ONYO kwa wanaonunua simu humu

DullyJr

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
13,981
11,830
Kumekuwa na matangazo mengi sana yahusuyo mauzo ya simu na vitu vingine ila mimi nitaongelea zaidi kwenye simu.

Simu nyingi zinazouzwa humu ni vimeo utakuta mtu anajua kimeo kinaelekea kumfia anakitupia huku.

Juzi kuna JF member nusu nimpeleke polisi kama si huruma iliyonijia ghafla.

Wengi wanauza vimeo vilivyoshindikana au cm za kuungaunga kwa mafundi!

USHAURI: Tuache uvivu twende madukani, simu mpya na guarantee bei rahisi. Tupunguze tamaa za kupata vitu vizuri kwa bei za kutupa.
 
Embu toa habari ki Great thinker! Ni member gani na ilikuwaje? Utatusaidia na wengine.

PICHA LILIKUWA HIVI:
nimekuta tangazo la BB CURVE inauzwa kwa 100k,
kwa sifa zilizowekwa nikawa interested.
Nikamtafuta jamaa ili ninunue simu,
akanambia nimfate kwao TABATA,
kwakuwa mimi naishi SINZA nikamwambia tukutane UBUNGO TERMINAL ili kushare cost.....
Jamaa akafika eneo husika akiwa na bidhaa husika ikiwa ipo ON tayari!
Kama ilivyo kwa mtoto wa mjini mwingine sikutaka kuuziwa mbuzi kwenye kiroba nikaizima na kuiwasha simu,
yan process ya kuwasha tu ilichukua dk10 na charge ikawa imeisha hapohapo hivyo simu ikazima zzzzzz....!
(Kimoyomoyo nikasema biashara hakuna hapa)
MUUZAJI:(kwa kujistukia)dah..!ndo kawaida ya BB ukiwasha inaload sana na sijaichaj toka juz

MNUNUZI: sasa kwanini hukuichaj full leo na unajua toka jana kama kuna biashara?kwnza vitu vyake viko wapi?(charger&earphone)

MUUZAJI: ah!nilijisahau kuichaj ila charger ilipotea mi huwa naazima ya samsung

MNUNUZI: dah!sasa hapo itabidi katika hiyo pesa nitakayokupa itakayokupa itabidi ipungue ninunue charger

MUUZAJI: sawa haina shida,

MNUNUZI: sasa wewe nenda kachaj full,alafu tukutane hapahapa badae sawa?
(tukakubaliana akaondoka,akajua kashaula tayari)
ilipofika badae

MUUZAJI: tayari iko poa hii hapa mkubwa

MNUNUZI: ok!nikaizima nikaweka line yangu na memory card,
simu ilipowashwa ikakata display
(jamaa akawa anaiweka kwa kufichaficha inaelekea ndo tatizo la hyo simu)

MUUZAJI: (baada ya kuhangaika sana bila mafanikio,huku akinichek kwa jicho la wizi)
dah!yan tatizo hili ndo kwanza linantokea leo,itakuwaje mkuu?

MNUNUZI: nakusikiliza wewe unasemaje?

MUUZAJI: mi naona biashara ishakuwa ngumu hapa.

MNUNUZI: kama umelitambua hilo vizuri,
kajipange upya ukiwa na simu nzuri,nzima nitafute()
 
Ungemtaja jina ili tumuogope kama ukoma kuuza simu si lazima iwe kimeo mtu anaweza kuwa na shida ya haraka ya hela

mwenyewe yupo humuhumu na jana kaweka tangazo jipya la simu,
hivyo nataka aje mwenyewe acomfirm kama hatocomment hapa ntamtaja kweupeee
 
Kumekuwa na matangazo mengi sana yahusuyo mauzo ya simu na vitu vingine,
ila mimi nitaongelea zaidi kwenye simu,
simu nyingi zinazouzwa humu ni vimeo utakuta mtu anajua kimeo kinaelekea kumfia anakitupia huku,
juzi kuna jfmember nusu nimpeleke polisi kama si huruma iliyonijia ghafla,

wengi wanauza vimeo vilivyoshindikana au cm za kuungaunga kwa mafundi!
USHAURI:Tuache uvivu twende madukani,simu mpya na guarantee bei rahisi,tupunguze tamaa za kupata vitu vizuri kwa bei za kutupa

rekebisha usemi kuna wauza simu humu wana maduka yao kama Godfrey Electronics sasa wewe unapotoa onyo sielewi
Hapa kila mtu kakomaa akili akiona simu akaipenda humu anawasiliana muuzaji anaiona face yake akiridhika ndo analipa

usitaku ku implant spirit mbaya kwa watu

pia hii ni sehemu ya biashara sana so ktk soko au market place mambo kama hayo hayakosi ni wewe tu kuangalia wapi kuna ukweli na uhakika

