On Star TV: Tuongee Asubuhi Kupitia JF - Umri wa wagombea Urais

Umri unahusika sana kwangu lazima afikishe miaka zaidi ya 45,tukiwapa hawa watoto wa dotcom kuna siku wataleta disco ikulu na kuweka kiingilio getini pale.

mkuu umri hauna tija kwa taifa hili.................... mbona kiongozi wako ana umri mkubwa lakini anafanya mambo ya kitoto?
 
Umri si kigezo cha mtu kuwa rais, wale wote wanaozungumzia umri ni wale wny tamaa na madaraka, ila tanzania tunahitaj rais anayeweza kutuvusha hapa tulipo na kuelekea nch ya ahad kwahiyo haijalsh rais ni kijana au mzee..
 
Mkuu Yahya, asante sana kwa mjadala huu, kule kwa Mzee Mwanakijiji, nilijibu hivi:
Mkuu Mzee Mwanakijiji, nakuunga mkono kwa asilimia 100 % ndio maana sifa kuu za wale wagombea wangu wawili kijana ZZK na Mzee EL ni uwezo!. Hivyo kwa muktadha huu, kabla hatujaangalia uwezo, first lets remove the "red tape"ya kigezo cha umri, tena sio tuu kushusha umri wa kugombea urais, bali pia tushushe "the age of majority" kutoka miaka 18 hadi miaka 16 au 15!.

Kama umri wa mwisho wa mtoto ni under 14, then kuanzia umri wa miaka 15 ni mkubwa na hata sheria yetu ya ndoa inalitambua hilo kuwa binti wa kuanzia miaka 15 anaweza kuolewa! (kwa ridhaa ya wazazi wake).

Natoa wito tuungane kuhakikisha kwanza hii "red tape" inakuwa removed, ndipo sasa tutafute sifa, vigezo na uwezo!.
Pasco.
 
Tanzania inatakiwa Iongozwe na kizazi kipya. Kizazi kilichotuletea uhuru kiondoke kwani mawazo yao yamebobea kwenye misaada, kuamini zaidi watu wa nje na kushindwa kuwezesha vijana wa kitanzania kufanya yale ambayo wageni wanayafanya hasa yale ya kisayansi.
 
Swala la umri wa kiongozi hasa ngazi ya uraisi ni muhimu sana kujadili, kizazi kilichopita (viongozi wa sasa) wanabaki kuadili walikotutoa, utasikia tumeleta uhuru na wakasahau kuhangaikia matatizo yetu kwa sasa, matatizo yetu kwa sasa si ukoloni wa zamani tunahitaji vijana watakao ondoa ukoloni mamboleo, watatuletea maendeleo yetu wenyewe.

Pia viongozi wazee/wenye rika kubwa wanaongeza tatizo la ajira, kwani vijana wenye uwezo wapo wanaweza fanya kwa ufanisi lakin eti kwa sababu ya umri wao hawafai wakati wanahangaika mitaani kutafuta ajira, kwa mfano ukuu wa mikoa, wilaya na nafasi nyingine.
 
Tunawajenga watu wafikie ambition zao za kuwa marais bila kujijua.

Huu mjadala wa umri kwa sasa hauna tija kwa taifa kwakuwa umegeuka kuwalenga watu fulani fulani badala ya kuweka mazingira ya jumla kwa mtu yeyote mwenye sifa kutuongoza.
 
Mpaka sasa, Dr. Ayoub Rioba na Dr. Bana, wote wanasupport kuondolewa kwa red tape ya miaka 40!. Katiba ijayo hiki kipengele kandamizi na baguzi kitaondolewa!, vijana washindwe wenyewe!.
 
Tunawajenga watu wafikie ambition zao za kuwa maraisi bila kujijua.
Huu mjadala wa umri kwa sasa hauna tija kwa taifa kwakuwa umegeuka kuwalenga watu fulani fulani badala ya kuweka mazingira ya jumla kwa mtu yeyote mwenye sifa kutuongoza.
Mkuu Mwita Maranya, na wewe umeingia choo cha kike kwa kudhani lengo la kushusha umri ni ili kwa ajili ya kum accomodate kijana fulani simply because fulani alishaonyesha ambition?!.
P.
 
Urais sio kliniki wala kambi ya kutunza wazee.

Kama kuna anayefikiri umri wake ni kigezo cha kuwa rais wa Tanzania huyo ni wakuogopwa kama ukoma.

Kwa nini lijadiliwe sasa? Nafikiri ni kwa sababu kuna watoto wanataka urais.

Mimi nashauri kama waganga wao wamewaambia ni lazima wawe marais tanzania basi hajakosa kabisa kwani kuna rais wa BOXING UNION OF TANZANIA, TPDC, TFF, NK.

Dk Bana naomba usituangushe leo maana na wewe hutabiriki.
Mkuu.
Umeweka sawasawa kisu kwenye mfupa.
 
Kuna watu wana ndoto ya kufunga ndoa ikulu. Haya mawazo ya ajabu sana kuwa nayo na ndio dalili ya utoto wenyewe
 
tanzania inatakiwa iongozwe na kizazi kipya. Kizazi kilichotuletea uhuru kiondoke kwani mawazo yao yamebobea kwenye misaada, kuamini zaidi watu wa nje na kushindwa kuwezesha vijana wa kitanzania kufanya yale ambayo wageni wanayafanya hasa yale ya kisayansi.

kakende haya unayoyasema si ya kuingiza kwenye katiba tunataka katiba ya miaka 50 ijayo.
Haya unayoyasema ni mambo ya kama miaka 10 kwa hiyo haya unatakiwa kuyaleta kwenye kampeni 2015 ili tuwaondoe walioshindwa na si wazee.
 
