One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,890
Ndugu wana JF,

Kwa muda mrefu na hasa siku za hivi za karibuni kumekuwa na threads nyingi sana humu ndani kuhusu Zitto na kuhusu Chama cha ACT Wazalendo. Kumekuwa na tuhuma kwamba chama cha ACT Wazalendo kinashambulia vyama vingine vya upinzani hapa nchini. Napenda kusema mambo machache sana

Chama cha ACT Wazalendo ni chama cha siasa chenye mrengo wa kushoto na kinajitanabaisha na siasa ya Ujamaa iliyoasisiwa na Azimio la Arusha. Lengo letu ni kueneza siasa zetu zenye mrengo huo.

1. Chama cha ACT Wazalendo kwa sasa ni chama cha upinzani nchini. Kimekuja kuhuisha zaidi siasa za upinzani ili kuiondoa CCM madarakani. Chama cha ACT Wazalendo hakina lengo hata kidogo kuzorotesha upinzani nchini. Tofauti zetu tulizokuwa nazo katika chama tulichokuwamo wengine tumeshazifuta, tumepiga mstari na kutazama mbele.

Ndio maana hutasikia kiongozi hata mmoja wa ACT Wazalendo akihangaika na vyama vingine vya upinzani. Hata tukichokozwa namna gani tumefanya maamuzi kwamba hatutajibizana na chama kingine chochote cha upinzani hapa nchini. Tutapambana na chama tawala ili kubomoa mfumo wa uchumi unaonyonya wengi na kufaidisha wachache. Tutapigania uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi. Tutapambana na ufisadi kwa nguvu zetu zote. Hizo ndizo kazi tulizo nazo.

2. Tunasisitiza, tunayo vita moja lakini una njia nyingi za kupigana dhidi ya adui. Huko tulipokuwa tulitofautiana mbinu hizo. Sasa tumepata jukwaa la kutumia mbinu hizo. Wenzetu watumie mbinu zao pia. Hatimaye kila mmoja alenge shabaha kwa adui mmoja. Tunasema One Struggle, Many Fronts

3. Kuitana mamluki, wasaliti nk ni siasa za framing tu. Sio mara ya kwanza siasa hizi kutumika nchini katika kujaribu ku frame watu. Mwaka 1995 Mrema wa NCCR aliita CHADEMA chama cha mashushu kutoka Benki Kuu na kila mtu alimwamini. Leo Mrema yupo wapi na CHADEMA ipo wapi? Mwaka 2000 mpaka 2005 CUF ndio ilikuwa chama kikuu cha upinzani na kuidharau CHADEMA. Mwaka 2013 CHADEMA iliita CUF chama cha mashoga.

Miaka yote Mbatia amekuwa akiitwa pandikizi nk. Yote haya hayajazuia vyama hivi kufanya kazi pamoja hivi sasa. Ni vizuri sana wanasiasa kuweka akiba ya maneno. Hakuna sababu ya kutukanana na kuitana majina mabaya. Tunachohitaji ni kila mmoja kumlenga adui ili kumshinda. Tulishindwa kufanya kazi ndani ya moja, tunaweza kufanya kazi tukiwa majirani. Adui bado ni yule yule.

4. Sisi ACT Wazalendo tutachochea kuni kuwasha moto wa mapinduzi nchini kwa kuendesha siasa za masuala (issues). Tumeanza ziara yetu mkoa wa Ruvuma kwa sababu ni mkoa ambao wabunge wake wote ni CCM. Tutaweka nguvu sana maeneo hayo badala ya maeneo ambayo tayari vyama vingine vya upinzani vina nguvu. Sisi katika ACT wazalendo tunataka kuona uchumi unarudi kwa wananchi wenyewe badala ya uchumi kushikiliwa na watu wachache.


Tunataka kuona Miiko ya Uongozi inarudi ili kurejesha imani ya wananchi kwa viongozi wao. Tunataka kuona mfumo madhubuti wa uwajibikaji nchini. Hayo ndio mapambano yetu. Hayo ndio maelekezo yetu kwa wanachama wetu; Kupambana na adui mmoja tu - CCM.
 
