OPERATION GOTHIC SERPENT: Nguvu ya Itikadi, Imani na Ushujaa uliotukuka

OPERATION GOTHIC SERPENT: Nguvu ya Itikadi, Imani na Ushujaa uliotukuka

images (70).jpeg
 
OPERATION GOTHIC SERPENT: NGUVU YA ITIKADI, IMANI NA USHUJAA ULIOTUKUKA




FINALE


Kwa muda wa siku kumi na moja Mohammed Farrah Aidid aliendelea kumshikilia rubani wa Super 64 Michael durant. Kwa siku zote hizi Farrah Aidid alikuwa akitoa matakwa yake juu ya vitu ambavyo alikuwa anataka vifanyike ili amuachie Michael Durant. Na sharti lake kuu alikuwa anataka vikosi vya UNOSOM wakiongozwa na Marekani kuondoka Somalia.
Lakini pia Adid alisambaza video za propaganda zikimuonyesha Michael Durant akiongea kupinga uwepo wa Wanajeshi wanzake wa Marekani juu ya uwepo wao ndani ya Somalia. Ni dhahiri kabisa kwamba Michael Durant alikuwa analazimishwa kusema kile ambacho alikuwa anakiongea.

Mpaka leo hii kuna utata mkubwa ya ni namna gani hasa Marekani waliweza kumshawishi Aidid kumuachia Michael Durant.
Ziko ripoti ambazo zinaeleza kwamba Marekani walilipa kiasi cha dola Milioni 10 ili kuachiwa kwa Michael Durant na mjadala juu ya malipo haya unazua nadharia juu ya kushamiri kwa uharamia katika pwani ya bahari ya hindi na hasa hasa kwenye pembe ya Afrika (tukipata nafasi tutajadili zaidi suala hili).

Mohammed Farrah Aidid alimuachia Michael Durant kwa shirika la misaada la msalaba mwekundu baada ya siku kumi na moja za kumshikilia. Baada ya Michael Durant kupatikana tu haraka alichukuliwa na jeshi na kusafirishwa kwenda nchini Ujerumani kwenye kituo cha tiba za kijeshi cha Landstuhl Regional Medical Center ambako alikaa kwa wiki kadhaa akitibiwa na kufanyiwa upasuaji kurekebisha paja na sehemu ya uti wa mgongo ambazo alivunjika kwenye ajali ya chopa ya Super 64.

Nilieleza kwamba miili ya wanajeshi wa Marekani ambao ilikuwa imechukuliwa kutoka kwenye chopa zilizodondoka, yaani Super 61 na Super 64 ilichukuliwa na wananchi na kuburuzwa barabarani na kudhalilishwa mno.
Wiki moja baadae jeshi la Marekani waliwabana viongozi wa koo za kisomali wakitaka miili ya wanajeshi wao irejeshwe. Ulikuwa ni mzozo mkubwa kweli kweli mpaka kufikia hatua ya Marekani kutishia kuingiza majeshi zaidi nchini Somalia ndipo ambapo viongozi wa koo za kisomali wakafanya juhudi za kusaka miili hiyo mpaka kupatikana na yote kurejeshwa kwa jeshi la Marekani. Miili ilikuwa katika hali mbaya kabisa na mengine ikiwa haina vichwa.

Mapigano haya ambayo nimeyaeleza kwenye makala hii ambayo kwenye vitabu vya historia yameandikwa kama "Vita ya Mogadishu" ni moja ya vipigo vya aibu kabisa na maumivu makali ambayo jeshi la Marekani limewahi kupata.
Kutokana na maumivu haya ba aibu hii, waziri wa ulinzi wa Marekani wa kipindi hicho Les Aspin alilazimika kujiuzuru na kuchukua lawama zote kutokana na kufeli kwa aibu kwa opareshenu hiyo. Moja ya masuala ambayo Waziri Aspen analaumiwa sana ni kitendo cha kukataa kuidhinisha kutumika kwa vifaru na magari ya silaha nzito na katika mapigano hayo.
 
images (72).jpeg


Siku ya octoba 6 1993, Rais Bill Clinton aliitisha kikao kikao cha tathimini katika Ikulu ya Marekani ambapo kupitia kikao hicho alimuagiza Mwenyekiti wa kamati ya Majemedari (Chairman of the Joint Chiefs of Staff) Jemedari David E. Jeremiah kuagiza vikosi vya jeshi la Marekani vilivyopo nchini Somalia kujiondoa katika mapambano yoyote yale dhidi ya wapiganaji wa Aidid isipokuwa tu kama ni kwa ajili ya kujilinda.

