Operation Jicho la Paka na dakika za Mwisho(with Wolf rules )

Operation Jicho la Paka na dakika za Mwisho(with Wolf rules )

Asante sana kudo.hadithi nzuri na kwa sasa tupo vinyumbani visiwani znz
 
Mkuu Kudo 900 pls, pls tenganisha story wengine ni vichwa vya panzi tutapata taabu sana kuelewa na kwendana na mwendelezo.!!
 
Mkuu Kudo 900 pls, pls tenganisha story wengine ni vichwa vya panzi tutapata taabu sana kuelewa na kwendana na mwendelezo.!!
Sawa itaendelea moja
 
Op.Jicho la Paka

Sehemu ya tano

Alijibu kisha akaanza kutoka ndani ya chumba kile na alipofika nje akasimama na kufikiria kuhusu maamuzi ya rais ya kupeleka familia yake nje ya nchi,maswali kadhaa yalipita kichwani pake lakini hakupata majibu yeye akabaki msikilizaji tu na mtekelezaji.

Maongezi ya rais na mkurugenzi yule wa cobra squad yalikuwa yanasikiwa na mtu nje ya Ikulu na kisha mtu yule akapiga simu pahali flani

“ameanza kuhaha na sasa anahamisha familia yake nje ya Ikulu…..ndio..eh Uganda…ok tutajitahidi tujue wanapitia njia gani, OK” kisha akakata simu na kuwageukia vijana sita waliokuwa wamemzunguka na kusema nao

“Wewe Chitah hakikisha unazurura eneo la nje ya Ikulu saa ishirini na nne kuanzia sasa na utatupa taarifa kila baada ya msafara wowote unapotoka Ikulu”

Aliepewa maagizo kwa jina la chitah akaitikia kisha haraka akatoka ndani ya chumba kile hivyo kufanya waliosalia kuwa watano na mtoa maelekezo ni wa sita.

“Jongo kazi yako ya jana umefanya lakini hili sio faili la classified hivyo unatakiwa kulitafuta haraka sana na Safari hii inakupasa mtu wa kumtafuta ni kanali mstaafu bwana Zwange,kumbuka bila hili faili hakuna tunachopigania na taarifa tulizonazo kutoka usalama wa taifa kitengo cha kuhifadhi kumbukumbu faili hili la mwaka 1997 halipo na hata rais mwenyewe hajui lilipo na hili ndio roho yake na mauti kwetu,nadhani unatakiwa kuanza safari sasa na urudi ukiwa nalo mkononi”

Alimaliza kusema mwagizaji na hapo bila kuuliza mtu alieitwa Jongo akaondoka ndani ya chumba kile.

Na wakabaki wanne na mwagizaji wa tano.

“Nimesikia katoroka gereza la Kurusu na ninachojua lazima aje hapa Dar es laam hivyo nyinyi hakikiseheni mnafuata nyendo za watu wote wanaoshuka na boti za Kilimanjaro ahsubuhi hii na ninavyojua lazima atataka kumuua rais hivyo hakikisheni hafanyi kingine zaidi akienda kinyume ueni sisi tutamaliza wenyewe kazi ya kuchukua nchi japo yeye nchi si hitaji lake,Angalizo kwa wote..” alisita kusema mwagizaji kisha akawatazama vijana imara waliokuwa wakimsikiliza kisha akaendelea

“mtu yule ni hatari kuliko hatari yenyewe anaogopwa na kila mwanajeshi wa nchi hii na anaogopwa na viongozi wote wakiliokuwa nyuma ya Operation Jicho la Paka mwaka 1997,mfano mdogo tu kaweza kutoroka ndani ya gereza la kuzimu kiajabu na hakuna anajua aliwezaje hivyo kuweni makini na kila hatua mnayopiga yule mtu ni zaidi ya jini.”
Alimaliza kusema na hapo vijana wake hawakuwa na cha kusema zaidi kila mtu alitoka ndani ya chumba kile na kwenda kutekeleza agizo.

Mwagizaji akabaki peke yake na kisha akanyanyua simu na kupiga nje ya nchi na huko akapokea maagizo kadhaa na kukata simu kisha akashusha pumzi nyingi na kuegemea kiti cha kisasa ndani ya chumba kile.

Mwaka 2006
KOME ISLAND UGANDA

Chopa aina ya Chinook isiokuwa na mlio ilikuwa imeganda angani mita mia kutoka usawa wa bahari na kulikuwa na makomando wapatao kumi na nne.

Waliteremka kwa kutumia kamba huku waliokuwa wametangulia wakiwa kufika chini wakiwa wanaangaza kila kona kuhakikisha usalama kwa wanashuka eneo lile.

Ilikuwa ni operation ya kufa ama kupona na sasa waliokuja kuifanikisha ndio walikuwa wanamalizikia kutua chini.

Makomando wale walikuwa wamejizatiti kwa silaha nzito aina ya bulggutc12 yenye kiwambo cha kuzui sauti.

Sifa kuu ya silaha ile ni kuwa ilikuwa na uwezo wa kupachikwa silaha nyingine ubavuni kwake na pia ilikuwa na uwezo wa kutoa risasi na eggrunate kwa wakati mmoja.

Masikio ya makomando yalikuwa yamezibwa kwa vitoa sauti vya kisasa kabisa huku kila kinasa sauti kikiwa na kimeunganishwa na vinasa sauti vilivyokuja hadi usawa wa mdomo wa kila komando.

Komando walipohakikisha wametua chini salama kiongozi wa makomando wale kumi na nne Luten kanal Mwinyi Kisoda akatoa ishara kwa kila komando angojee amri yake huku yeye muda huo akizungumza na rubani wa chopa iliowashusha

“go rout eigt and wait” alisema Luten kanal Mwinyi Kisoda.

“copied soldier!!”alijibu rubani wa chopa ile Luten Haji Makame kisha akaiondosha na kwenda usawa alioelekezwa huku akingoja kukamilika kwa operation ile na kuwachukua salama makomando wenzie.

Mvua na upepo mkali ulikuwa ni adha nyingine kwa makomando wale lakini walifunzwa namna ya kukabiliana na hali ya hewa ya aina yoyote.

Luten kanal Mwinyi Kisoda alikuwa amevaa koti ya kijeshi iliokatwa mikono na kumfanya awe na kizibao kilichokuwa juu ya vest ya madoa madoa,kichwani alijivika kitambaa kilichokuwa kimezunguka kichwa chake chote huku mdomoni akiwa na njiti aliokuwa anaizungusha kutoka kushoto mwa kingo za midomo yake hadi kulia mwa kingo za midomo yake.

Machoni alikuwa amevaa mawani pana yaliomsaidia kuona ndani ya kiza kile.

Makomando wenzie walikuwa wapo makini kungojea amri kutoka kwake na kila mmoja alikuwa na ari na jambo walilokuwa wanataka kulifnya ndani ya kisiwa hicho usiku huo.

Itaendelea
 
Back
Top Bottom