Ona majina ya Wana-JF yanavyotengeneza habari

Ona majina ya Wana-JF yanavyotengeneza habari

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Posts
1,941
Reaction score
1,011
Nimejaribu kuanza kuandika visa habari kwa kutumia majina ya wana-JF. Tafadhali soma, angalia jina lako au la mwenzako lilivyitumika, furahi kisha nawe fanya mwendelezo.

Ni kama vile Sijali, na mimi nataka niwe MVUMBUZI. Ni baada ya kuwa Mfuatiliaji wa Jamiiforums, japo si MwanajamiiOne wala mkuuwakaya lakini ni Kiumbemwanadamu mtaratibuuuuuu.

Mimi mambo ya kumwagiana tindikalikali au kulishana MtamaMchungu na Mauza uza ya kuwa Invisible kama Jasusi, halafu Sometimes usiku wa Mbalamwezi anakuwa kama tototundu kuchukua inkosokaazi, UmkhontoweSizwe na ak47 kisha kupandia Kichuguu na kuwa Sniper sipendi. Sawa Ninaweza kufanya kama SILENT ACtOR au Msolopagazi na watu wakaniita Mndundu au Mtumishi Wetu lakini Wacha watu hatu kama ni watu8 wanione ni Mbangaizaji.

Najua Sikubaliki katika Yakuza kwani si Mr. Politician kama companero au MWANAKIjiji, wala si Polisi kama Chris Lukosi (japo alifukuzwa huko).

Mimi ni Mwafrika Halisi, MTAnzania Haswa yaani Mtanzania1, JituParaTupu, mwenye nguvu zaidi ya Yombayomba, wala si mwoga kama kautipe mpenda mchuzi wa kuku na kitumbua.

woyowoyo
!!
Mwenzenu ni mwelimishaji nafanyakazi za Mentor, si Mwalimu wala Profesa, ni Mkulima WAKUNJOMBE, (si wa Mtu wa Pwani kama maralia Sugu) nimelima Kinyungu na mashamba, najua Duduwasha na NG'OTIMBEBEDZU na msadapadasi.

Hivyo Son of Africa na daughter, Mzee Mzima, Mamndenyi, Kadada pamoja Sabry001 na kadhalika wote karibu kwa mwendelezo wa habari tusichoke.

Hii ni kama kucheza computer-words game.


Nyongeza:


rev Masanilo akiwa na Jipu mgongoni lilisababishwa Mbu Sugu, alitoka Kiguu na njia kwenda Igwachanya akiwa na ThinkPad yake. Njiani akakutana na The Boss, yule Mtafiti Makini rafikiye Researcher wa MORIA, akiwa na Tumaini Jipya la kupata ushauri toka kwa senetor huyu wa Kinyerezi. Loh! Kumbe amekosea The Boss (Kweli ni Dr wa ukweli) lakini ni mtoto wa mjini mwenye kiingereza kama cha Mwita Maranya au Kiranga. Yaliyomkuta rev Masa, hatakagi kusimulia. Akiwa ni Mtumiabusara aliondoka kama Mwendabure au Mkulima wa kuku. Mbele kidogo kwenye mtaa kama wa kwamtoro, kando ya Zagazaga kadhaa alikutana na Mnyamahodzo (mwenye Mlengo wa Kati) na chief-mkwawa, yule mtaalamu wa Tekelinalokujia). Akawasalimia, kinehe Mwadila! . wakamjibu, Mwadila baba! chief-mkwawa, akauliza, The Priest mbona uko kama MkimbizwaMbio? Akamjibu, ni The Boss yule rafikiye Pdidy. Mnyamahodzo akauliza, Pdidy yule mnywa Tusker Bariiiidi? rev Masa akajibu, huyohuyo, mpenda Ngambo Ngali. Hao watu, basi tu.
Basi pakawa na maongezi marefu kidogo juu ya maswahibu yaliyomkuta.

Ilipotimu saa kenda alasiri, waliwaona @St. Ivuga na Zing wakishuka kwenye magari wakiwa na vifaa kadhaa tayari kwa mkutano wa hadhara. Kwa mbali walikuwapo Watu wengi wakiwemo wakina faizafox, Preta na @Husinyo wakinywa supu ya SANGARA. Rev Masa akawafuata, kwa sauti ya chini aliwaambia @M'hodzo na Chief, sasa ni Babylon. Mnyamahodzo alijipiga kifua na kusema, The last don. Ndipo Rev Masa kwa sauti kavu kavu akaanza kuhutubia " Hii ni SaHaRa Voice, Voice of Reason yenye kuleta TUMAINI. Habari za goodgud ambaye ni invicible na @Yumwema.
....Niliye mbele yenu si MpitaNjia, naipenda tanzania,....hata kama mkitaka niwe raisi wa paka..." mara likasikika sauti ya mabomu booom!!
 
Last edited by a moderator:
Ni article nzuri lakini kama ungetaka watu wajue jinsi ulivooanisha hadith yako na majina ya wan Jf ungetumia angalau rangi katika majina hayo
 
Umetisha japo jina langu halijatengeneza habari yako.
 
Hahahaahahaahaaa imesomeka uzuri saaaana, tumepunguza stress kidogo
 
.....aisee hiko vizuri, ila sijui kwa jina ninalo tumia mimi kama linaweza kupata nafasi kwenye article yako kwani kwa hakika naamini ni vigumu kulitafutia kiunganishi.
 
ungewa tag hao uliowataja ili tujue ID ni zipi, but good creativity dude.
 
Usingekuwa na haraka....ungekopy majina yao na kupaste kwenye thread yako,,ingekuwa njema sana...wahusika wangepata ujumbe kwa urahisi....anyway umejitahidi...
 
Selemani alisema ..kutajataja majina tena kwa mistari isiyo na vina, kisha mnaleta utani..

Bei mbaya nilitegemea maajabu kwenye uzi wako hola
 
mikazó;8576893 said:
Mbna jina langu halipo hapo

kwa sababu wakati anaandika ulikuwa na Mikazo ya tumbo itabidi Nyaningabu aliyepo mbugani Katavi akuchimbie Mzizi mkavu uchemshe unywe! Ingawa nae huko porini nasikia ametekwa na kakajambaz ambaye nyumbani kwake anafuga kina pakajimi wengi. Kwa kuwa mimi ni kamanda,nitatuma Swat team huko ikamuokoe ili upate dawa ya tumbo!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom