Online Shopping and Shipment | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Online Shopping and Shipment

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by sniper619, Aug 10, 2011.

 1. s

  sniper619 Member

  #1
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Habari zenu wana JF...sikupata forum nyingine yeyote zaidi ya hii kuwasilisha hoja yangu...

  Nataka kujua kama yupo yeyote aliyewahi kununua online kupitia kwa "e-bay" na akaipata hapa TZ mzigo wake...maana hawa jamaa huwa hawafanyi shipping outside US..

  Wanauza vifaa bei nzuri sana...nimewahi kununua kwao External HDD ya 1TB Western Digital kwa $139..nilileletewa na jamaa yangu...lakini natafuta njia ya kuagiza vitu vingine bila kutegemea mtu wa kuileta...

  Naomba info. on this matter...
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu ebay ni shopping platform inaounganisha sellers and buyers.. (kwahiyo shipment in African countries ni chaguo la muuzaji)

  Hata hivyo wengi huwa hawapendi ku-ship Africa sababu ya usumbufu na uonga wa kutapeliwa...

  Anyway kuna njia ambayo unaweza ukatumia kampuni ambazo zinakupa address ya USA ili kila muuzaji ajue upo US, baada ya hapo watafanya consolidation mizigo yako na kukutumia sehemu ulipo, So unaweza ukanunua from A, B, C na D, mizigo ikatumwa kwa hawa jamaa ambao wakakusanya yote na kutuma kama mzigo mmoja..

  Angalizo hawa jamaa wa customs busara zao wanaweza wakakulima ushuru hadi ukashangaa na ukaona bora ungenunua Bongo... So jaribu kuangalia ushuru ni kiasi gani kabla haujaagiza

  kampuni za mail forwading zipo nyingi jaribu ku-google moja wapo ni USA2ME, RV Mail Forwarding Services, Remailing, US Mailing Address, Mail Receiving Forwarding
   
 3. a

  ammah JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kuna seller wana ship worldwide. Unaweza kwenda kwenye advance search. Nimenunua vitu maraa kadhaa ebay na sijawahi kupata tatizo lolote.
   
 4. K

  Karry JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  thanx kwa ufafanuzi na siisi tumepata naelekea e-bay
   
 5. e

  elf miaka Member

  #5
  Aug 14, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ila matapeli kwenye mtandao ni wengi siku hizi jitahidi kuwa makini na njia yeyote utakayopata
   
 6. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Ebay kuna feedback na ratings (kila mteja akinunua kitu anaacha feedback) kwahiyo ukinunua kwa mtu mwenye feedback nzuri na high ratings ni vigumu kukutana na tapeli sababu watu wanaogopa kupata ratings mbaya sababu zinaweza kuwaletea bad impression na kupoteza wateja... Ukinunua direct from amazon na sio amazon affiliates hakuna tatizo sababu Amazon ni reputable company

  Kwahiyo ukinunua kwenye hizi platforms za sellers/buyers (alibaba, ebay n.k. ) ni vizuri udeal na mtu ambae ameshafanya biashara zaidi ya mwaka kama miaka 2 hivi sababu matapeli wengi huwa wanaiba na kubadilisha ID kila mwaka sababu wakishaiba watu huwa wanashituka na kutoa complaints
   
 7. samito

  samito JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Good sred
   
 8. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,796
  Likes Received: 2,570
  Trophy Points: 280
  Vipi usalama wa parcel ikifika bongo? Je wahuni hapo cargo hawezi kuchomoa vitu?
   
 9. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  kama mzigo sio mzito less than 45kgs shippers wengi huwa wanapenda kutumia door to door (express) (dhl, ups, fedex, n.k.) hii ni safe kabisa tena wanakufanyia clearing wenyewe pesa za ushuru unawapa alafu wanakulipia inachukua kama siku saba tu kufika..., EMS /Post office inachukua muda alafu sidhani kama ni safe sana cause inapitia posta (na nimeshasikia watu wanapoteza mizigo)

  Kama mzigo ni mzito zaidi ya 45kgs ni bora utumie air cargo ambayo inakuja na ndege mpaka airport hapa inabidi utumie clearing and forwarding agent ili afanye clearing sababu huruhusiwi kufanya clearing mwenyewe...

  Kwahiyo it depends mzigo mwepesi less than 45kg (door to door is cheaper)
  Mzigo mzito over 45kgs (air cargo is cheaper)
  na zote ni safe kabisa
   
Loading...