One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!


...Kilichoudhi zaidi wakati wananchi wako busy kuidiscuss Elimu wanayopewa na M4C yeye ili kuwachanganya akaitisha waandishi wa habari na kuwatangazia "...nautaka uraisi kupitia CHADEMA" Bila shaka aliagizwa hivo na akina Wasira na Zoka ili kudivert attension ya raia kwenye elimu inayotolewa na M4C.
Swali: Lengo lako la kugombea urais bado lipo au ndo biashara na waliokutuma ilishakamilika?
 


Inachekesha sana, wengi humu wanamuuliza Zitto maswali waliyokuwa hawathubutu kuwauliza viongozi wao ndani ya CDM, na labda hadi sasa wanaogopa kufanya hivyo.

Mnauliza kuhusu mchanganuo wa mapato ya ACT, lakini sikuona mwana CDM aliyesapoti waraka uliokuwa unauliza maswali haya haya yaliyojaa humu ndani.

Waraka ulivyotoka wengi tuliwashauri CDM wa-calm down na ku-deal na mazuri ya waraka kiutu uzima na vijembe vya hapa na pale, na pale kina kitila walikoteleza wapotezee, lakini hot heads prevailed. Sasa ACT wanafanya walichoamini kwenye ule waraka imekuwa tatizo.

Imagine kama CDM wange-intergrate waraka kwenye siasa zake, na kuwaachia wapiga kelele nao waendelee, leo hii wangekuwa wanai-attack CCM on all fronts, kisera, na kwenye majukwaa pia.

Sasa hivi sehemu pekee CCM inatishwa na CDM ni kwenye majukwaa ya siasa, ambayo platform yake haipatikani kila siku, kwani huwezi kuitisha mkutano bila siku bila sababu,ndio maana sehemu pekee CDM inaweza kufight back against CCM ni wakati wa bunge, au kukitokea kashfa flani.

Waraka was CDM's biggest blunder, and missed opportunity, you could have punished Zitto and Team and bar him from party politics for a year or so, while internally digest waraka wao na kufanya nao kazi inakobidi.isingewapunguzia chochote.

Sasa inabidi mfanye kazi besides them, and i have yet to hear a CDM leader talk of "sera" for the past year or so.
 
mimi huwa nacheka sana...ati Ujamaa!? Nyerere alichemka na akatuletea umasikin ati leo zito mjamaa? wa wap kwanza wew.. mtu tajiri hivi ati mjamaa!!!!!! zito bwana anambwembwe sana
 

Nakushauri uandike tu kwa Kiswahili mkuu.Unalazimishia kiingereza usichokijua.Sitakuwa nimekosea nikisema umeishia Form Four shule za Kata.

Samahani kama nimekuudhi..
 
Nakushauri uandike tu kwa Kiswahili mkuu.Unalazimishia kiingereza usichokijua.Sitakuwa nimekosea nikisema umeishia Form Four shule za Kata.

Samahani kama nimekuudhi..


Wala usijali, nimezoea kadhia ndogo ndogo kama hizi kutoka kwa pro CDM, hazijaanza leo. Kuhusu Elimu yangu hapa si mahala pake, ukitaka kufungua mada kuhusu elimu yangu fungua tukayaongee huko.
Now, let's get back to discussing issues at hand, enough about Kimweri.au vipi?
 
Hili jibu ni jepesi sana, mlishauriwa muunde chama cha wazalendo au chama kinachoitwa wazalendo? Iwe chama au mtu huitaji kujiita mzalendo ni matendo yako yatakayopelekea watu wakuite mzalendo. Hebu onyesha ukomavu, mbona chama ulichofukuzwa ulisema hakuna demokrasia wakati hicho chama kinaitwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo au waanzilishi wa chama hiki neno demokrasia hawakushauriwa na wananchi ndio maana hakunademokrasia kama mnavyodai?
 