Mkuu Zitto hiki chama kimesajiliwa kama ACT Tanzania hii ACT Wazalendo imetoka wapi, au ni chama tofauti?

Lakini pia ninaomba utupe tofauti ya kiongozi mkuu wa chama na mwenyekiti wa chama, majukumu yako ni yapi ukitofautisha na yale ya mwenyekiti.

Pia ulisikika ukiri kwamba wewe ni mwanzilishi wa chama ukiwa bado chadema, huoni huu ni usaliti na uhaini?
 
Kama malengo yenu ni haya kwa nini msijiunge na UKAWA? Katibu mkuu wenu alisikika akisema chama chenu kitaisambaratisha CUF mikoa ya Pwani, huoni kama ulichoandika juu ni kujikosha tu? kwamba lengo lenu ni kupambana na upinzani

Hiyo namba 4 yako ina lengo ovu, na haita-apply kwenye chama chako, vyama vingine vilianzishwa na watu safi ndio maana viling'ara, si hivyo kwa hiyo ACT yako.
 
Mh. Zitto. Aksante kwa ufafanuzi huu.

Ninapenda kukupongeza sana kwa uwezo wako mkubwa wa kuswitch your political passion from one political party to another maana kwa wengi niliowashuhudia huwa inawachukua muda kidogo kuweza kuamua chama gani wahamie in case wanataka au kutarajia kuhama katika vyama vyako.

Wengi huwa inawachukua muda mrefu kuinternalize nia na madhumuni ya chama kipya. Lakini wewe ni kichwa maana mpaka imebidi wakupe na uongozi mkuu meaning wamekuamini sana. Je unaweza kushare na sisi how was this possible angalau na wengine wajifunze?
 
"Msiwaamini wanasiasa".......by Zitto Zuber Kabwe.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu Zitto , acha kutufanya watanzania wote wajinga na hatuoni mnachokifanya au hatusikii mnayoyaongea,

Ni juzi tu hapa Mwigamba kiongozi wa ACT alisema ACT itahakikisha inaifuta CUF Pwani sasa niambie je lengo la Mwigamba ni nini??

Ni majuzi tu hapa ulisema kuwa Ukawa ni wasaka tonge je lengo lako lilikuwa nini?

Ni lini wapi viongozi wa vyama vya upinzani umeishambulia ACT?
 
Last edited by a moderator:
Kama kweli mkiyaishi hayo uliyoyanena, nadhani mtakuwa katika mstari nyoofu kama chama cha upinzani.

Tatizo kunavifaranga vilivyo chini ya KIONGOZI WA CHAMA kutwa nzima kuishambulia CHADEMA na CUF! Na hatujaona "Taswira ya chama" ukiwakemea na hapo ndipo mnapofungamanishwa na tuhuma za kuwa vibaraka wa "Jembe na Nyundo"
 
ZZK katika mada zake hapo awali ukiwa CHADEMA miaka ya nyuma, alisema hivi wakati wa uchaguzi vya vipya huanzishwa kwa malengo ya kugawa kura, UMELITIMIZA HILO na malengo ya ACT ni kugawanya kura za upinzani, maana yake kazi kubwa ya ACT ni kusafisha njia ya CCM. YAANI ccm imebinafsisha jitihada za kuweka fitina kwa upinzani, sub contracted ZZK.
 
fikirikwanza

Siasa ni mapambano. Siwezi kuacha mapambano. Sijawahi fanya usaliti wowote. kuitana majina hayo hakusaidii lolote zaidi ya kufurahisha ego zetu tu. ACT Wazalendo ina shabaha moja tu nayo ni kupambana na mfumo wa uchumi unaonyonya watanzania. Ku surrender mapambano hayo ndio usaliti. Tutaendelea kupambana
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Zitto heshima kwako,

Mimi ni kati ya watu wanaoamini kwenye maono ya mtu hata awe adui yangu vipi, nitasema kweli kuwa mtu huyo atafika mbali sana, lakini pamoja na mtazamo chanya nilionao kwako, wewe umekuwa ukibaldilika badilika na kubadilisha kauli mara kwa mara kiasi kwamba ni ngumu sana kukuamini, unakumbuka jana EATV unasema umevuna wanachama wa CHADEMA 200 Moshi Mjini, Bado Arusha nk?

