Riwaya:Op.Jicho la paka
Sehemu ya pili
Ilikuwa Jang’ombe,sasa ikashika pemba nzima,kisha ikafuatia unguja na Mafia,kote hakukalika,watu walikufa kama mchezo wa kuigiza.
Na hii ilikuwa ni habari mbaya kwa wapenda amani wa Afrika na dunia kiujumla.
*****
Night singer ahsubuhi hiyo ilimkuta akiwa kakaa kwenye tarakilishi yake na kazi aliokuwa akifanya ni kuhifadhi sauti aliorekodi usiku wa tukio la mauji ya mbunge wa viti maalumu Bi Kaisa.
Akaifunga tarakilishi yake na kisha akasimama na kujinyoosha viungo vya mwili wake kisha akaruhusu mwayo mkubwa umtoke.
Alipojirishisha na sayansi yake hiyo ya kujiondolea uchovu akayatwaa mavazi yake ya kiheshima,ilikuwa ni suti ya kisasa kabisa,kisha akakisogelea kioo chake kilichokuwa kimewekwa ukutani akajitizama.
Dakika tano baadae zilimkuta akiwa amesimama nje ya nyumba yake na alikuwa anatia ufunguo kwenye gari yake corola mbovumbovu,kisha akakamata barabara ambayo haikuwa mbali na nyumba yake kisha akaanza safari yake.
Gari yake ilisimama nje ya uzio wa geti la gereza Kuruso,kisha akashuka na kujitizama mbele ya kioo cha corola yake kilichokuwa kimepasuka katikati,kwa mbali akatabasamu baada ya kuiona sura yake ilivyobadilika na moyoni alikiri ya kuwa asingelikuwa ni yeye mwenyewe basi angejisahau.
Akataka kupiga hatua kuingia ndani ya lango kuu,lakini kabla hajapiga hatua zaidi akatokea askari magereza mwenye nembo maalumu ilioonesha yeye ni kutoka kikosi maalumu cha magereza au wenyewe huitwa makomando wa gereza.
“Mzee hujasikia tangazo huko ulikotoka!?”
“Sijasikia kiongozi!?”
“ok kifupi ni kuwa hamtakiwi kukanyaga hapa kwa wiki yote hii kwa raia wote wenye ndugu zao hapa na wageni wa aina yoyote”
“Kwanini kiongozi!”
Askari yule akaona kama anadhihakiwa kwa maswali mengi wakati mgeni huyo anajua kabisa nchi imechafuka na pengine kubwa hakujua ya kuwa kuna mfungwa katoroka,mfungwa hatari kuliko hatari yenyewe na ndio maana hadi kikosi maalumu cha askari magereza kipo pale.
Askari yule akaona anadhihakiwa akataka kujiandaa kumshambulia night singer ambae alikuwa amejibadilisha pakubwa sana .
Night singer aliona mienendo ya askari yule na hivyo akajipanga kumkabiri japo aliamini halikuwa jambo la busara kumkabiri eneo kama lile.
Kabla askari yule mwenye gadhabu za nyegere hajatimiza adhima yake,wote masikio yao yakanasa sauti ya king’ora cha tahadhari kutoka kwenye vipaza sauti vilivyokuwa vimefungww kila kona ya gereza lile.
Askari yule kama alieona Simba jike akakimbia kuelekea ndani ya lango la kuingilia mle ndani na hapo ndipo Night singer akapanda corola yake na kupotea eneo lile huku nyuma akiacha kimbembe ndani ya gereza lile.
Hakwenda mbali sana,akapaki pembeni mwa barabara na kujiunga na baadhi ya raia kushangaa moshi mkubwa uliokuwa ukitoka ndani ya gereza lile.
Penye wengi hapakosi jambo,Night singer akasikia wamama wakiteta kuhusu kinachoendelalea ndani ya gereza lile.
“Mwanaisha nasikia usiku wa kuamkia leo kuna mfungwa katoroka gerezani”
“ Na mimi nimesikia hivyo” alieitwa Mwanaisha akajibu lakini mwingine nae akadakia
“Jamani sasa kigereza kidogo hivi kwanini katoroka,si nasikia hapa wanaletwaga wanaomalizia kifungo chao?!”alimaliza kuongea na kutupia kiswali.
Night singer akatabasamu na kisha akainyoshea serikali mikono kwa kuwahadaa watu kuhusu gereza lile la Kuruso.
Kitu ambacho wakazi wa eneo lile hawakufahamu na hawajawahi kuambiwa kuhusu gereza lile ni kuwa,pale hawakufungwa wafungwa wa kawaida tu,kulikuwa na wafungwa wa maisha pale,wafungwa ambao serikali haitaki watu wajue sehemu walikofungwa,wafungwa wengi walikuwa ni makomamdo au majasusi walionekana wanatishia usalama wa nchi.
Gereza hili la Kuruso lilikuwa na sehemu mbili na aina mbili za wafungwa.
Sehemu ya kwanza ilikuwa ni juu ambako walifungwa wafungwa wanaomaliza kifungo chao hivi karibuni lakini sehemu ya pili ilikuwa ni sehemu ambayo ilikuwa imejengwa chini ya ardhi na huko ndiko walikofungwa watu wenye makosa ya ajabu au waliwekwa watu waliokuwa wanahatarisha usalama wa nchi.
Ajabu ni kuwa hata wafungwa wajuu hawakujua kama chini ya vyumba vyao kuna watu wanaishi huko na hata baadhi ya askari magereza hawakujua ya kama kuna sehemu ndio njia hasa ya kuingilia huko chini.
Night singer alikuwa ameenda pale kwa nia ya kuangalia usalama na mazingira yalivyokaa,kuna mtu akihitaji kukutana nae au kumuokoa na alijua ni miongoni mwa wafungwa walitangazwa ya kuwa ni adui wa taifa na wakaamua kumfungia pale.
Itaendelea