Kuanzia Tarehe 31 March 1993 majeshi ya Marekani yalianza kuondoka nchini Somalia. Vikosi kadhaa vya Marines vilibakia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba raia wa kawaida wa Marekani walioko ndani ya Somalia wanaondoka wakiwa salama.

Kujitoa huku kwa Marekani kulileta mpasuko mkubwa katika diplomasia za kimataifa kutokana na mataifa mengi kutounga mkono kujitoa kwao ghafla hivyo. Tukumbuke kwamba vikosi vya Marekani vilikuwa ni sehemu ya vikosi vya umoja wa mataifa vya UNOSOM kwa ajili ya kusaidia usambazaji wa misaada ya kiutu nchini humo.
Nchi ya Somalia ilikuwa bado haijatulia, mapigano ya kikabila yalikuwa yameshika kasi na Aidid alikuwa amejilimbikizia madaraka makubwa sana. Kwa hiyo kujitoa kwa Marekani katika misheni hiyo bila kukamilika kwake ulikuwa ni usaliti mkubwa kwa jumuiya ya kimataifa.
Lakini vyombo vya habari vya Marekani vilikuwa vimeikalia kooni serikali ya Rais Bill Clinton. Picha za maiti za wanajeshi wa Marekani zikiburuzwa na kupigwa mawe kwenye mitaa ya Mogadishu zilionyeshwa kwenye televisheni. Wananchi walijawa na hasira. Na katika Bunge, wawakilishi wa chama cha Republicans walishupaa kweli kweli kwamba wanataka jeshi lao liondolewe nchini Somalia, hawawezi kuvumilia kuona jeshi likidhalilika namna hiyo. Hii ndio ilikuwa presha iliyomfanya rais Bill Clinton kuagiza vikosi vya Marekani virudi nyumbani.


Jinamizi hili la kudhalilika nchini Somalia ndilo ambalo Marekani walitumia kujitetea kwa kushindwa kwao kuingilia kuzuia mauaji ya Kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.


Vita ya Mogadishu na Operation Gothic Serpent kwa ujumla inabakia kama moja ya misheni za machungu zaidi kuwahi kushuhudiwa na jeshi la Marekani. Ubaya zaidi kuna masuala mengi sana ambayo yalipata mwanya masuala mengine makubwa nyuma ya pazia. Kama amabavyo nimesema kwamba tukipata wasaa unaofaa tutajadili namna ambavyo uharamia katika pembe ya Afrika ulipata mwanya wa kushamiri baada ya kipindi hiki.

Lakini suala lingine ambalo kwa kipindi kile halikutiliwa maanani sana ni Osama Bin Laden. Kwa kipindi kile Marekani walikuwa wanajua juu ya uwepo wa Al-qaida na Osama Bin Laden lakini hakikuwa kitu ambacho wanakitilia maanani sana kwa kuwa hawakuwahi kutekeleza misheni yoyote kubwa ya kuigharimu nchi ya Marekani. Jambo ambalo hawakulifahamu kipindi kile ni kwamba, nyuma ya pazia ya umahiri wa wapiganaji wa Mohammed Farrah Aidid alikuwa ni Osama Bin Laden.
Kama umesoma kwa makini makala yangu ya "Behind The Curtain" utakumbuka kwamba katika kipindi hiki ndipo ambapo Osama Bin Laden alikuwa amejificha ndani ya nchi ya Somalia. Ni vijana wa Osama Bin Laden wakiongozwa na Mohamed Atef ambao walihusika kuwapa mafunzo mapiganaji wa Mohammed Farrah Aidid. Katika kitabu changu ambacho kitatoka siku si nyingi, nimejadili pia namna ambavyo kuna kijana wa Kitanzania kutoka Zanzibar ambaye alikuja kuigharimu sana nchi yetu na ulimwengu (tuhifadhi jina kwa sasa (sio Mohammed Ghailani)) alivyosafiri mpaka Somalia kwa mualiko wa Mohammed Atef kwa niaba ya Osama Bin Laden na kupata mafunzo pamoja na vijana wa Mohammed Farrah Aidid.

