Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,521
- 96,267
Miaka yote ambayo zao la korosho limekuwa bei yake ipo juu na kuliingizia taifa mapato ya kujivunia sehemu kubwa ya korosho ilikuwa inavushwa mpaka kutoka msumbiji na kuingizwa Tanzania na inauzwa bila tatizo lolote,na ubora wake unalingana na zile za Tanzania yaani wastani wa sot 51-54 na nuts count zao ni kati ya 160-190.
Lakini leo hii wakubwa wa operation hii wanazizuia hizo korosho zisiingie tena nchini mwetu kwa kigezo kisicho julikana ni jambo la kushangaza sana na sijui wanamkomoa nani kati ya Tanzania na Mozambique?wilaya za Tandahimba na Newala zilikuwa zinanufaika na korosho nyingi kutoka Mozambique kwani tozo zote zilikuwa zinaingia kwenye wilaya hizo sasa hali imekuwa kinyume kabisa.kweli nimeamini ule usemi wa hasira za mkizi!!!