Ooow! Too bad! Hii mpaka lini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ooow! Too bad! Hii mpaka lini!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Horseshoe Arch, Mar 17, 2011.

 1. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Bandugu! Kaka yangu mmoja askari polisi aliuawa Juzi Shinyanga baada ya wahalifu aliokua anawalinda kumhadaa kana kwamba wanaomba kusikilizwa kidogo na alipowasikiliza ghafla wakamzidi nguvu kabla ya kumpora bunduki aliyokua nayo na kumshindilia risasi na alipokuja askari mwenzake kusaidia naye akauawa na kuporwa bastola...hata hivyo wananchi walifanikiwa kumuua jambazi mmoja wao na mwingine kutoroka! Leo nipo Kilwa road kutoa heshima za mwisho! R.I.P bro! Damu yako haikumwagika bure!
   
 2. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mhh!Pole sana.Tumuombee alale pema peponi.Wote twaenda njia moja.Mungu alimpenda zaidi.
  Pole tena Mkuu
   
 3. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Horseshoe Arch ,

  Pole sana Mkuu kwa msiba wa Kaka yako.

  Nadhani ndo ule uliotokea Kituo Cha Polisi pale Kagongwa, Kahama na Polisi wawili kuuwawa Kinyama!

  Kituo kile nakifahamu vizuri sana kwani kipo mita chache toka barabara kuu ya lami, mkono wa kushoto kama unatoka Isaka kwenda Kahama.

  Mungu azilaze Roho za Marehemu hao mahali pema peponi. Amina
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hii habari niliisikia leo asubuhi, imenisikitisha sana.
  Mbaya zaidi jambazi moja ni raia wa Burundi.
  Poleni sana wafiwa na Watanzania kwa ujumla kwa kupoteza askari.
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Duh hii mbaya sana
  RIP
   
 6. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Too bad too bad Salim ndio kwanza alihitaji miezi 6 kutimu miaka 30...alipanga mengi ikiwa ni pamoja na kufunga ndoa mwaka huu ila Mungu naye alikua na yake ambayo hatuna budi kuyakubali! Nimekubali kila nafsi hai ni sharti ionje mauti!
   
 7. c

  chetuntu R I P

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole mkuu tuko pamoja, hakika damu yake haikumwagika bure. SALIM "KATWE" umetangulia sote tupo nyuma yako. PUMZIKA KWA AMANI, TULIKUPENDA SANA NA TUTAENDELEA KUKUPENDA DAIMA. SALIM hukudeserve kifo cha kikatili namna hii. MUNGU AKUREHEMU UPUMZIKE KWA AMANI. Imeandikwa tumshukuru MUNGU kwa kila jambo.
   
 8. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Nimesikiliza redio muda fulani asubuhi na kujikuta nagadhibika ila sikufahamu ghadhabu yangu ii juu ya nini hasa! maana watangazaji walikua wanazungumza kwamba askari hao waliuawa kizembe...kweli nimeumia kidogo hasa ukizingatia trick waliyomwekea hawa mabwana! Well,Salimu alikua mtu makini na mtafiti kwa kile alichoamini...hakubweteka wakati akiwa dereva wa mkurugenzi wa makosa ya jinai na kuonesha uhakiki wa hilo aliamua kuchukua mafunzo ya awali idara ya upelelezi kwenye kitengo cha madawa ya kulevya!
  Hakuishia hapo kwani alionesha ukomavu kabla hajahamishiwa kitengo maalumu cha kupambana na ujambazi kazi aliyoifanya hadi mauti yanamkuta saa 12 jioni tarehe 15/03/2011 katika kituo cha polisi Kabongwa! R.I.P bro! Safari yako imeisha kiume!
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu, ni mapenzi ya Mungu!
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Poleni sana wafiwa!
   
 11. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Yeah mkuu Genekai...tutahakikisha hawa wanaharamu hawabaki mtaani huru...maana si wema wao ulifafikisha pale! Kikombe alichokinywea Salimu hakitawapita! Mungu awalipie kwa kua ahera ya waovu ii duniani!
   
 12. c

  chetuntu R I P

  #12
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inakera sana watu wapoanza kusema askari walikuwa wazembe hata hapa jamvini kuna watu wamecomment the same, majambazi wa hii kanda ( Kigoma, Tabora, Mwanza, Shinyanga) sio wale waliozoeleka Dar na kwingineko hawa ni ma ex soldiers wa Burundi ni wakaidi sana na wana roho za ajabu kabisa na wana mbinu za kivita. Huku unakuta majambazi wana RPG na mabomu ya kutupa. SALIM tutakullilia daima.
   
 13. c

  chetuntu R I P

  #13
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sa nyingine inakuwa ngumu sana kusema mapenzi ya Mungu, me naona ni shetani tuu.
   
 14. L

  Leornado JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nimesikitika sana, RIP wazalendo halisi.

  Lawama zote kwa serikali ya JK manake ndie alietufikisha hapa hadi watanzania kuwa wanyama kiasi hiki wakishirikiana na majangili kutoka nchi jirani.
   
 15. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Chetuntu heshima yako mkuu,nadhani kwa kutumia sense yangu ya sita kuna jambo nimeliona nyuma ya unaoitwa ujambazi...hii kitu ina watu nyuma! K ufikishwa mbele kwa wale watuhumiwa kungeharibia watu!...watalipa damu yake...shukrani kwa shupavu wanaoona uzembe!
   
 16. c

  chetuntu R I P

  #16
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima pia kwako mkuu, nimekuelewa na sasa naanza kupata mwanga halisi. Damu ya SALIM haitapotea bure.
   
Loading...