Lakini pia ni Al-Qaida ambao waliwezesha kudungua chopa zile mbili za Black Hawk na kuwatia wazimu Wamarekani.
 
ca4916c52d50426697b110df71b4bb7e_18.jpg


Masuala haya (Al-Qaida kumsaidia Aidid) yalithibitishwa pia na Osama Bin Laden mwenyewe alipofanya mahojiano na John Miller wa kituo cha habari cha ABC cha nchini Marekani mwaka 1998 katika eneo lisilojulikana. Katika mahojiano yale ukimsikiliza Osama namna ambavyo anawakashifu wanajeshi wa Marekani kama 'cowards', unawez kuelewa ni kwa namna gani kukimbia kwa vikosi vya Marekani nchini Somalia kulitumiwa na watu kama Osama kipropaganda kuwatia moyo vijana wake wasiogope jeshi la Marekani.

Kuna mengi ya kujifunza kijeshi, kiitikadi na hata kiimani na pengine kuchochea ushujaa kutoka kwenye kisa hiki cha Vita ya Mogadishu na Operation Gothic Serpent. Licha ya vikosi vya Marekani kuwa na silaha za kisasa zaidi na weledi zaidi wa kijeshi, lakini vijana wenye mori ya itikadi na imani wakiwa na mapanga na mundu tu mikononi waliweza kuwatoa jasho na mpaka kusalimu amri. Ni mara chache sana katika maisha ambapo tunapata kukumbushwa na kushuhudia kwa macho yetu namna nguvu hii ya itikadi na imani lakini pia hatupaswi kubeza ushujaa uliotukuka ulioonyeshwa na makomando wa Marekani.


MWISHO


Makala mpya inakuja wiki hii…

Ramadhan Kareem


Habibu B. Anga "The Bold"
To Infinity and Beyond
 
View attachment 802402

Masuala haya (Al-Qaida kumsaidia Aidid) yalithibitishwa pia na Osama Bin Laden mwenyewe alipofanya mahojiano na John Miller wa kituo cha habari cha ABC cha nchini Marekani mwaka 1998 katika eneo lisilojulikana. Katika mahojiano yale ukimsikiliza Osama namna ambavyo anawakashifu wanajeshi wa Marekani kama 'cowards', unawez kuelewa ni kwa namna gani kukimbia kwa vikosi vya Marekani nchini Somalia kulitumiwa na watu kama Osama kipropaganda kuwatia moyo vijana wake wasiogope jeshi la Marekani.

Kuna mengi ya kujifunza kijeshi, kiitikadi na hata kiimani na pengine kuchochea ushujaa kutoka kwenye kisa hiki cha Vita ya Mogadishu na Operation Gothic Serpent. Licha ya vikosi vya Marekani kuwa na silaha za kisasa zaidi na weledi zaidi wa kijeshi, lakini vijana wenye mori ya itikadi na imani wakiwa na mapanga na mundu tu mikononi waliweza kuwatoa jasho na mpaka kusalimu amri. Ni mara chache sana katika maisha ambapo tunapata kukumbushwa na kushuhudia kwa macho yetu namna nguvu hii ya itikadi na imani lakini pia hatupaswi kubeza ushujaa uliotukuka ulioonyeshwa na makomando wa Marekani.


MWISHO


Makala mpya inakuja wiki hii…

Ramadhan Kareem


Habibu B. Anga "The Bold"
To Infinity and Beyond

Ramadhan imeisha boss, tunasubir story nyingine
 
View attachment 802402

Masuala haya (Al-Qaida kumsaidia Aidid) yalithibitishwa pia na Osama Bin Laden mwenyewe alipofanya mahojiano na John Miller wa kituo cha habari cha ABC cha nchini Marekani mwaka 1998 katika eneo lisilojulikana. Katika mahojiano yale ukimsikiliza Osama namna ambavyo anawakashifu wanajeshi wa Marekani kama 'cowards', unawez kuelewa ni kwa namna gani kukimbia kwa vikosi vya Marekani nchini Somalia kulitumiwa na watu kama Osama kipropaganda kuwatia moyo vijana wake wasiogope jeshi la Marekani.

Kuna mengi ya kujifunza kijeshi, kiitikadi na hata kiimani na pengine kuchochea ushujaa kutoka kwenye kisa hiki cha Vita ya Mogadishu na Operation Gothic Serpent. Licha ya vikosi vya Marekani kuwa na silaha za kisasa zaidi na weledi zaidi wa kijeshi, lakini vijana wenye mori ya itikadi na imani wakiwa na mapanga na mundu tu mikononi waliweza kuwatoa jasho na mpaka kusalimu amri. Ni mara chache sana katika maisha ambapo tunapata kukumbushwa na kushuhudia kwa macho yetu namna nguvu hii ya itikadi na imani lakini pia hatupaswi kubeza ushujaa uliotukuka ulioonyeshwa na makomando wa Marekani.


MWISHO


Makala mpya inakuja wiki hii…

Ramadhan Kareem


Habibu B. Anga "The Bold"
To Infinity and Beyond
Mkuu samahani naona sehemu ya nne iliishia hapa naomba muendelezo nn kilitokea hapo


(Vijana wa kisomali walio na silaha za moto, wenye mapanga, majembe, mundu, akina mama na mpaka watoto, kama vile tai wakisikia harufu ya mzoga mahala… walimiminika kwa makundi ya mamia ya watu wakikimbia kuelekea Super 64 ilikodondoka. Hii ilikuwa ni siku ya sherehe na siku ya msiba… siku ya kupimana misuli kati ya imani na itikadi dhidi ya misuli ya weledi na ushajaa.)


Sent using Jamii Forums mobile app
 
mbona mwanzo wa story paka mwisho sijaona andishi kwamba kuna wasomali walikufa au wewe mwandishi ni msomali nn?
 
OPERATION GOTHIC SERPENT: NGUVU YA ITIKADI, IMANI NA USHUJAA ULIOTUKUKA

View attachment 729968

Tarehe fulani isiyojulikana mwaka 1993 - Sudan

"…ndugu zangu nyote katika imani, popote mlipo dunia. Wote tumeshuhudia udhaifu wa adui yetu. Wote tumeshuhudia kudhalilika kwa Marekani. Hili ni onyo, na huu ni ujumbe kwao. Kwamba tutawapiga tena, na tena na tena mpaka siku tutakapowafuta juu ya uso wa dunia au siku watakapo ongoka na kumuamini Mwenyezi Mungu. Huu ni ushindi kwetu sote na ishara ya kwamba adui yetu ni dhaifu. Nawataka wapigania imani wote, popote mlipo duniani, endeleeni kuwa na moyo mkuu. Adui yetu ni dhaifu, tumpige tena na tena na tena.."

- Sauti ya Osama Bin Laden katika moja ya rekodi zilizokuwa zinasambazwa kwa vikundi vya wapiganaji wenye msimamo mkali.




Nchini Marekani mwaka huo huo 1993

Wananchi wa Marekani walikua wamemka na habari ya kushtua. Vyombo vyote vya habari vilikuwa vimetawaliwa na habari juu ya kujiuzulu kwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani Bw. Les Aspin.

Ilikuwa ni habari ya kushitusha kuzingatia kwamba nchi bado ilikuwa imefunikwa na giza kutokana na kifo cha idadi kubwa ya wanajeshi wake barani Afrika.

Wakati huo huo rais Bill Clinton alikuwa kwenye mvutano mkubwa na Umoja wa Mataifa juu ya muelekea wa hali ya amani nchini Somalia. Bill Clinton akitaka kuondoa wanajeshi wake haraka huku Umoja wa Mataifa wakitaka Marekani kusubiri kidogo ili kuongoza oparesheni ya kuondoa wanajeshi wengine wote wa UN waliopo nchini humo.



Mogadishu, Somalia - Pembe ya Afrika

Mamia ya wananchi walikuwa wameandamana. Si kwamba walikuwa wameandamana kupinga jambo fulani au kuhamasisha suala fulani, la hasha… maandamano haya yalikuwa ni ya kusheherekea. Walikuwa wanasheherekea huku wakiwa na 'trophy' mbele yao. Mwili wa binadamu aliyekufa ambao walikuwa wameufunga kamba wakiuburuza mitaani wakiwa wameuvua nguo zote mwili huo. Tofauti na muonekano wa waandamanaji hawa ambao wengi walikuwa wembamba na weusi na sura za kuchongoka, mwili huu waliokuwa wanauburuza ulikuwa ni wa mtu mweupe, mzungu. Ulikuwa ni mwili wa mwanajeshi wa Marekani, mmoja wa mwanajeshi wa weledi ambaye alikuwa kwenye chopa ya kivita ya 'Super Six Four'.


