Sister Abigail
JF-Expert Member
- Sep 2, 2020
- 4,814
- 14,927
Ujumbe mzuri
Unapoamua kuondoka eneo ulilozaliwa au lile lililokukuza, kurudi nyuma kifikra au kimtazamo ni kujirudisha kwenye lile koti la zamani ambalo tayari limeshakubana.Na ukiondoka eneo ulilozaliwa usiwaze kurudi nyuma tena yaani ni mbele mbele yao
Huruma iliyopitiliza kutoka kwa wazazi mara nyingi hugeuka kuwa "mtego wa dhahabu" (golden cage) unaomnyima mtu fursa ya kukomaa, kupambana, na kugundua uwezo wake kamili.Huruma unayopewa na wazazi wako ni kikwazo kikubwa san kwenye mafanikio yako.
sio rahisi lakin ukifanikisha hili utakua umefika mbali Sana ....Ondoka, ukakue, ukaongezeke!
Unapobaki katika mazingira uliyozaliwa, unakuwa unacheza mchezo ukiwa katikati ya watu wanaojua uwanja wako wote wa nyuma;Kwanza ulipozaliwa huwezi kufanikiwa maana unafuatiliwa kila hatua unayopiga maana wanakujua
Kwahiyo zitatumika mbinu zote ukiwemo hata uchawi kusimamisha juhudi zako au kukuzima kabisa
Kukubali kuhama kijiwe, iwe kifikra au physically ni gharama na inahitaji ujasiri. Nachukua mfano wa baadhi ya wadau, utakuta anaishi Kibaha lakini anasali Kijitonyama. Kule Kijitonyama anakoenda kuabudu kuna kitu cha ziada anachokifuata. Kinaweza kuwa kizuri au kibaya, ila kama ni mazoea basi ni hasara.
Wewe mbona hujahamia iran ili uongezeke?Duh..🥺🥺🥺🙌🏿
Mabibo ni irani tangu lini wewe kichaa?Ndiko niliko mbona
Kinachoendelea Tanzania sasa hivi ni kama kilichotokea kwenye nchi ya Kusadikika. Ma-CCM wa Kusadikika ya Shaaban Robert walikuwa na hoja kama za CCM ya sasa. Eti walikuwa wanasema umri wa mtu wa kuishi ni mfupi hivyo kujenga nyumba za kudumu ni hasara tupu. Eti unyayo wa mwanadamu hauzidi futi moja hivyo kujenga barabara hakuna faida. Eti magonjwa huja na kuondoka yenyewe, hayahitaji kujikinga wala kutibu.Shaaban Robert alilitilia mkazo sana jambo hili katika kitabu chake maarufu cha Kusadikika, hususan kupitia safari ya mhusika Karama, na pia katika mashairi yake mbalimbali yanayohimiza kutafuta maarifa na ridhiki ugenini.
Katika riwaya ya Kusadikika, nchi hiyo ilikuwa imefungwa na haikutaka raia wake wasafiri nje kujifunza mambo mapya. Karama anakuwa miongoni mwa wajumbe wanaokiuka mwiko huo na kusafiri nchi za nje (Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi) ili "kujaribu bahati" na kuleta maendeleo, akiamini kuwa kukaa mahali pamoja kunadumaza akili na maendeleo.
Falsafa ya Shaaban Robert kuhusu kusafiri ugenini na kujaribu bahati inajikita katika misingi hii mikuu:
Mwandishi huyu nguli aliamini kuwa "bahati" haimfuati mtu aliyekaa kiganjani, bali inamtafuta yule anayethubutu kupiga hatua na kuvuka mipaka aliyoizoea.
- Kupanua Maarifa na Busara: Aliamini kuwa mtu anayebaki kijijini au nchi kwake tu anakuwa na upeo mdogo wa kufikiri. Kusafiri ugenini kunamfanya mtu aone mifumo mipya ya maisha na kupata hekima mpya.
- Kutafuta Ridhiki na Fursa: Katika kazi zake, anasisitiza kuwa ardhi ya Mungu ni pana. Ikiwa fursa zimefungana nyumbani, ni wajibu wa binadamu mwenye nia ya kupiga hatua kutoka na kwenda kutafuta maisha kwingine, akitegemea juhudi na akili zake.
- Kujipima Uwezo: Ugenini hakuna kujuana wala kubebana; huko ndiko mtu anapokutana na uhalisia wa maisha na kujua kama ana uwezo wa kusimama mwenyewe bila msaada wa ndugu au mazoea ya nyumbani.
Mhusika Majivuno, ambaye ni Waziri Mkuu na kiongozi wa baraza la mawaziri, ana sifa ya dharau, kiburi, na kujiona kuwa serikali yake ina akili na haki kuliko mtu mwingine yeyote, tabia inayowakilisha baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa chama tawala (CCM) au serikali ya sasa ambao mara nyingi hukabili ukosoaji wa wananchi au wapinzani kwa kutumia kauli za kejeli na dharau badala ya kujibu kwa takwimu na hoja za msingi.Kinachoendelea Tanzania sasa hivi ni kama kilichotokea kwenye nchi ya Kusadikika. Ma-CCM wa Kusadikika ya Shaaban Robert walikuwa na hoja kama za CCM ya sasa. Eti walikuwa wanasema umri wa mtu wa kuishi ni mfupi hivyo kujenga nyumba za kudumu ni hasara tupu. Eti unyayo wa mwanadamu hauzidi futi moja hivyo kujenga barabara hakuna faida. Eti magonjwa huja na kuondoka yenyewe, hayahitaji kujikinga wala kutibu.