Open Source softwate in advertisment marketplace

.........................................................................
Naamini nimejibu suala/swali lako.
Umetoa lekcha poa sana.

Naendelea na nategema kujifunza mengi zaidi kutoka kwako kwenye ulimwengu wa graphics na animation design. Huwa najaribu jaribu kufuata training za Lynda.com nilzopakua. Kama una link ya resource nyingine nzuri za Adobe Premire na after affects nidondoshee hapa

Kwa sababu ni begiiner na sababu ya muda sitaki kujaribu jaribu application tofauti nataka niwe "begginer" mkali wa Adobe lol
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
3D this is Impressive!!!! Is the second paragraph of the edited qoute for real?? Really.... Yaani smell of rubber?

Mi nadhani tunapoongelea 1D,2D, 3D na 4D tunaongela sense organ za eyes zinavyotasfiri na kuona kitu au vitu So kusema smell(Pua) or touch ( ngozi) sidhani kama inaweza kuwa explained kama concept ya 4D hata kama inakuwa introduced kwenye CINEMA.
 
Umetoa lekcha poa sana.

Naendelea na nategema kujifunza mengi zaidi kutoka kwako kwenye ulimwengu wa graphics na animation design. Huwa najaribu jaribu kufuata training za Lynda.com nilzopakua. Kama una link ya resource nyingine nzuri za Adobe Premire na after affects nidondoshee hapa

Kwa sababu ni begiiner na sababu ya muda sitaki kujaribu jaribu application tofauti nataka niwe "begginer" mkali wa Adobe lol

Adobe Premiere sana nimejifunza kwa trial and error hivyo sijafuatilia mitandao inayotoa tutorials zake. Hata hivyo naamini yYouTube kutakuwa na tutorials nyingi... ukifahamu Premiere utajikuta ni rahisi kujua Sony Vegas na hata Final Cut kwa kuwa working principles zao zinafanana sana. Sana.

AfterEffects tutorials unaweza kuzipata hapa VIDEO COPILOT | After Effects Tutorials, Plug-ins and Stock Footage for Post Production Professionals hapa ndiyo mwisho wa reli. Ila katika mtandao huuhuu anzia hapa After Effects Basic Training kuna tutorials 10 za basic training ya AfterEffects. Mtandao mwingine ni kama motionworks.com.au, creativecow.net .... kutoka katika mitandao hii utapata links zingine. YouTube.com na Vimeo.com pia ni poa but you must type AfterEffects or Premiere or so..
 
Mi nadhani tunapoongelea 1D,2D, 3D na 4D tunaongela sense organ za eyes zinavyotasfiri na kuona kitu au vitu So kusema smell(Pua) or touch ( ngozi) sidhani kama inaweza kuwa explained kama concept ya 4D hata kama inakuwa introduced kwenye CINEMA.



I have never observed this from this angle.... THANK YOU.

Ipo so very clear sasa... na makes 4D ieleweke zaidi ya pale 3D alielezea.
 
4D film - Wikipedia, the free encyclopedia

Me nah say more.. see for yourself. Your first avatar here at JF was of AVATAR, ever watched AVATAR in 4D or it was simply over a scratchy DVD?



hahahah.... Sasa hayo madongo 3D.... Of coz you know I didn't even know 4D existed if it was'nt because of this thread. I Love the movie "Avatar" watched it first in a scratchy CD as per your words...lol... But was fortunate to see it kwa 3D.... It was as if I was watching the movie for the first time.... Astounding!
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Mi nadhani tunapoongelea 1D,2D, 3D na 4D tunaongela sense organ za eyes zinavyotasfiri na kuona kitu au vitu So kusema smell(Pua) or touch ( ngozi) sidhani kama inaweza kuwa explained kama concept ya 4D hata kama inakuwa introduced kwenye CINEMA.

