Ongezeko la Posho za Wabunge ni Wizi na Dhulma dhidi ya Wafanyakazi

sasa nitaacha hata kusoma na kuchangia posti zinazohusu clouds kwa sababu niliacha kusikiliza na sitaki kusikilizishwa hapa jf.
Hahahahaha! Kweli aiseee una akili sana,ukisoma thread ya radio ya Wafu maana yake umesikilizishwa bana!
 
Juzi Spika Anne Makinda alipofafanua hoja juu ya kuongeza posho kwa wabunge (sitting allowance), alisema wamefanya hivyo kwa sababu gharama za maisha zimepanda (kama kulipia malazi). Najiuliza kitu kimoja,hivi gharama za maisha zimepanda kwa wabunge tu peke yao nchi hii? Na wala sio kwa walimu,madaktari na watumishi wengine wa umma? Na je,gharama hizi ni mkoa wa Dodoma tu ndio zimepanda na si mikoa mingine ya Tanzania?
Mantiki ni kuwa mbunge analipwa posho hizi kwa kuwa yupo nje ya jimbo lake,hivi mbunge anapaswa awe wapi ili ionekane yupo eneo lake la kazi asilipwe posho? Nijuavyo mimi mbunge anapochaguliwa anatakiwa kwenda kuwakilisha wananchi wake bungeni,sasa how comes alipwe tena posho kwa kufanya kazi yake ya msingi?
 
Yaani we acha tu: 1. Mshahara 2. Posho ya Vikao 3. Posho ya Kujikimu 4. Posho ya Mafuta 5. Mkopo wa gari 6...19. Hawa ndio wanatakiwa washerehekee miaka 50 ya Uhuru!
 
Wadau nimenukuu kitabu cha ushairi cha "FUNGATE YA UHURU"kimeandikwa seif khatibu.kuna shair la "fungate"uk 1.
nashusha hapa chin
1.Fungate ya uhuru,bado inaendelea."Harusi" waru nuru,wazuri wanavutia.Wengi inawadhuru,na teru wanaumia.
2.Karamu za fahari,mabembe ya kupepewa.Na majumba mazuri,wamekwisha jijengea.Watembea kwa magari,hivi zimewazowea.
3.Ngoma zisizokwishwa,nakupeana fidia.kila siku zakesha,na kuhamiahamia.Mpigo huu ukisha,mwingine unaingia.
Hili shair lina beti sita,hizo tatu,zingine kesho,nalitafakali hili shair ambalo limeandikwa na Mh;seif khatibu(mbunge na wazir wa zaman)natafakari hiiz posho za wabunge akiwepo na seif na wenzake,wanao fikir sisi watumish wengine atuchangii misiba,shule,maafa mbalimbali,wagonjwa,wamesahu kuwa kutoa n moyo sio utajir
wakatabahu
 
[h=2]08 DECEMBER 2011[/h][h=3][/h]

Nchi imetumbukia Baharini- Dkt.Slaa
*Atamani zitumike kulipa madai ya walimu
*Alilia watoto wa maskini kukosa mikopo

Na Rehema Maigala

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Wilbroad Slaa, amelaani vikali kitendo cha Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda, kukiri na kutetea uamuzi wa ofisi yake kupandisha posho za wabunge huku Watanzania wakitaabika na hali ngumu ya maisha.

Kwa mujibu wa Spika Makinda posho hizo za wabunge zimepandishwa kutoka sh. 70,000 hadi 200,000 kwa siku na tayari wameanza
kulipwa.
Akizungumza na gazeti hili jana, Dkt. Slaa alisema kitendo cha spika kuridhia na kutetea kuwapandishia posho wabunge ni kielelezo tosha kuwa nchi imetumbukia baharini na hakuna msaada wa kuiokoa kwa sasa.

Dkt. Slaa aliyezungumza huku akionesha masikitiko alisema, hakutarajia kama spika angetoa kauli hiyo hasa kwa kuzingatia kuwa bunge ni kioo cha nchi na kwamba jukumu lake ni kusimamia serikali na vyombo vyake vyote kwa masilahi ya wanyonge.
Alisema kauli ya Spika Makinda kukiri kuwapandishia wabunge posho ni sawa na kuwavunja matumaini Watanzania na kwamba wanapaswa kujiuliza ni nani wa kuwasaidia ikiwa wabunge wanajisaidia wenyewe.

