Op.Jicho la Paka
Sehemu ya sita
Makomando wenzie walikuwa wapo makini kungojea amri kutoka kwake na kila mmoja alikuwa na ari na jambo walilokuwa wanataka kulifnya ndani ya kisiwa hicho usiku huo.
Luten kanali Mwinyi Kisoda aliwapa maagizo vijana wake waliounda kikosi cha 309 unit.
“Kila kitakachoonekana tofauti na lengo ni kuua na kuwakomboa mateka wote ndani ya ndege,kuna mateka zaidi ya ishirini na sita akiwamo rubani wa ndege ya AirZanzibar,na kwa mujibu wa taarifa zinasema mateka wote wamewekwa upande wa mashariki mwa ngome.” Alimaliza kuwapa maelekezo muhimu na kabla hajaendelea akawatazama wenzie waliokuwa kimya wakimsikiliza na walikuwa wamengojea amri yake tu ili vijana wasonge mbele.
“Koboko mtaelekea upande wa kusini na mtangojea amri kutoka kwetu endapo tutahitaji usaidizi na Luten Zaza utaongoza huko mimi na wengine saba tutaenda kufanya wokozi kwa kupitia mbele,idadi ya watekaji ni chini ya kumi na tano” alimaliza kusema na kuanza kuondoka huku vijana saba wakiwa wanamfuata nyuma na kikundi cha koboko kilichoongozwa na komando Luten Zaza nacho kilifuata uelekeo walioaelekezwa.
Ulikuwa ni mwendo wa kukimbia katikati ya msitu wa miti mifupi ndani ya kisiwa cha Kome.
Luten kanali Mwinyi Kisoda alikuwa mbele huku mwili wake uliojaa kimazoezi ukionekana kila radi ilipopiga na hivyo makomando wenzie walikuwa wakiona kiwiliwili chake vile kilikuwa kinakata giza usiku ule huku bunduki yake ikiwa mkononi tayari kwa lolote.
Ngome ya kikundi cha waasi wa LRA ilikuwa tulivu usiku huo na kutokana na mvua kuwa kubwa walinzi wa nje wengi waliamua kwenda kwenye mahema na kujihifadhi huku akili zao zikiwaza mabilioni ya fedha walioyahitaji kutoka kwa serikali ya Tanzania ili waweze kuwachia mateka zaidi ya Ishirini na tano wa timu ya mpira ya Zanzibar iliokuwa inaenda kushiriki michezo ya kirafiki nchini Uganda.
Kiongozi wa waasi wale bwana Mangazeni Nkunda ndie alikuwa anajua kitakachojiri usiku ule hivyo kila mara alikuwa anatazama saa yake ya mkononi na ilipofika majira ya saa tano na nusu usiku akachukua simu yake iliokuwa mezani akapiga pahali na kusikiliza upande wa pili kisha maongezi yakaendelea
“Chopa ipo upande gani…ok vikosi vingapi..ok..”kisha akakata simu na moja kwa moja akawageukia vijana wake aliowaamini na kuwambia “Kumekucha wapo hapa”hakungoja swali akachukua koti lake la baridi na kulivaa kisha akachukua bastola zake tatu na kuzisunda maeneo tofauti ya mwili wake kisha akachukua na mabomu mawili ya kutupa kwa mkono na kuyaweka mifukoni na haraka akaamuru vijana wake wapitie njia ya magaribi kutoka ndani ya ngome ile na kweli hiyo ndio ilikuwa salama yake maana vijana wa 309unit walikuwa upande wa mashariki na wengine kusini wakiikaribia ngome ile.
Nchini Tanzania usiku huo.
Waziri wa ulinzi na waziri wa mambo ya ndani wa Zanzibar walikuwa wapo ndani ya kikao usiku ule na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania bwana Mwenda Mpya.
“mheshimiwa C. D. F anangoja sahihi yako ili operation hii ikamilike na watu wetu wakombolewe”alisema waziri wa ulinzi
“Au kwa kuwa waliotekwa ni wazanzibar basi Rais hutaki kusaini operation hii..”alizungumza waziri wa mambo ya ndani wa Zanzibar aliekuwa ndie mwakilishi wa Rais wa Zanzibar ambae alikuwa nje ya nchi kikazi.
Rais alimtazama waziri wa mambo ya ndani wa Zanzibar kisha akamuuliza kiupole kama ilivyodesturi yake hasa anapokuwa amekwazika
“Wazanzibar sio watanzania?”
“ila mhe…” hakumaliza kuongea waziri yule na haraka Rais akaendelea
“bwana Makoye naona unataka kufanya haya mambo kwa mihemko na sasa unaleta ubara na visiwani,mimi ni Rais wa wote na kabla sijafanya maamuzi inatakiwa nijue madhara na faida ya uamzi huo na sijaona sababu ya kupeleka wokozi wakati watekaji wanafanya mazungumzo ya kumaliza hili jambo bila ya kumwaga damu na sioni sababu ya kuharakisha jambo hili,Makoye kumbuka wale ni waasi na hawana cha kupoteza.
Alizungumza Rais na Waziri wa ulinzi akatikisa kichwa kukubaliana na jambo lile huku Waziri wa mambo ya ndani akiwa amenuna kwa kuona mawazo yake hayajaafikiwa.
Rais aliagiza wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waingie katika kikao kile na hapo CDF,IGP,na DG walijumuika katika kikao kile ndani ya ikulu.
Ni katika utoaji wa taarifa ndipo mkuu wa majeshi alipokutana na ripoti ya kumstua ambayo hakuwa ameona katika nyaraka zake huko mwanzo.
Kulikua na ripoti kutoka kwa Major jeneral Kambi Kibeyo aliekuwa na jukumu la kusimamia kambi zote upande wa Zanzibar.
Ripoti hiyo ilikuwa inatoa taarifa ya kuruhusiwa kikosi cha makomando cha 309 kilichokuwa kimekwenda Kome usiku huo kufanya wokozi.
Taarifa hiyo iliibua tafrani ndani ya Kikao kile huku Waziri wa mambo ya ndani Zanzibar akichelea moyoni.
Itaendelea