Operation Sangara: Chadema yajipanga Upya

Baada ya uzinduzi uliofanyika Mbagala Zakhem, Operesheni Sangara ilizunguka katika kata mbalimbali za jimbo la Ukonga. Baada ya jimbo la Ukonga Operesheni hiyo sasa inakwenda katika jimbo la Ubungo. Siku ya kwanza katika jimbo tarehe 16 Januari itahusisha za: Goba(Hamad na wenzake), Kibamba(Ndesamburo na wenzake), Makuburi(Benson na wenzake), Mbezi(Zitto na wenzake) na Kimara(Mbowe na wenzake). Mtakaokuwepo viwanja hivyo mtujulishe yatayojitokeza. Nikipata ratiba ya tarehe 17 nitawaletea pia. Lakini siwaoni Dr Slaa na Mnyika katika ratiba hii. Wako wapi hawa?

PM
 
Slaa yuko ktk LAC- ni mwenyekiti na wabunge wengine wanazunguka wilayani na kamati yake kuzuia ufisadi usitokee kama wabunge wetu; naona amefika mwanza; na arusha sijui wataelekea wapi tena

Sangara watakamatwa tu sio daga kama wengi wanavyotaka hii operation isifanikiwe;

Mwaka huu mtaona Sangara wakikamatwa; ingawa shehe yahya hakuyasema haya
 
Kwa Dar operesheni hii inafanyika kwa taabu kidogo, mahudhurio ni hafifu, yote yayosemwa na viongozi hawa tayari tunayajua. Lakini waendelee tu wasikate tamaa.
 
Kwa Dar operesheni hii inafanyika kwa taabu kidogo, mahudhurio ni hafifu, yote yayosemwa na viongozi hawa tayari tunayajua. Lakini waendelee tu wasikate tamaa.

Mimi sijui lakini kama hizi ndizo strategy cha chama hiki tukuka kabisa... basi Tanzania we have a long way to go!
 
Huku Dar labda wangesema operesheni Papa maana Sangara hakai maji bahari!
 
Huku Dar labda wangesema operesheni Papa maana Sangara hakai maji bahari!

Na ndio maana wakaanzia huko kanda ya ziwa.Ama watu wa kanda ya ziwa si watanzania?
Issue hii ni ya Taifa so dont worry,Dar pia wanakula Sangara...Ama?
 
Nimesoma katika gazeti la leo la UHURU kichwa cha habari Operesheni Sangara kupingwa nchi nzima, Tamko hilo limetolewa na Baraza la Habari la Kiislam Tanzania (BAHAKITA) kupitia kwa mtu aitwaye Mwaipopo ( naamini siyo msemaji wa BAHAKITA, kama nimekosea nisahihishwe), katika mkutano na Waandishi wa Habari. Katika kufanikisha hilo kila Muumini ametakiwa achange shilingi 500 na kiasi cha shilingi milioni 100 zinatarajiwa kuchangwa. Zoezi hilo linatarajia kuanza Mkoani Mwanza.

My Take: Sidhani kama hawa wanawawakilisha Waislam wa Kweli, bali ni kikundi Fulani kinachojipendekeza kwa lengo la Kuganga Njaa na Serikali inabidi iwe makini sana na Vikundi kama hivi vyenye lengo la kuligawa Taifa katika Makundi ya Kidini!

Nitalishangaa sana Jeshi la Polisi kama litatoa Kibali kwa kikundi hiki kueneza Chuki Miongoni mwa jamii inayoishi pamoja bila kujali Mising ya Kidini!

Na Kama Serikali itakaa kimya tutaiuliza kama Imekituma Kikundi hiki.
 
1. Waislamu wanachangishana kumwondoa Sangara(Kikundi kidogo, BAKWATA wamekanusha kuwa hawahusiki)

2. CCM wanataka kumwondoa Sangara(Makamba amesema anaanzisha operesheni Nyavu, Wassira Operesheni Ndoano)

3. CUF wanasema Operesheni Sangara ni Mkakati wa CCM kuitumia CHADEMA kuiua CUF(Nao wameanzisha mkakati ondoa Sangara chini ya JUSSA)

4. TLP wanasema Sangara inachukua wanachama wake(Mrema naye ameanza kuiponda CHADEMA na Sangara)

5. NCCR wanasema Sangara inawahujumu(wamalia na Zitto)

Hivi huyu Sangara ni yupi haswa? Mbona ana muudhi kila mtu?

Kwanini kila mtu ni adui ya CHADEMA? Hivi CHADEMA ni chama cha siasa au kikundi cha magaidi? Kama sio magaidi, kwanini wanashambuliwa hivi kila kona?

Kwanini haishambuliwi SAU, CHAUSTA au vyama vingine kila siku ni CHADEMA, CHADEMA?

Asha
 
Asha, ukiona mambo yanakuwa hivyo, jua kuna madhara yameanza kuonekana kwa huyo sangara kuachiwa. Natamani waendelee hivyo hivyo. Maana, wanaweza kutuletea mwana mapinduzi wa kweli wa kuitoa nchi hii kwenye lundo la umasikini hadi kwenye neema. Usiogope Sangara kuchukiwa.
 
Kumbe CHADEMA walishavunja ushirikiano wa vyama kabla hata ya Mbeya Vijijini. Hii si kauli ya Mbowe hapa? Ndio maana Dr Slaa akatangaza ushirikiano ulifia Tarime nini?

Asha
 
Nasikia CHADEMA mmetua Dom,

I do believe on this move, safi sana na endelea kutuma SMS neno CHADEMA kwenda 15510. Kama nimekosea nirekebisheni. Wananchi wanahitaji kuelimishwa ila wabadilike FIKRA.
 
Utungwe wimbo maaluma mfupi wa kuamsha hisia na kukaa vichani mwa watu.
 
Chadema wanapata wapi pesa za kukodisha Helicopter for the whole Sangara Project?

Why other Opposition Parties fail?

Huu nao ni ufisadi tu. Leo sheria ya mapesa ya vyama inasainiwa, ndipo tutajua ukweli. Chadema ????? Hapana, labda sema wengine. Ukicheza wanaku - Chacha Wangwe.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA na Rais wa Madagascar hawana tofauti, wote ma-DJ. Nchi gani ya kuongozwa na DJ ????
 
Natumaini tena sasa UKAWA waje na staili dizain hii.

swissme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…