Chuo Kikuu "Huria" cha Tanzania leo kimetangaza kurejeshwa kwa Foundation Program ambayo awali ilisimamishwa na serikali. Kwa hiyo njia nyingine ya kwenda vyuo vikuu imefunguliwa tena ingawapo dhana ya uhuria wa chuo kikuu hiki imepungua. Nasema imepungua kwani sasa vigezo vya udahili ni
1. Form 6 mwenye point 1.5 kwenye masomo mawili
2. Mwenye Diploma ya GPA 2 hadi 2.9
3. Mwenye Cheti cha NTA level 5/Professional Level II Certificate.
Hivyo mwenye certificate baada ya o-levels inabidi apate Diploma au NTA level 5 sio kama zamani ambapo certificate ilitosha.
Program ni mwaka 1 Gharama ni Tshs 630,000. Wahitimu wa program hii wanaruhusiwa kujiunga na chuo chochote nchini.
Kazi kwenu.