“Watanzania wengi wanaishi katika hali ngumu kwa sababu ya maisha kupanda, kipato cha Mtanzania kwa siku ni kidogo ambacho hakiwezi kukidhi matumizi yake ya kila siku.
Lakini Mtanzania huyo hana wa kumsemea wala wa kumpunguzia mzigo mzito ili awe na unafuu wa maisha, hana wa kumsaidia ili awe na maisha mazuri hata kidogo,” alisema Dkt.Slaa na kuongeza.

“Watoto wa kimaskini wengi hawaendelei na masomo ya elimu ya juu kwa sababu ya kukosa mikopo kutoka serikalini, kwa nini hizo pesa zilizoongezwa kwa wabunge zisingepelekwa kwa wanafunzi?

Au tunaithibisha ile kauli inayosema kuwa mwenye nacho anazidi kuongezewa?” Alihoji Dkt.Slaa.Alisema wabunge wamekuwa na posho nyingi za kila aina ambazo zingine hata hazistahili kulipwa huku wakiwaacha Watanzania wakiwa na hali ngumu ya maisha.

Alisema kitendo cha Spika Makinda kutetea posho hizo bila kujali maisha ya Watanzania walio wengi ni dalili ya chombo hicho kuwakandamiza wananchi hivyo kwenda kinyume na kazi ya bunge ya kuwatetea wananchi.

Alisema ni aibu kwa wabunge kuongezewa posho bila hata kuwajali wafanyakazi ambao wengi wao wanalipwa mshahara mdogo na kuwataka Watanzania kwa ujumla kutafakari wanatembea katika mstari upi.

Alisema sehemu kubwa ya umaskini wa Watanzania unatokana na viongozi wa serikali kujigawia posho nyingi ambazo hazina maana yeyote kwa taifa.

“Mpaka hivi sasa walimu bado hawajalipwa madeni wanayoidai serikali, wanatishia kugoma ni vyema posho hiyo ingepelekwa kwa walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa watoto wetu,” alishauri Dkt.Slaa.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari juzi wakati akizindua ripoti ya Maendeleo ya Wanawake Duniani kuhusu haki kwa mwaka 2011, Spika Makinda alikiri nyongeza ya posho za vikao vya wabunge kupanda kutoka sh.70,000 hadi 200,000 kwa siku.

Alisema wamefikia hatua hiyo kutokana na kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma na kwamba wabunge walianza kupokea posho hiyo mpya Novemba 8, mwaka huu.

Akisisitiza umuhimu wa posho hizo alisema sh.70,000 isingemsaidia mbunge kumudu gharama hata za chumba kwa madai kuwa zimekuwa juu kutokana na mji wa Dodoma kuwa kitovu cha elimu ya vyuo vikuu kwa sasa.

“Kila kitu kimepanda bei na kwa bahati mbaya nyumba zile za CDA (Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu) zilizokuwa nafuu zilichukuliwa na wabunge wa bunge la tisa kwa mikataba binafsi na wengi hawajazirudisha hadi sasa ili kuwezesha wapya kuzipangisha,” alinukuliwa akisema Spika Makinda akitetea posho hizo juzi.

Mkurugenzi naye awashangaa wabunge


Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi, Bw. Yefred Myenzi, amesikitishwa na kitendo cha Spika Makinda kutete posho hizo na kuwataka wabunge kutambua kuwa hali ngumu ya maisha ipo kwa kila Mtanzania na si kwao pekee.
Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Bw. Myenzi alisema hali halisi ya Mtanzania hairuhusu mbunge kupandishiwa posho kutoka sh. 70,000 hadi 200,000 kwa siku na kwamba hizo ni anasa .
Alisema wabunge wanavyanzo vingi vya mapato mbali na mishahara yao hivyo hawakustahili kuongezewa posho kiasi hicho huku Watanzania wakizidi kulilia hali ngumu ya maisha.
“Hali hii inaonesha ni kwa jinsi gani wabunge walivyo wabinafsi, wanajali masilahi yao wenyewe na kuacha wananchi wakiumia,” alisema.

Katibu wa Bunge akanusha

Hata hivyo hivi karibuni Katibu wa Bunge, Dkt.Thomas Kashililah, alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akikanusha kuwepo kwa nyongeza hiyo.

Katika taarifa hiyo Katibu huyo wa bunge alikiri kuwa wabunge wanataka waongezewe posho za vikao lakini mapendekezo hayo hayajaanza kutekelezwa.