Malengo ni mazuri nia ni mzuri lakini sina imani na njia munayotumia au munayotaka kutumia. Kupambana ukiwa jeshi la mtu mmoja ni ngumu lakini ukiunganisha nguvu na wapinzani wengine itakuwa njia mzuri zaidi. Binafsi naamini watanzania wengi wanataka mabadiliko na wamechoshwa na ccm lakini bado wanaichagua ccm kwakukosa imani na upinzani. Ushauri wangu ukiupenda chukua usipoupenda achananao """"Unganisha chama chako na ukawa ili kuongeza nguvu ya upinzani Tanzania"". Pia nikushauri usipende kujipa madaraka makubwa wewe bado mtoto kwenye siasa, naomba ufanye siasa madaraka yatakuja automatically. Ulichokifanya act kujipa madaraka makubwa ni utoto. Ulitakiwa uiongoze act ukiwa kama mwanachama wakawaida ili ukiongoze chama ukiwa mafichoni. Simaanishi nakulaumu huo ni mtazamo wangu. Kwasasa jambo jema kwako nikufanya muungano wa vyama ili tuiondoe ccm. Kubaki act ikifanya siasa kivyakevyake itatuaminisha kwamba wewe ni shushu wa ccm kitu ambacho binafsi sitaki kuamini. Kwasasa wewe ni kiongozi wa chama chako cha siasa hivyo ukipeleka wazo lakuungana na ukawa itakuwa safi sana ukizingatia mjadala wa wewe na cdm ulishafungwa, kwahiyo kwasasa unanafasi kubwa yakufanya kazi pamoja na cdm, cuf, nccr, na vyama vingine kila mmoja akitokea kwenye chama chake.

Ni ushauri tu Brother zitto.
 
mimi huwa nacheka sana...ati Ujamaa!? Nyerere alichemka na akatuletea umasikin ati leo zito mjamaa? wa wap kwanza wew.. mtu tajiri hivi ati mjamaa!!!!!! zito bwana anambwembwe sana
Kama sio kutafuta mass popularity ni wendawazimu karne hii kuongelea ujamaa, hasa ujamaa wa Tanzania ambao Dr, Mazrui aliuita "Nyerererism" kutokana na mfumo wake ambaa haukuwai tokea sehemu yeyote duniani.
 
Mie ninachofikiri zitto alileta thread hii ili ajue watu wanamuonaje kuhusu chama alichokianzisha kudhoofisha upinzani na madaraka aliyojitwalia.mie nimepitia comments za watu mbalimbali nikafanya tathmini na kugundua zaidi ya 90% hawakubaliani nawe hata kidogo hiyo 10% ni wale waganga njaa walio tayari kuikana kweli ili tu mkono uende kinywani. OMBA TO MH.ZZK UMEPOTOKA KWA KUSALITI HARAKATI ZA MAGEUZI KISA NJAA YA UMARUFU NA MADARAKA.
 

Kamwe, Never hatuwezi kuiondoa ccm madarakani kwakuanzisha vyama kiholela. Tunahitaji kuunganisha nguvu za upinzani. Siasa sio kigodoro kwamba ukiweka taarabu mzuriiiii ndo utajaza watu kwenye unyago wako.
 
Last edited by a moderator:
zito unamawazo finyu ujafungua kujipambanunua kama kweli una dhamira ya dhati na hii nchi chama chako kingeweka kipaumbile kupambana na umaskini kupitia rasilimali na pato la taifa kama tunavyoomuona julius malema, wewe unajinasibu kupambanana na chadema siyo kiongozi wa kweli, kiongozi wa kweli atengenezi wafuasi anatengeneza viongozi km wewe mbowe alivyokutengeneza.
 
Ajitafakari! Kwa usaliti wake Kigoma bendera nyingi za ccm zinapepea. Huu ni uzaliti! Kwa kujua au kutojua anajaribu kuirudisha ccm madarakani (hasa jimboni/mkoani kwake)
 
Je hayo ya kweli!


CC Kurugenzi ya Habari.
 
Last edited by a moderator:
Kaka Zitto Ukiwa Mwongo Usiwe Msahaulifu na Ukiwa Msahaulifu Usiwe Mwongo, Umekuwa Unatoa Kauli Tata Zenye Ukakasi.

Rejea kauli Zako Unazozitoa Zinatufanya Tukose Kukuamini Kwa kila Unachokifanya Sasa.

MAISHA MEMA
 
Zitto, swala la ujamaa hutaliweza kamwe! Wewe danganya wafuasi wako ila huo ndo ukweli!
 
Last edited by a moderator:
...but many uncoordinated fronts can lead to friendly-fires!!
 
Ndugu yangu Zitto! Nikihitaji nakala ya ilani na katiba vinapatikana wapi kwa huku Arusha? Au mna tovuti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…