Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,196
- 25,515
Mwanzo mwanzoni nikiri kuwa nimefuatilia na bado naendelea kuchambua Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Kuna jambo, lakini, nimeliona kwa haraka. Ni kuhusu pendekezo la kupunguzwa kwa adhabu kwa makosa ya barabarani kwa waendesha pikipiki almaarufu kama bodaboda na bajaji. Imependekezwa na Waziri wa Fedha jana Bungeni kuwa adhabu kwa kosa moja ipunguzwe kutoka shilingi elfu 30 za sasa hadi shilingi elfu 10.
Pendekezo hili, hakika, lilishangiliwa pakubwa na Wabunge na hata Spika alimtaka Waziri wa Fedha kurudia pendekezo hili na kushangilia kukatamalaki tena Bungeni. Adhabu za barabarani ni sehemu ya kuwarekebisha wamiliki na watumiaji wa vyombo vya usafiri. Ingawa elimu na maonyo hayatumiki sana na askari wa usalama barabarani, adhabu za faini zimekuwa zikitumika zaidi na zimeonyesha mafanikio ya angalau 'kuwatisha' wahusika.
Katika uga wa kisheria, 'kutisha' hutumika kama njia ya kurekebisha na kuzuia wengine kutenda kosa. Ndiyo maana imekuwa kawaida kusikia mahakama ikitamka kuwa 'adhabu hii iwe fundisho kwa wengine...'. Hapo ameadhibiwa mkosaji na kutishwa yeyote anayeelekea kukosa. Kimsingi, adhabu za faini barabarani ingawa wakati mwingine zinatumika vibaya zimepunguza kwa kiasi kikubwa makosa ya barabarani kupitia kutisha kwake.
Je, kupunguzwa kwa faini hizo/ 'vitisho hivyo' kwa watumiaji wa pikipiki na bajaji, hakutachochea makosa ya usalama barabarani na kuleta usumbufu kwa watumiaji wengine wa barababara wakiwemo wenye magari na watembea kwa miguu? Serikali imejiridhisha vya kutosha juu ya jambo hili kabla ya kuja na pendekezo la punguzo hilo la jana ambalo kwa mazingira ya Bungeni linakwenda kupitishwa?