Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
Idara ya Usalama wa Taifa ilianza kuajiri vijana kutoka UVCCM tangu enzi za Jakaya Kikwete. Huyo mlinzi aliyetishia kumuua Zitto Kabwe ndio mfano wa vijana wa CCM waliopo ndani ya Usalama.
Anayesema huyo kijana ni Green Guard anapotosha. Ukweli ni kwamba kuna vijana wengi wa CCM ndani ya idara ya usalama wa Taifa, kwa ajili ya kufanyia kazi CCM. Hii inafanya idara kuwa chombo cha CCM, kwa maslahi ya CCM.
Mtu mmoja anadai eti, CCM kuingilia idara ya usalama haina maana idara yote ni CCM, zipo kazi nyingi zinafanywa kwa maslahi ya nchi.
Mimemwambia...Ukichukua usafi ukachanganya na Uchafu unapata Uchafu. Kwa kifupi idara ya usalama wa Taifa imechafuliwa kwa kuingiliwa na CCM, inatakiwa kusafishwa na kuundwa upya. Sehemu ndogo ya watu makini wasiofanya kazi kwa upendeleo wa kisiasa haitoshi kusema idara ipo sawa. Hata kuwe na ma-ghost wenye uwezo wa James Bond au Sherlock Holmes, kama uwezo huo unatumiwa zaidi kwa manufaa ya dola la CCM badala ya Nchi ya Tanzania...ni uchafu tu.
Chombo cha dola cha kutumainiwa ni Jeshi na taasisi zake. Angalau huko siasa hata ikiingizwa inaingizwa kwa woga na uangalifu mkubwa. Huku kwengineko... tusubiri miaka ijayo wenye akili watakaposhika dola.
Sent using Jamii Forums mobile app