Kwa kweli "dimension" hutegemeana na context ya mazungumzo. Kwa habari ya macho kuona kwa kawaida huwa yanaona 3D. Mfano, meza ikiwa mbele yako utaona upana na urefu wake (Upana + Urefu = 2 Dimension) pamoja na surface yake ya juu ambayo italupa picha ya depth (3rd dimension), hivyo three dimension means Length, Width and Depth. Kama meza itakuwa ndefu kiwango cha level ya macho yako na ikawa mbele yako (si pembeni) then utaona upana na kimo chake tu (2 Dimension). Sijasikia kuhusu 1 Dimension. Hivyo kimsingi macho hayaoni 4th dimension. Katika sinema 4th Dimension haihusiani na dimension ya kuona..ni kielelezo tu cha kwamba "zaidi ya sinema ya 3D tutakayokuonesha tutakupa na hisia kabisa (4th dimension)."

Muktadha (context) mwingine wa Fourth Dimension soma Fourth dimension - Wikipedia, the free encyclopedia
 
hahahah.... Sasa hayo madongo 3D.... Of coz you know I didn't even know 4D existed if it was'nt because of this thread. I Love the movie "Avatar" watched it first in a scratchy CD as per your words...lol... But was fortunate to see it kwa 3D.... It was as if I was watching the movie for the first time.... Astounding!

You were lucky to watch it in 3D. Kama kuna mtu (aisee Mtazamaji nakusema wewe bana) hajaona sinema katika 3D afanye hivyo haraka. Haielezeki hadi ujionee mwenyewe. Adventures of Tintin (in 3D) inaoneshwa Mlimani City wiki hii na ijayo (Nimesoma post ya Vusile kwenye jukwaa la Entertainment). Napanga kuitazama next thursday. Niliiona tu trailer yake kwenye YouTube...my my my...

.................................

Watched Adventures of Tintin: Secret of the Unicorn (In 3D stereo) today ...... extraordinary!!!!!
 
You were lucky to watch it in 3D. Kama kuna mtu (aisee Mtazamaji nakusema wewe bana) hajaona sinema katika 3D afanye hivyo haraka. Haielezeki hadi ujionee mwenyewe. Adventures of Tintin (in 3D) inaoneshwa Mlimani City wiki hii na ijayo (Nimesoma post ya Vusile kwenye jukwaa la Entertainment). Napanga kuitazama next thursday. Niliiona tu trailer yake kwenye YouTube...my my my...



Hii post imelenga kuchomana mioyo.... Ngoja tu nisepe!
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Kotin vouches for Blender 3D...
Why I say this, since blender 3d is a free software, you will have access to a full featured application without the constraints of costs or a crippled application.
3D terms and techniques are almost similar and very tiny differences do actually exist, more like very specific wording of similar actions, hence once you learn one application, it will be easy to turn to a different one with little hassle.
As 3D stated, you will need to start small, and build up the ambitions as you gain more experience in the 3d world.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Hii post imelenga kuchomana mioyo.... Ngoja tu nisepe!

Pole! Lakini sikukusudia kumuumiza mtu, lols!! Nina hamu ya kuiona kwa kuwa mimi ni shabiki Mkubwa wa Peter Jackson ambapo katika filamu hii ni producer, director akiwa Steven Spielberg. BTW, of all the movies I have ever watched I consider Peter Jackson's The Lord of the Rings trilogy the best movies ever made. I miss Frodo, Gollum, Gandalf, Saruman, Bilbo, Aragon, The Two Towers... just my mind... just my mind... here comes "Aye Captain... this is Captain Jack Sparrow... the best Pirate....." Captain Hector Barbossa. Beware, what I've just said here isn't related to Kotinkarwak's thread.. I was just speaking my mind... You wouldn't forget George Lucas' Star Wars - The phantom menace.... Aisee watu wanatengeneza sinema. Peter Jackson anaandaa "The Hobbit" then ata-direct sequel ya Tintin... niishie hapa maana naona mzuka unazidi kupanda tu. Peter Jackson ni namba nyingine.. acha kabisa.. nilitaka kumsahau James Cameron.. Titanic - "It's been 84 years, and I can still smell the fresh paint. The china had never been used. The sheets had never been slept in. Titanic was called the Ship of Dreams, and it was. It really was."

"No, mate. Titanic go to America. In five minutes."
I gotta go guys.
 
You were lucky to watch it in 3D. Kama kuna mtu (aisee Mtazamaji nakusema wewe bana) hajaona sinema katika 3D afanye hivyo haraka. Haielezeki hadi ujionee mwenyewe. Adventures of Tintin (in 3D) inaoneshwa Mlimani City wiki hii na ijayo (Nimesoma post ya Vusile kwenye jukwaa la Entertainment). Napanga kuitazama next thursday. Niliiona tu trailer yake kwenye YouTube...my my my...


3D

Kwa nin kuona movie ya 3D inabidi watu wavae miwani? Je Ina maana macho yetu binaamu uwezo wake unaishia kwnye 2D mpaka tuhitaji msaada artificial.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
3D

Kwa nin kuona movie ya 3D inabidi watu wavae miwani? Je Ina maana macho yetu binaamu uwezo wake unaishia kwnye 2D mpaka tuhitaji msaada artificial.

Hii teknologia ya zamani kidogo, nadhani ilipata umaarufu miaka ile ya 1950, japokuwa hii technologi ilianza karne ya 18. kwa sasa ndio inaonekana kuchukuwa kasi kidogo, japokuwa wataalam wanahisi kama haikupokelewa vyema na watumiaji kwa sababu watu wengi wanalalamika kuwa inawasababishia matatizo ya macho (ukavu wa macho), maumivu ya macho, kichwa na hata kizunguzungu.


Kuna aina nyingi kidogo za miwani inayotumiwa kama vile Anaglyph, Polarized 3D glasses, Eclipse method n.k macho ya binadamu hayawezi kuona mambo mengi sana, na ndio maana yanadanganyika hata na simple illusion.


3D Stereoscopy inatengenezwa na taswira mbili zinazo kinzana kushoto na kulia (offset images separately to the left and right eye of the viewer). Hizi taswira kwa macho ya kawaida haziwezi kuwekwa sawa mpaka upate visaidizi kama vile hizi miwani za 3D. Hizi miwani ni ghali kidogo kama utanunua 3D TV bila miwani yake, zinafikia mpaka $300 kwa pair moja. Kwa sasa kuna 3DTV ambazo zinakuja na miwani ya bei rahisi kama zile zinazotumika kwenye majumba ya sinema.


Sasa hivi kuna 3DTV without glass (Autostereoscopy) ambazo utumii miwani tena ila hata hizi bado watu wanazilalamikia pale object zikiwa zinakwenda kwa haraka sana, utaalam bado unatafuta suluhisho ili watumiaji waweze kufurahia hii kitu ya 3D.


Kwa ujumla 3D TV ni ghali kidogo, wakati mwingine si kidogo inategemea na brand na uwezo wa mtu, kwa sasa mimi binafsi sishauri mtu kununua hii kitu zaidi ya kwenda sinema na kungalia kule, lakini kwa kununua 3DTV na kuweka nyumbani bado sana, inatakiwa at least hii kitu ifikishe miaka kama 10 hivi ili wawe wameweza kurekebisha kasoro ndogo ndogo zote na mtu anapoangalia asipate matatizo ya macho, kichwa kuuma au kizunguzungu.


3DTV bila miwani zimeanza kuuzwa ila nazo bei ni ghali sana. Toshiba Japan wame launch mwaka 2010, na bei yake ilikuwa ¥120,000 sawa na $1,450 na hii ni kwa TV ya inch 12, ukitaka 20-inch iliuzwa ¥240,000 sawa na $2,920. Sasa piga mahesabu kwa pesa ya bongo.


Unaweza kuangalia kurasa za wikipedia kuhusiana na hii teknolojia.
 
Upo mkuu..
Tumekumisi Jukwaa la Dini/Imani mpaka wengine wanasema umeingia mitini :)
Nipo mkuu, ni majukumu tu, hao wanaodai kuwa nimeingia mitini, utoto unawasumbua, wakikua wataacha.

Ukiwa na jambo lolote just nitumie PM.
 
Mtazamaji mimi najua nafahamu sana Adobe Premiere, naweza kukusaidia. Nilijaribu kujifunza After effect lakini sikwenda mbali sababu ya majukumu lakini bado nina ambition.
Hata hivyo 3D imenivutia sana na kunifanya nijiulize kwa nini nisijifunze? Ngoja nijitayarishe.
Asante sana 3D. Nimependa sana hizi animations zako kwa kweli. Niseme nimepata wivu sana ( sio mbaya hapana) teh teh teh teeeee

 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Kwa kweli "dimension" hutegemeana na context ya mazungumzo. Kwa habari ya macho kuona kwa kawaida huwa yanaona 3D....
Mkuu, kwanini msianze kujifunza vitu rahisi kama cartoon za 2D mfano wa The Simpson au Tom n Jerry Cartoon? Japokuwa hapo chini nimeweka hizo Cartoon, na zimetengenezwa na makampuni makubwa, lakini waanzilishi wake walikuwa na mawazo kama yenu, na baada ya jitihada nyingi kazi zao zimekuwa maarufu sana... Nahisi hata program zake si ngumu sana kiivyo.


Ethiopian Moment On The Simpson's



Tom n Jerry Cartoon



2D cartoon animation film for kids by BMG Animations

 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: 3D.
3D

Kwa nin kuona movie ya 3D inabidi watu wavae miwani? Je Ina maana macho yetu binaamu uwezo wake unaishia kwnye 2D mpaka tuhitaji msaada artificial.

MACHO YA BINADAMU YANAVYOONA
Macho ya binadamu yanaona 3D. Hebu tazama mouse ya kompyuta yako au kitu chochote kilicho mbele yako. Fumba jicho la kulia na kitazame hicho kitu kwa jicho la kushoto bila kuyumbisha shingo. Then kitazame kwa jicho la kulia na fumba la kushoto. Rudia kitendo hiki haraka-haraka...kushoto-kulia kushoto-kulia kushoto-kulia ..haraka haraka bila kugeuza shingo. Utagundua kuwa ukikitazama kwa jicho la kulia kina-appear kuwa kulia zaidi na ukikitazama kwa jicho la kushoto kinaonekana kuwa kushoto zaidi..ni kama vile kinahama-hama position. Ukikitazama kwa macho yote kina-appear kuwa katika position ambayo ni average ya jicho la kulia na kushoto. Hii inamaana kuwa kila jicho hupeleka picha tofauti kidogo katika ubongo na ubongo hufanya kazi ya kutafsiri average position kwa kutumia taarifa ya positions mbili zinazoletwa na macho mawili.

Chukua simu yako halafu igeuze uitazame upande wake mwembamba (namaanisha usiitazame upande wake wa mbele wala wa nyuma badala yake tazama upande wa thickness). Ukitazama kwa jicho la kulia pekee utaweza kuona upande wa thickness wote na upande wa mbele kidogo (kama mbele ulipageuzia kulia). Ukitazama kwa jicho la kushoto utauona upande wa thickness wote na upande wa nyuma kidogo (kama nyuma ulipageuzia kushoto). Hii inamaanisha ukitazama kwa macho yote mawili utaona upande wa nyuma kidogo, upande wa thickness wote na upande wa mbele kidogo... hapa ubongo umefanya tena kazi ya kutafuta average.

Hivyo ubongo husaidia kuunda taswira yenye perspective pana zaidi ambayo kimsingi ndiyo 3D yenyewe.
Kwa msaada wa views mbalimbali za macho kama nilivyoeleza hapo juu na kwa msaada wa vitu mbalimbali ambavyo huwa vimeambatana na mazingira kama watu, miti, mawe, magari nk ambavyo huwa katika sizes, positions, movements na distances tofauti tofauti tunaweza kuona dunia kwa namna ya kawaida kama unavyoona wewe sasa..yaani 3D. Kilicho mbali unakiona hivyo, kilicho karibu unakiona hivyo. Kilicho nyuma ya kingine unakiona hivyo na unapata picha kiko kwa nyuma kwa umbali gani.

