Saidia polisi usinunue tairi mpya nje ya duka au mitaani

East African Eagle

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
3,759
2,205
Kuna utapeli wa kupaka matairi ya zamani mabovu rangi na kuyafunga na makaratasi yaonekane kama mapya kabisa na kisha kuyauza kwa bei poa kwa wateja wapenda vitu rahisi mitaani baada ya kuwalaghai kuwa wanauza matairi mapya kwa bei poa kuliko dukani.Ukiyanunua waweza dhani mapya ukienda kufunga ndio utaambiwa na mafundi ulizonunua sio tairi ni takataka na haziwezi hata faa kwa lolote ukiwatafuta hao matapeli wanakuwa wameshatokomea kusikojulikana na simu zao huwezi wapata.

Huu mtandao unakua kwa kasi na unaliza hadi wageni na unaharibu biashara halali ya matairi

Mnaowajua wahuni hao au mliowahi kulizwa saidieni polisi kwa kuwataja hata humu jamii forums na mahali walipo ili jeshi lichukue hatua stahiki

Ushauri wangu ni vizuri mtu ununue tairi mpya dukani na si nje ya maduka au mitaani.Dukani utapewa guarantee na utaondoka na amani kuwa ulichonunua ni kipya na si vinginevyo.Pia wale mnaotuma watu wawanunulie matairi ni vizuri mwende madukani wenyewe msije kuletewa msichokijua kikafungwa kwenye gari.
 
Back
Top Bottom