yeyote atakayejaribu kuwarushia risasi"

alisema."Huu si wakati wa kuchezeana kwa kurushiwa risasi, kwani muda waliopewa kusalimisha silaha ziliisha kama yeye ni raia mwema muda huu hatakiwi kuwa na silaha yoyote kinyume cha sharia, kama mtu anasilaha heri aitelekeze huko huko porini"alisisitiza.
Aidha aliwataka wananchi wenye haki wasihofu lolote waendelee na shughuli zao za maendeleo.

Kwa upande wa Mkuu wa mkoa wa Kagera, Kanali Fabian Massawe amewaka vyombo vinavyoendesha operesheni kuwa makini katika zoezi hilo kwa kuzingatia haki za binadamu.

Alisema wanatakiwa kuhakikisha wahamiaji haramu hao wanaondoka na vitu vyao na wananchi wasikubali kuwahifadhia mali zao.
"Kuna taarifa kuwa kuna baadhi ya wahamiaji haramu, wanawapatia wananchi kuwahifadhia mali zao, tunataka waondoke navyo na kama wana wauzia iwe katika maandishi mtu yeyote atakayebainika kuhifadhi vifaa vya wahamiaji haramu watakamatwa na kushtakiwa kwa kuhujumu nchi"alisema.

Aidha Kanali Massawe alisema katika zoezi hilo halitawakumba wale wahamiaji haramu wa kike waliolewa na Watanzania wanatakiwa kwenda idara ya uhamiaji ili kuweza kupewa hati maalum na baadaye kuhalalishiwa uraia wake.

"Katika utekelezaji wa zoezi hili kuna malalamiko kuwa wanawake ambao ni wahamiaji haramu wanarudishwa,
huku baadhi yao wakiwa na watoto watatu hadi sita, hatuko kwa ajili ya kutenganisha ndoa za watu, wale walioondoka bila kujua sheria wanatakiwa kurudi kama walivyoondoka"alisema.
Alisema lengo la serikali si kwa ajili ya kuachanisha familia za watu na wala hawatamfukuza mtu kwa vile amemwoa mhamiaji hamu katika utekelezaji wa agizo la Rais Kikwete.

Alisema kabla ya kuanza kwa zoezi hili jumla ya wahamiaji haramu 11,061 waliondoka mkoani Kagera, silaha 65 zilisalimishwa SMG zikiwa tatu,Short gun 10 na magobore 52.

Alisema pamoja na idadi hiyo kuondoka kwa hiari mkoa ulitazamia kuondoka kwa wahamiaji haramu 52,000 -53,000 hivyo idadi ya wahamiaji haramu bado ni kubwa.

Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa timu ya operesheni kwa kuwataja wahamiaji haramu
waliko ili sharia iweze kuchukua mkondo wake.
Juali 26, mwaka huu Rais Kikwete akiwa wilayani Biharamulo alisema operesheni hiyo ambayo itaendeshwa katika mikoa hiyo itakuwa ni ya aina yake ambayo haijahi kutokea katika nchi hii.

RORYA KWETU: Operesheni Kimbunga yaanza rasmi ya kuwarejesha wahamaji haramu makwao, ni agizo la Rais Kikwete
Huyo Kikwete tena kaingia vip hapo
 
Back
Top Bottom