Alisema mapendekezo ya nyongezo hiyo yaliibuka katika mkutano wa wabunge mjini Dodoma, Novemba 8, mwaka huu walipoiomba serikali iangalie upya suala hilo kwa lengo la kuboroshewa.
Dkt. Kashililah alisema serikali ilikuwa haijatoa taarifa iwapo posho hiyo imeongezeka kutoka sh.70,000 hadi 200,000.

Balozi Seif atetea posho Wakati huohuo, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amesema wabunge kuongezwa posho za vikao ni halali kwa kuwa gharama za maisha katika Mkoa wa Dodoma zimepanda.

Alisema ongezeko hilo litalinda heshima za wabunge pindi wanapokuwa wakiendelea na vikao vya bunge.
“Nafikiri siyo heshima kwa mbunge baada ya kumaliza vikao anakwenda kulala kwenye gesti ya sh. 5000 hii ni aibu, ni sawa posho zilivyopandishwa,” alisema.

Alisema anakubaliana na uamuzi wa serikali kuwa ni mzuri na utampa nafasi nzuri mbunge ya kuishi wakati wa vikao.



 
Mkulo: I`m in the dark

By Felix Andrew

8th December 2011

As controversy rages over reports of massive rise in allowances for Members of Parliament

Finance Mustafa Mkulo has said he does not know whether sitting or any other allowances for Members of Parliament have been increased substantially as reported in the media and confirmed by National Assembly Speaker Anne Makinda on Tuesday.

While Makinda told journalists that the daily sitting allowance during House sessions had risen from 70,000/- to 200,000/-, chiefly owing to hikes in house rental charges in Dodoma, the minister told this paper in a telephone interview in Dar es Salaam yesterday that he knows "completely nothing" on the matter.
Pressed for elaboration, Mkulo recommended that the appropriate place to go for details was the Speaker's Office. (Mhhhhh!! Minister of finance is not aware of this issue:shock:)
"It is better you contact the Speaker for details on what she is reported to have said. As I speak, I know completely nothing about the increase being talked about," he said.

Winding up debate on the 2011/2012 government Budget in July, the minister said the effect of personnel allowances on the national budget was "very minimal".
He said the 2011/2012 Budget totalled 13.5trn/- but personnel allowances accounted for only 352.74bn/-, including 25.65bn/- in sitting allowances for public servants – out of which 4.92bn/- went to MPs.

Correspondents Rose Mwalongo and Gadiosa Lamtey meanwhile report that Ubungo legislator John Mnyika of the opposition Chadema has said that the President, "in his capacity as the First Employer, is the only one with the legal mandate to increase MPs' salaries and allowances, and so far he has not notified notify us (legislators) in writing on the said rise".

"For all I know, the reported review of perks has yet to be approved by the President and is therefore null and void," he noted.
Mnyika made the remarks in a presentation on the role of the legislature at a seminar in Dar es Salaam yesterday organised by the Legal and Human Rights Centre for 50 students from 17 universities.

"The much I remember is that copies of the only letter specifying our salary and allowance levels were given to us when we came to the House last year. We are yet to receive any further memo or other communication in connection with the issue," he said.

According to Mnyika, the National Assembly is not allowed to discuss its own (MPs') allowances, "and some legislators once raised the matter with Prime Minister Mizengo Pinda and he promised to find another session at which to discuss the issue".
The MP further explained that, under parliamentary regulations, allowances are normally deposited into MPs' personal accounts weekly depending on the attendance of each legislator.

A number of academics, private sector employees and ordinary citizens also faulted the decision to increase allowances in respect of MPs and other senior public servants without the benefits trickling down to the rest of the population, particularly lowly paid employees.
Most said the practice was unfair and unjustified in that it came when a significant number of Tanzanians survived on less than one dollar a day.

A visibly enraged Tanzania Media Women Association (TAMWA) executive director Ananilea Nkya described the reported hiking of MPs' allowances as "daylight robbery that ought to be condemned in the strongest terms".

"It's absurd and totally against the principles of good governance. Everybody, every Tanzanian, must condemn the payment of the new package. We must join forces and ensure the decision (to pay the hiked allowances) is rescinded," she said in an interview.
"The package should be scrapped immediately, and this should be done regardless of whether the allowances are justified by law or custom or regulation," she added.
Nkya said the allowances were being paid while millions of Tanzanians were facing life-threatening problems relating to vital infrastructure and provision of basic goods and services such as food, housing, education, health, clean and safe water and electricity.
Dr Benson Bana, a political scientist and lecturer with the University of Dar es Salaam, was recently quoted as criticising the whole idea of paying MPs and senior civil servants on routine duty what is vaguely known as sitting allowance.