Ulimwengu wote ulikuwa kana kwamba umesimama na macho na masikio yote yalikuwa yameelekezwa nchini Somalia. Hakuna ambaye alikuwa anaamini kilichotokea. Hata Marekani wenyewe hawakutegemea kutokea kitu ambacho walikuwa wanakishuhudia.

Siku hii imeingia katika historia ya jeshi la Marekani kama moja ya siku chungu zaidi ambazo waliwahi kupitia. Ni siku ambayo kwa mara ya kwanza tangu kuisha kwa vita ya Vietnam, wanajeshi wa Marekani ndipo walipokabiliwa na mapigano mazito ya ana kwa ana na adui.

Lakini pia siku hii itufundisha kitu adhimu sana… kwamba hasira, imani na itikadi inauwezo wa kupambana dhidi ya weledi na ushujaa wa hali ya juu na ikashinda.

View attachment 729970

View attachment 729972


Genesis

Katika miaka ya 1986 Rais wa Somalia wa kipindi hicho, Mohammed Siad Barre alipata ajali ya gari katikati ya mji wa Mogadishu. Ajali hii ilitokana na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa ambao ulisababisha gari ambayo ilikuwa inatumika kumsafirisha kwenda kujibamiza nyuma ya gari kubwa la usafiri wa umma. Rais Barre alipata majeraha makubwa sana, hasa hasa kichwani na pia alivunjika mbavu kadhaa. Ilibidi asafirishwe kwenda kutibiwa nchini Saudi Arabia kwa ajili ya matibabu.

Kwa miezi kadhaa ambayo Rais Barre alikuwa kwenye matibabu nchini Saudi Arabia, Jenerali Mohamed Ali Samatar ambaye alikuwa makamu wa Rais ilibidi akaimu nafasi yake na kuongoza nchi kama Rais wa Somalia.

Katika nyanja za siasa na masuala ya madaraka nchini humo kukaanza kuibuka minong'ono ya kutaka apatikane mrithi wa Urais wa Somalia. Barre alikuwa ameitawala Somalia kwa kipindi kirefu sana, umri wake ulikuwa umeenda mno na pia watu walikuwa na shaka na uimara wa afya yake.

Hata kipindi ambacho Rais Barre alitibiwa na kurejea kwenye afya njema na kurudi nyumbani Somalia, bado minong'ono iliendelea ya kutaka apatikane mrithi wake.
Ili kuonyesha kwamba yuko ngangari, Rais Barre aligombea tena Urais mwaka 1986, Mwezi desemba na kushinda ikimaakisha kwamba alipata muhula mwingine wa miaka saba wa kuendelea kuwa Rais wa somalia.

Lakini minong'ono haikuisha. Watu walitaka mrithi apatikane. Walitaka sura mpya kwenye uongozi wa nchi.

Na katika minong'ono hii kuliibuka majina mawili ambayo yalikuwa yanatajwa tajwa sana. Jina la kwanza lilikuwa la Jenerali Mohamed Ali Samatar, makamu wake wa Rais. Jina la pili lilikuwa la waziri wa Mambo ya Ndani Jenerali Ahmed Suleiman Abdille ambaye alikuwa ni mkwewe Rais Barre aliyemuoa moja ya binti yake.

Lakini kama ilivyo kwa madikteata wote duniani, kunapotokea tishio la madaraka yao kupokwa ni kana kwamba wanapata wehu. Rais Barre alianza kuwa dikteta katili akiwafunga na kuua wapinzani wake na wote ambao walikuwa wanaonekana kuwa na mwelekeo wa kumpinga.

Rais Barre woga wa madaraka kumponyoka ulioanda kwenye akili yake. Aliacha mpaka kusikiliza ushauri wa baraza lake la Mawaziri na badala yake aliongoza nchi kwa kuhusisha watu wachache sana ambao alikuwa anawaamini.

Kama ilivyo ada, watawala wakizidisha ukatili ndivyo navyo moto wa upinzani dhidi yao unavyozidi kukolea. Kwa hiyo Rais Barre sasa alikuwa anapingwa wazi wazi, ndani na nje ya Somalia.

