Juzi usiku nikiwa mataa ya kuelekea Kkoo (barabara ya Morogoro), kuna boda boda alikuwa amempakiza abiria (mtu mzima hivi, kaulamba mchomeko na kitambi hivi) na hakuwa amevaa helmet.
Sasa, ile kusimama kwenye mataa tu polisi wakafika na kuwadaka.
Dah! Yule bwana abiria akaruka kutoka kwenye boda boda akampangua polisi akatimua mbio, kidogo agongwe na mwendokasi. Ikabidi jamaa wasimame wampishe ... Watu wote vicheko! Akatokomea huko.
Polisi wakabaki na boda boda sijui walimalizana vipi..!
Ila yule bwana alitia fora! Teh! Si kwa zile mbio.
Kwanza nunua kofia weka nyumbani , ukijua siku hiyo utapanda BODA,unaweka kwa mfuko mkuuHiyo sheria ipo ila kiafya wadau hii kitu ni mbaya sana,hebu imagine katika hao abiria kama ana mba kwenye nywele au usoni,au kama ana Chawa kichwani au ugonjwa wowote wa kuambukiza,ni hatari sana.Na kwa sie tunaofuga nywele ndefu ni usumbufu sana,ukipanda bodaboda tatu ujue kabisa nywele zako zitakuwa timtim,hali kadhalika wanawake ambao hawasuki ukiweka style yako lazima ivurugike.
hahahahahahhaaaaaaahapo sawa wadada na nywele zetu nyingi kama vichwa viwili tutengenezewe zetu speial
Sitegemei kama kila mtumiaji wa bodaboda huwa anajipanga toka nyumbani kuwa anakwenda kupanda bodabodaKwanza nunua kofia weka nyumbani , ukijua siku hiyo utapanda BODA,unaweka kwa mfuko mkuu
Hiyo nayo sheria nyingine au mawazo yako!Kwanza nunua kofia weka nyumbani , ukijua siku hiyo utapanda BODA,unaweka kwa mfuko mkuu
Ukipanda bodaboda dai kofia yako