KAMERA YA KAWAIDA NA KAMERA AMBAYO NI STEREOSCOPIC
Kamera ya kawaida iwe ya video au still picture huwa na apecha (tundu la lenzi) moja tu. Kamera za 3D stereoscopy huwa na apecha mbili kama inavyoonekana ktika picha hapa chini:

em3d.jpg panasonic-pro-3d-camera-xl.jpg

Kamera hizi hurekodi images za positions mbili tofauti kama macho yanavyofanya. Hebu tazama hapa chini mfano wa picha ile ile kama ilivyoonwa na matundu mawili tofauti ya kamera moja:

3D-PHOTO.jpg

Unagundua tofauti yoyote katika hizo picha mbili? Angalia picha ya kulia, miti iliyo mkono wa kushoto wa msichana mkubwa inaonekana kumgusa zaidi kuliko inavyoonekana katika picha ya kushoto. Pia katika picha ya kulia kuna kidude fulani cheusi hewani juu ya kichwa cha msichana mdogo, katika picha ya kushoto kidude hicho kiko zaidi kwa msichana mkubwa nk nk. Hivyo ndivyo camera ya apecha mbili hurekodi (kama ambavyo macho mawili yaonavyo).

Sasa hebu sasa tupate average ya ubongo ya picha hiyo ya wasichana hapo juu hapa ndipo utapoona 3D image (Hata hivyo inahitaji ku-concentrate kidogo akili na kupractice kwa sababu ubongo unakuwa haujatarajia kuona utachokiona):

Ukitazama kawaida hiyo picha utaona ni picha mbili kama unavyoona sasa. Anza kufanya makengeza kidogo kidogo huku ukizidisha makengeza kidogo kidogo...utaanza kuona picha tatu..mbili pembeni na moja imeongezeka katikati... usizidishe makengeza maana utaanza kuona nne...nataka uone tatu tu. Ukiweza kuona tatu sasa concentrate kwa ile ya katikati... move kichwa chako pole pole mbele na nyuma huku ukiendelea ku-concentrate akili yako katika picha ya katikati... itafikia hatua hiyo picha ya katikati itakuwa very clear na hapo utaona fimbo aliyoishika huyo mdada imesogea mbele na mazingira kama miti na nyumba waliyoipa mgongo iko nyuma sana. Hivyo ndivyo 3D inavyoonekana kwa kuvaa miwani.

SINEMA NA UVAAJI MIWANI.
Kama X-Paster alivyoeleza hapo juu teknolojia ya 3D ni pana na kuna miwani tofauti-tofauti tegemeana na teknolojia husika... kwa kawaida ukitazama sinema iliyokuwa enabled katika 3D usipotumia miwani utaona video iko kama gazeti lililochapishwa vibaya, kama picha ifuatayo inavyoonesha:

CYAN.jpg

Picha hii imekuwa distorted kidogo kwenye colour channels (kama unavyoiona picha....sitazungumzia kiundani). Sasa huwezi kuona 3D ya picha hii kwa kufanya makengeza.. unahitaji miwani ambayo imekuwa designed kusoma hizo colour channels ("colour channels" ni lugha yangu mwenyewe.. nadhani kuna jina sahihi zaidi) na kuupa ubongo illusion ya 3D. Hii ndiyo sababu ya kuvaa miwani katika sinema za 3D.

Sasa kwanini wasitengeneze TV itayoji-convert yenyewe ili kuondoa ulazima wa miwani kwa kuweka kioo chenye teknolojia ya miwani katika TV yenyewe? .... wameshatengeneza kama alivyosema X-Paster.

Nadhani nimejibu sehemu kubwa ya ulichouliza. Naomba tu nisisitize kuwa teknolojia hii ni pana sana kama alivyosema X-Paster hivyo maelezo niliyotoa ni sahihi (basing on my knowledge only). Tarajia kusikia mambo mengine tofauti-tofauti tegemeana na teknolojia husika.

All the best.
 

Attachments

  • 2289885289_d5649fd221_o.jpg
    2289885289_d5649fd221_o.jpg
    160.9 KB · Views: 56
  • 3Dhand2.bmp
    960.1 KB · Views: 16
Back
Top Bottom