Lakini kama tujuavyo kwamba nchi ya Somalia ina mgawanyiko mkubwa sana wa koo. Kwamba kuna uadui wa miaka mingi sana baina ya koo tofauti nchini humo. Rais Barre alianza kutumia mwanya huu wa uadui wa koo ili kuwaweka baadhi ya koo upande wake na wengine akiwapambanua kama koo adui kwa Taifa la Somalia.

Tunafahamu kwamba katika kipindi hiki 'Derg' ilikuwa na ushawishi mkubwa sana katika nchi zilizoko kwenye pembe ya Afrika. Derg ni kamati ya uongozi wa kijeshi ambao walisimamia kuondolewa madarakani kwa Mfalme Haile Selassie. Wao ndio waliokomesha utawala wa Kifalme nchini Ethiopia.

Japokuwa Rais Barre alikuwa anafanya uovu nchini kwake Somalia, lakini Mengistu Haile Mariam, kiongozi wa Derg huko Ethiopia alichukizwa mno. Ndipo hapa akaanza kuunga mkono vikundi vya wapiganaji wa kisomali ambao walikuwa wanataka Rais Barre aondoke madarakani.

Rais Barre hakuwa na simile… alitumua jeshi na silaha nzito kupambana na adui zake. Kufumba na kufumbua maeneo ya kaskazini mwa Somalia ambao ndiko hasa upinzani dhidi yake ulikuwa mkubwa, kuligeuka uwanja wa vita.

View attachment 729973

View attachment 729974

Hali hii ya nchi kuingia kwenye machafuko iliwahuzunisha sana watu wengi wazalendo na wenye ushawishi ndani ya Somalia akiwemo Rais wa kwanza wa nchi hiyo Aden Abdullah Osman Daar. Osman Daar aliongoza wanasiasa wengine wapatao mia moja wenye ushawishi mkubwa nchini humo kusaini waraka maalumu wenye kumtaka Rais Barre afanye suluhu na vikundi vya wapiganaji.

Kama wasemavyo kwamba sikio la kufa halisikii dawa. Rais Barre hakutaka kusikiliza rai hii ya wanasiasa wenzake wakongwe. Aliendeleza ukatili dhidi ya wote ambao walikuwa wanampinga na mapambano dhidi ya vikundi vya wapiganaji yalipamba moto.


Mapambano haya kati ya majeshi ya serikali na vikundi vya waasi yalidumu kwa miaka kadhaa.

Kadiri muda ulivyokuwa unaendelea ndivyo ambavyo majeshi ya Rais Barre yalikuwa yanazidiwa nguvu.
Mpaka kufikia katikati ya mwaka 1990 majeshi ya serikali yalikuwa yamezidiwa nguvu kwa kiasi kikubwa sana. Waasi walikuwa wametwaa sehemu kubwa ya vijiji na mitaa inayozunguka mji mkuu wa Mogadishu. Ndipo hapa ambapo watu walimbatiza jina la utani Rais Barre kwamba ni 'Meya wa Mogadishu', wakimanisha kwamba ni eneo la Mogadishu ndilo pekee ambalo Barre alikuwa na mamlaka nalo na maamuzi kutokana na vikundi vya waasi kutawala maeneo mengine yote ya nchi na Raias alikuwa hawezi hata kutoka nje ya mji huo.

Mwezi desemmba mwaka huo 1990 waasi wa USC (United Somali Congress) waliingia ndani ya mji wa Mogadishu wakiingozwa na Jenerali Mohamed Farah Aidid. Baada ya kuingia zilifuata wiki nne za mapigano makali kati ya USC na jeshi la rais Barre.
Mpaka kufikia mwezi January, wapiganaji wa USC walikuwa wamefanikiwa kuyashinda majeshi ya Rais Barre na hatimaye kumuondoa Barre mwenyewe madarakani.

Shida nyingine ikaibuka…

Nilieleza hapo nyuma kidogo kwamba Somalia wana mgawanyiko mkubwa na uadui wa koo. Kwa hiyo hata baada ya vikosi vya USC kumshinda Rais Barre na kumuondoa madarakani, koo nyingine zilikataa kumtambua Jenerali Farah Aidid kama kiongozi mpya wa Somalia. Matokeo yake vikundi hivi vya waasi vikaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe. Kila kikundi kikipigania kutawala eneo fulani.