Unakumbuka ulivyosema mnataka majimbo ya Kawe, Ubungo, na Segerea? Bila kujali nguvu ya Upinzani hasa CHADEMA maeneo hayo? nilitafsiri kuwa pengine una hasira.. lakini ni bora ukatulia kwanza,

Wenzako kwenye chama wala hawaelewi adui yao ni nani..wanajua CHADEMA inangoza nchi, sasa dawa ni kupambana nayo, muulize Mwl. Kaijage or what it is atakwambia "anavyoishughulikia CHADEMA"

Bado wewe bila kujua unahitaji support ya watanzania wakati uanajua wamechoshwa na LiCCM nyie mnakuja na mbadala wa upnzani kuisaidia CCM.

Hujawahi popote narudia popote kuionya CCM kuishambulia CHADEMA na Upinzani kwa ujumla huku wakikusifia wewe, bila kujua kuna siku utapigwa virungu na kuwekwa Lupango ikionekana ni mpinzani kweli?

Mimi nakutakia kila la kheri Mkuu, lakini ujue kuwa siasa ni zaidi ya Mikakati na mbinu za darasani anazowafundisha kitila..Siasa ni watu.. na political wind inawabeba UKAWA... check that out with your team.
 
ZZK katika mada zake hapo awali ukiwa CHADEMA miaka ya nyuma, alisema hivi wakati wa uchaguzi vya vipya huanzishwa kwa malengo ya kugawa kura, UMELITIMIZA HILO na malengo ya ACT ni kugawanya kura za upinzani, maana yake kazi kubwa ya ACT ni kusafisha njia ya CCM. YAANI ccm imebinafsisha jitihada za kuweka fitina kwa upinzani, sub contracted ZZK.

Lengo langu na wenzangu siku zote limekuwa hilo. Kama tumekoseshwa jukwaa la kupambana, njia nzuri ni kutafuta jukwaa lingine. Tunapambana kupitia ACT Wazalendo
 
Ningependa kujua jinsi gani mtarudisha uchumi kwa wananchi,mikakati gani chama cha ACT itafanya.

Tumeainisha vizuri sana kwenye ilani yetu ya uchaguzi mwaka 2015 na tutafafanua zaidi kwenye Azimio la Arusha lililohuishwa.

Moja ya sera zetu ni kukomesha kabisa uporaji wa ardhi nchini kwa kuhakikisha wananchi wanamilikishwa ardhi ya kilimo na ufugaji. Mashamba yote yaliyokuwa ya NAFCO yakabinafsishwa yatarejeshwa kwa wananchi na kugawiwa kwao kwa kilimo kwa mfumo wa outggrowers scheme.

ACT Wazalendo imeamua kusimama masuala yanayohusu wananchi. Naomba upate nakala ya ilani yetu uweze kujisomea
 
Hata hivyo hujawahi kujibu tofauti kati ya ACT -Wazalendo na ACT -Tanzania... kipi ni kipi.

ACT Tanzania ndio ACT Wazalendo. Baada ya kufanya tafiti kwa wananchi ilionekana wananchi wanataka chama kitakachowarejeshea uzalendo kwa Taifa lao.

Wananchi wengi walishauri iundwe Chama Cha Wazalendo. Hivyo tukaboresha jina letu kwa mujibu wa katiba yetu na kuitwa ACT Chama cha Wazalendo
 
Hongera kwa uamuzi wako! Nina maswali mawili tu,

1. kwa nini mashabiki wako wengi waliomo humu ni manazi wa CCM, huoni inakutia doa?

2. Vijana wengi wa ACT waliomo kwenye jukwaa hili wamekuwa wakiishambulia chadema, mfano ACT yachukua wanachama wa chadema. Pamoja na yote haya, hatujasikia kauli ya chama juu ya hili. Houni hili bandiko lako haliwiani na kile kinachoendelea kivitendo?
 
Back
Top Bottom