Hope nimeeleweka na sitaki tangazo hili likutwe na wageni sababu litachafua jukwaa kwa mambo ambayo yanaitaji umakini wa mnunuaji

Uwezi enda duka la vifaa used ukakurupuka kununua kitu
pia kama ujui hili soma sticky hapo juu kaweka robot inayotutahadharisha na haya yote

Lidumu jukwaa la matangazo
 
Last edited by a moderator:

mkuu weye ndio muuzaji nini..? hehehe ukiona manyoya ....!!!
 
Kiongozi Onyo tumelizingatia! Hata hivyo, wauzaji wengine ni waungwana katika biashara zao. Nimewahi kununua tablet na Mifi humu humu Jf na walinitumia huku mikoani bila ya matatizo na bidhaa zinadunda kama kawa!
 
Kumekuwa na matangazo mengi sana yahusuyo mauzo ya simu na vitu vingine,
ila mimi nitaongelea zaidi kwenye simu,
simu nyingi zinazouzwa humu ni vimeo utakuta mtu anajua kimeo kinaelekea kumfia anakitupia huku,
juzi kuna jfmember nusu nimpeleke polisi kama si huruma iliyonijia ghafla,

wengi wanauza vimeo vilivyoshindikana au cm za kuungaunga kwa mafundi!
USHAURI:Tuache uvivu twende madukani,simu mpya na guarantee bei rahisi,tupunguze tamaa za kupata vitu vizuri kwa bei za kutupa

wewe umekutana na mzinguaji mmoja unahukumu wauzaji wote......mimi nishauzia watu humu vitu vingi tu na wananipm kuappreciate.....sasa hivi nauza iPHONE 4S brand new....boxed na accessories zote njoo ni-pm ununue na uje utoe feedback hapa....hata sisi wauzaji kuna wanunuzi tunagongana na wayeyushaji wengi tu lakini ni sehemu ya biashara...
 
Inashangaza mtu akiwa anauza simu yake atakwambia ina miez miwili tu toka ninunue!
Hata kama itakuwa na miaka mitatu dah!

Sasa vibaka wamehamia kwenye mitandao baada ya dili ya kukaba kudhibitiwa na ulinzi shirikishi
 
Kuwasaidia wengine, mtaje. Sisi tutaangalia IDs zake zote na kuziunganisha.

Ikibidi, tupe # yake ya simu tutamwanika hadi majina halisi. Threads zake zote zitafutwa na ID itawekewa status ya TAPELI.

Thanks

Huyu hapa

Ni blackberry curve one ipo katika hali nzuri inauzwa kwa shilingi laki moja na hii ni kwa wakazi wa dsm kwa mawasiliano 0718071138 WAHANE

Thread yake hii hapa https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogo/440101-blackberry-inauzwa-sawa-na-bure.html#post6509330
 
PICHA LILIKUWA HIVI:
MUUZAJI: mi naona biashara ishakuwa ngumu hapa.

MNUNUZI: kama umelitambua hilo vizuri,
kajipange upya ukiwa na simu nzuri,nzima nitafute()

Sasa hapo kuna shida gani, ndivyo biashara inavyofanyika, tayari ulijua simu ni used toka mwanzo!
mmekubali kukubaliana, sioni tatizo hapo hakuna utapeli ni njia genuine za ufanyaji bashara!
 
Kuwasaidia wengine, mtaje. Sisi tutaangalia IDs zake zote na kuziunganisha.

Ikibidi, tupe # yake ya simu tutamwanika hadi majina halisi. Threads zake zote zitafutwa na ID itawekewa status ya TAPELI.

Thanks

Hapa busara zinahitajika mkuu! upande wa pili haujasikilizwa! hata hivyo hakulazimishwa kununua, alikuwa na uwanja huru wa kufanya majadiliano bila kushurutishwa kwa namna yoyote ile! majadiliano ndivyo biashara zinavyofanyika na wamejadiliana vya kutosha!!
 
Nimesha weka bandika hapo juu #17 anaweza kuja kuleta ushuhuda wa upande wa pili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom