One night stand ...

One night stand ...

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,916
Leo nimejikuta nashanga halafu nikadhani labda ni ushamba au ni kitu gani na hatimae nikajikuta nikiwaza kama ni haki ya mimi kushangaa au nahitajika kujishangaa

Kuna wadada wamekuja kazini kwangu wakihitaji huduma,katika kutoa huduma nikajikuta naingia kwenye maongezi nao na kama kawaida ya maongezi tuliongea mengi sana na hatimae tulijikuta tunaongelea mahusiano

Tulifikia kuzungumzia mahusiano ya aina mbali mbali na vimbwana vyake na ndipo dada mmoja aliponishangaza sana kwa kusema kuwa anamkumbuka jamaa mmoja hivi ambae walikutana safarini na walikuwa wanakwenda sehemu moja,katika maongezi walikuja kugundua kuwa wote ni wanandoa lakini kwakuwa walihitaji kulala mahali halafu kesho yake wafike walikokuwa wanakwenda walikubaliana kuburudika pamoja kwa usiku ule

Dada huyu akaniambia kuwa usiku ule ulikuwa ni wafaraja sana kwani "gem" alilopiga na jamaa lilikuwa balaa hadi huyu dada alitamani waendelee lakini kwa kuwa walikuwa wamekubaliana hata wasipeane mawasiliano ili kulinda ndoa zao hakuwa na jinsi

Dada anasema kuwa jamaa ni fundi sana na alikuwa kila akilala lazima kijindoto kipite,nilimuuliza kama kuna alichomzidi mumewe dada aliniambia kuwa karibu kila "engo" jamaa alimfunika mumewe kwenye suala zima la "gem"

Baada ya dada huyu na mwenzake kuondoka nilichukua muda kutafakari sana kama kunawezekana mtu akakutana kimwili na "mgeni" ambae hata hana hisia nae na akafurahia kabisa

Nimewahi kusikia kesi nyingi sana kuhusiana na "one night stand" na mabalaa yake kwenye kuvunja ndoa pale ambapo mtu anapoingia kwenye hatari ya kunogewa na kuliendeleza hata kwa kulazimisha,sijui hasa ni kunogewa au kunakuwa na kitu kingine hapo

Ninachojiuliza sana ni kama kuna uwezekano wa mtu kufurahia "one night stand" kwa kiasi hicho,binafsi siwezi kabisa na sijawahi kuwaza kuwa na hii kitu kwasababu mimi siwezi kufurahia faragha na mwanamke ambae sina hisia nae za upendo,kufikia hapo nikajiuliza labda huenda ni ushamba wangu wa kuwaza kizamani maana haya mambo ya one night stand hayapo kabisa kwenye mawazo yangu

Hivi uishawahi kuipata hii one night stand na ulihisi nini kipya au ndio mwishowe ni kujilaumu tu?

Hebu niambie,kwako inawezekana one night stand ikuwehushe kiasi hicho?
 
Hi topic ishaletwa humu siku chache zilizopita:

Naomba mods muunganishe huu uzi na ule mwingine............

Umezidi utoro na wewe Eiyer

Isije kuwa neno one night stand ndio limekufanya udhanie mada hii inazungumza kitu kile kile ambacho mada ile nyingine ilizungumza

Hebu nipe link ya hiyo mada ili nione!
 
Dah!!! Hivi, unalalaje na mtu hata humjui? (wakati mwingine hata majina hawatambulishani)..
..Kweli kuna watu wana mioyo minene...!

Ndio hapo sasa mkuu!
 
I had mchumba na pete kidoleni
katika tembea tembea nikajikwaa kwanye hilo jiwe la one night stand
nikaanguka chali ba' paroko

Ulipata wapi ujasiri wa kufanya hayo makitu na mtu ambae hata humjui?
 
Back
Top Bottom