"My stand has always been clear on this issue. There is no justification of paying allowances to both MPs and senior government executives while they are executing their routine duties," he said.

The don, an expert in human resources management, said there was no scientific evidence of sitting allowances necessarily serving as an incentive to employees.
"Sitting allowances to public leaders is not duty facilitation allowance in meetings. It is not brain-facilitation allowance in meetings. It cannot be used as a motivational ingredient for improving performance of public leaders," he argued.
He said sitting allowances could be justified only if paid after one had genuinely worked beyond official hours.

Contacted for comment on the issue of MPs' allowances, Zanzibar Second Vice President Seif Ali Iddi said the government had done the right thing because the move would motivate the legislators into better performance.

"I don't want to comment any further on the matter because (National Assembly) Speaker Anne Makinda has given enough clarification. I hope everyone has understood her because there are no ill motives on the part of the government," he added.

SOURCE: THE GUARDIAN
 
Niliwahi kumsikia Mh.Lusinde mbunge wa Mtera akisema wabunge wapimwe akili wanapokuja Bungeni. Sikumuelewa lakini sasa naanza kuimuelewa! Wabunge wote wapimwe akili tujue kama ziko sawasawa! Maana walichokifanya ni sawa na uwendawazimu.
Nchi ya tatu kwa kuwa ombaomba Duniani leo mkajipandishie posho namna hiyo? hicho ni nini kama sio wazimu? MIMI SIJUI NANI ATAWAPIMA LAKINI KWAKUWA HOSPITALI YA VICHAA IKO HUKO HUKO DODOMA!! TUNASHAURI WAUGUZI WA MIREMBE WAKAIFANYE KAZI HIYO!!!! Labda baada ya hapo watawaza vizuri na kutunga sheria kama kazi yao inavyowataka. Na sio kutunga viwango vya posho.
Wameniharibia siku sana hawa jamaa.

Wapiga kura pia wapimwe akili coz walichagua wabunge wenye pepo wachafu.
 
Niliwahi kumsikia Mh.Lusinde mbunge wa Mtera akisema wabunge wapimwe akili wanapokuja Bungeni. Sikumuelewa lakini sasa naanza kuimuelewa! Wabunge wote wapimwe akili tujue kama ziko sawasawa! Maana walichokifanya ni sawa na uwendawazimu.
Nchi ya tatu kwa kuwa ombaomba Duniani leo mkajipandishie posho namna hiyo? hicho ni nini kama sio wazimu? MIMI SIJUI NANI ATAWAPIMA LAKINI KWAKUWA HOSPITALI YA VICHAA IKO HUKO HUKO DODOMA!! TUNASHAURI WAUGUZI WA MIREMBE WAKAIFANYE KAZI HIYO!!!! Labda baada ya hapo watawaza vizuri na kutunga sheria kama kazi yao inavyowataka. Na sio kutunga viwango vya posho.
Wameniharibia siku sana hawa jamaa.

Wapiga kura pia wapimwe akili
coz walichagua wabunge
wenye pepo wachafu.
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe CHADEMA amewataka wambunge wote warejeshe pesa zote zilizozidi walizopewa kama posho kwasababu walipewa nje ya utaratibu na kinyume cha sheria

MY TAKE:
Hiiposho siieleewi vizuri hapa Mbeya tuliwauliza wabunge wa CDM kama wamechukua hizo hela

MAJIBU: Hizi ni propaganganda za CCM wanataka kuwaondoa watu kwenye mjadala wa katiba Posho hatupati hiyo 200000/= na wala 70000/= ila ni 50000/=(Naomi Kailuki na Basil Lemma)

Kwanini CDM wanagongana kuhusu posho leo nasikia SHIBUDA anasema wanaobisha posho mpya ni mambumbu huku akishangiliwa na wenzake

Naomba tutafakari kwa kina .........."asante"..........
 
Kutoka Gazeti la Tanzania Daima

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*



CHADEMA: Posho za wabunge ni ufisadi
• Wataka Katibu wa Bunge awajibishwe

na Charles Misango
amka2.gif


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetishia kuchukua uamuzi mgumu kupinga nyongeza ya posho za vikao vya wabunge, kwa madai kuwa hakipo tayari kushirikishwa katika kile walichokiita ufisadi.

Taarifa ya CHADEMA iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, jana, imesema kuwa nyongeza hiyo ni haramu na inapaswa kusitishwa kwa kuwa imefanyika kinyume cha taratibu na haina uhalali wowote kimantiki, kwa kuwa haijazingatia uhalisia wa maisha ya wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla.

CHADEMA kimesema nyongeza hiyo ya posho ya vikao ni matumizi mabaya ya madaraka na ni dharau kwa walipa kodi wanaohangaika na kupanda kwa gharama za maisha na athari za ubadhirifu wa fedha za umma, kwa kuwa wananchi wengi ni waathirika zaidi wa kupanda kwa gharama za maisha kuliko wabunge.

 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe CHADEMA amewataka wambunge wote warejeshe pesa zote zilizozidi walizopewa kama posho kwasababu walipewa nje ya utaratibu na kinyume cha sheria

MY TAKE:
Hiiposho siieleewi vizuri hapa Mbeya tuliwauliza wabunge wa CDM kama wamechukua hizo hela

MAJIBU: Hizi ni propaganganda za CCM wanataka kuwaondoa watu kwenye mjadala wa katiba Posho hatupati hiyo 200000/= na wala 70000/= ila ni 50000/=(Naomi Kailuki na Basil Lemma)

Kwanini CDM wanagongana kuhusu posho leo nasikia SHIBUDA anasema wanaobisha posho mpya ni mambumbu huku akishangiliwa na wenzake

Naomba tutafakari kwa kina .........."asante"..........

Mkuu hapo kwenye Red!

1. Leo unamaanisha jana 8 Dec?

2. "Mambumbu" anamaanisha sisi wananchi au wabunge?

3. "Wenzake" unamaanisha wabunge au wananchi?

Kwa ujumla posho zote zinatakiwa kufutwa isipokuwa posho ya kujikimu basi. Ikumbukwe yeye alishasema "kwa kazi za mbunge, hata akipiwa posho ya 500,000/= ni sawa!". Ni aibu kuwa na mbunge mwenye mawazo ya namna hii akiwa anawakilisha watu maskini katika nchi maskini.

 
Huwezi kupata jibu moja linapokuja suala la posho kwa kuwa hata hao wabunge wa Chadema, wapo wanaoongozwa na matamanio binafsi.

Anna Makinda amekiri ongezeko la posho na ndio Zitto alipomkamata kuwa ni kinyume cha Sheria. Sasa huyo Lema na wengine wanachofanya ni kuwababaisha wananchi. Posho wanapokea na wanakula
 
Hivi kwa wabunge ambao sikuzote hawapo majimboni mwao,ina maana wanapewa hiyo 80,000 kila siku?Kuna wabunge walionekana jimboni wakati wa uchaguzi,ulipomalizika wakachukua ushindi kwa mabavu na kupotea!!!!
 
Huwezi kupata jibu moja linapokuja suala la posho kwa kuwa hata hao wabunge wa Chadema, wapo wanaoongozwa na matamanio binafsi.

Anna Makinda amekiri ongezeko la posho na ndio Zitto alipomkamata kuwa ni kinyume cha Sheria. Sasa huyo Lema na wengine wanachofanya ni kuwababaisha wananchi. Posho wanapokea na wanakula
Mkuu tatizo langu kwa nini wasiwe wakweli kuliko kutudanganya kama wanavyo fanya wanapata 70,000/= au 200,000/= lakini wanasema tunachukua 50,000/= Chadema tunatarajia wawe wakweli daima uongo ni Sumu mbaya mno
 
Hivi huyu Maalim Seif amekamata kacheo ka umakamu wa Rais wa Zenj ndio anaongea lugha gani hiyo?
 
Mkuu tatizo langu kwa nini wasiwe wakweli kuliko kutudanganya kama wanavyo fanya wanapata 70,000/= au 200,000/= lakini wanasema tunachukua 50,000/= Chadema tunatarajia wawe wakweli daima uongo ni Sumu mbaya mno

Kama ulikuwa umeweka matarajio yako yote kwa Chadema, basi anza kutafakari njia nyengine ya kuikomboa nchi yako
 
Hiyo 70000 ikikatwa kodi naona inabaki 50000,Makinda,katibu wa bunge + jk wote hawajatimiza wajibu wao
 
Back
Top Bottom