Kwa mfano, kikundi kingine cha waasi wa SNM walijiamulia kutangaza moja ya eneo la nchi ya Somalia kama nchi huru na kuibatiza jina jipya la Somaliland na kiongozi wao Abdirahman Ahmed Ali Tuur kuwa Rais wa nchi hiyo mpya. Mgogoro huu bado ungalipo mpaka leo hii wananchi wa eneo hilo wakitaka kutambulika eneo lao kama nchi huru.

Hata kikundi cha USC chenyewe nacho kiligawanyika baada ya makamanda wake wakuu Farah Aidid na Ali Mahdi Mohamed kutofautiana wakigombea madaraka na utawala wa mji wa Mogadishu.

Wapiganaji wa USC waliokuwa wanamuunga mkono Aidid na upande mwingine ambao walikuwa wanamuunga mkono Mahdi walianza kupigana wenyewe kwa wenyewe kugombea kutawala mji mkuu wa mogadishu.

Baada ya miezi kadhaa ya mapigano makali, mwaka 1992 ilibidi Aidid na Mahdi wakubaliane kuugawanya mji wa Mogadishu katika pande mbili… kusinu na kaskazini. Ukawekwa mpaka katikati ambao hakuna upande ulikuwa unaruhusiwa kuvuka.

Nchi ya Somalia ilikuwa imefikia kuwa kiroja cha namna hiyo. Ikiwa imegawanyika vipande vipande. Kila ukoo ukitawala eneo fulani. Kwa maneno mengine nchi haikuwa na serikali wala jeshi la pamoja bali kila ukoo ulkkuwa na lwake.


Ndipo hapa ambapo mwaka 1992 Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa walipitisha resolution namba 733 kuunda UNOSOM I (United Nations Operation in Somali I) kwa lengo la kusaidia kupeleka misaada ya kiutu nchini Somalia.

Mwezi desemba tarehe 3 mwaka huo 1992 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walipitisha resolution nyingine namba 794 kuunda kikosi maalumu cha UNITAF (United Task Force) kwa ajili ya kulinda watoa huduma za kiutu na kulinda amani nchini Somalia.

Mwezi January mwaka 1993 vikosi hivi vya umoja wa mataifa kwa ajili ya kazi hii maalumu. Hakuna ambaye alikuwa na hofu au shaka juu ya utekelezaji wa oparesheni hii. Ilikuwa inategemewa kwenda sawia na murua kabisa na amani kurejea nchini Somalia.

Jambo moja la msingi ambalo hawakuliangalia au hawakuling'amua mwanzoni ni kwamba… hakuna weledi au ushujaa unaotosha kupambana na wananchi wenye hasira au imani. Na kama waswahili wasemavyo, "usiingile ugovi wa ndugu… wakipatana watakurarua wewe". Ndicho kinachofanana kabisa na aambacho kilikuwa kinaelekea kutokea nchini Somalia.

Ni kweli nchi ilikuwa imemegeka vipande vipande… na vita vilipiganwa hovyo baina ya ukoo na ukoo kugombea utawala wa maeneo. Lakini kitendo cha Umoja wa Mataifa kuingiza majeshi nchinu Somalia ilikuwa ni kana kwamba kuwapa koo hizo adui mmoja wa wote kupigana nae.

Lilikuwa ni suala la muda tu kabla ya vikosi vya Umoja wa Mataifa vikiongozwa na Marekani kugundua kosa kubwa ambalo walikuwa wamelifanya. Kosa ambalo lilikuja kupelekea kufanyika kwa moja oparesheni ya za kijeshi hatari zaidi kwenye historia… Operation Gothic Serpent. Operation ambayo imeacha vidonda kwa pande zote mbili… Marekani na Somalia. Na kuchangia Somalia kutotengamaa mpaka leo hii.


Tuwe pamoja kuichambua mpaka mwisho.



Habibu B. Anga 'The bold' - 0718 096 811
To Infinity and Beyond

Muhimu: Ndani ya wiki moja ijayo nitatoa kitabu changu cha kwanza kabisa. Nitawataarifu hapa ni namna gani ambavyo utaweza kukipata. Kama ambavyo mmekuwa mkiniunga mkono hapa jukwaani, naomba muendelee kuniunga mkono pia kwenye hatua hii mpya niliyochukua.
tatizo nondo hzi hazfiki mwsho
 
Back
Top Bottom