Hii ishu ya kujadili umri wa kugombea urais ilitokana na zitto kuutaka urais. Kwani 2015 zitto atakuwa na umri gani?

Hata hivyo katiba itatakiwa ifanyiwe marekebisho kutokana na hali ya maisha ya mtanzania. manake tunaambiwa life expectancy ya mtanzania ni miaka 45, ikizidi ni miaka 52.

Sasa masharti ya mgombea urais sharti kuwa na miaka 40 inatuletea utata, manake tunaweza kujikuta tunaongozwa na rais miaka mitano halafu anakufa akiwa ameongoza kwa kipindi kimoja tu.
Kwani wenye miaka chini ya 40 hawafi Mkuu? Mimi ninachojua life expectancy ni average ndio maana wengine wanakufa na miaka mitano wakati kina Mzee Kingunge bado wanachapa mwendo. Hoja ya kushusha umri kuwa chini ya 40 haina maana kama hatujaweka umri maximum. Wanaotaka umri upunguzwe wana maslahi binafsi
 
Nchi kama Japani, China, Indonesi, Malasia, Singapore, India, Irani na zinginezo, ikwemo Brazil na Hata Ghana na Botswana kwa Africa hazijawahi kuongozwa na Vijana lakini ziko Mbali sana kiuchumi, hawa wakian Zito na January wanatafuta Umaarufu tu
 
swala la umri wa kiongozi hasa ngazi ya uraisi ni muhimu sana kujadili, kizazi kilichopita (viongozi wa sasa) wanabaki kuadili walikotutoa, utasikia tumeleta uhuru na wakasahau kuhangaikia matatizo yetu kwa sasa, matatizo yetu kwa sasa si ukoloni wa zamani tunahitaji vijana watakao ondoa ukoloni mamboleo, watatuletea maendeleo yetu wenyewe.

Pia viongozi wazee/wenye rika kubwa wanaongeza tatizo la ajira, kwani vijana wenye uwezo wapo wanaweza fanya kwa ufanisi lakin eti kwa sababu ya umri wao hawafai wakati wanahangaika mitaani kutafuta ajira, kwa mfano ukuu wa mikoa, wilaya na nafasi nyingine.

kaka na wewe huna tofauti na hao unaowaita wazee,katiba ni miaka 50.
Kuwaondoa walioshindwa ni sula la miaka mitano mitano kwa hiyo tusubirie kampeni,
 
Mkuu Mwita Maranya, na wewe umeingia choo cha kike kwa kudhani lengo la kushusha umri ni ili kwa ajili ya kum accomodate kijana fulani simply because fulani alishaonyesha ambition?!.
P.
Pasco!
Unataka kutuambia hujajua kwamba champion wa hii kitu ametangaza nia kugombea Urais na ametamka wazi kwamba watu waliozaliwa baada ya 1961 hawafai kugombea Urais?. Unaposema lengo la kushusha umri sijajua nanai ana lengo hilo zaidi ya wale waliotangaza nia na wafuasi wao?
 
Last edited by a moderator:
tusiendeshwe na tamaa za hawa wa Utatu muovuJussa , makamba,Zitto.Wapo kwenye ndoto, kuwa wakipata watajenga super union,ya vyama na pande mbili za nchi.Na hivyo si ajabu wakawa hata wamegawana nafasi ya urais
 
-Sidhani kama matatizo ya uongozi tuliyo nayo kama taifa yana uhusiano na Umri tu

-Nimekua nikipigania hii hoja ya vijana wenye uwezo,uzalendo na uadilifu wanafaa kutuongoza.Lakini hoja hapa ni uwezo na uadilifu kwanza

-Kwa bahati mbaya watu wanaweka umri kama kigezo cha ubaguzi.Tukimaliza ubaguzi wa umri sasa tutasema watoto wa viongozi ambao walishindwa hawafai kutuongoza kwa kuwa baba zao walishindwa.Tutakua tunaelekea wapi?

-Kwa sasa hivi succession plan iandaliwe.Hili ni tatizo la kimfumo
.
Mkuu Ben,
Umezungumzia jambo moja muhimu sana la "succession plan". Nilipokutana na Dr. Slaa
 
Urais ni dhamana kubwa kabisa kiasi haifai kukurupuka. Tuwaogope sana vijana ambao wanatamani kuipata nafasi hii kwa kubadili katiba hususani kwa kigezo cha umri. Hatuwezi kamwe Watanzania kumkabidhi nchi kijana wa umri chini ya miaka ya 40.

Sisi wote ni mashahidi tumeshuhudia vijana wakiwa vigeugeu na hata wakati mwingine ni wepesi kurubunika. Tuache umri uliwekwa kipindi cha nyuma uendelee.

Leo tumesema miaka 40 kesho akitokea mwenye miaka 25 akawa na hamu ya urais naye atataka tubadili katiba kwa kigezo cha utashi wake.
 
Habari za Asubuhi wadau, Jumapili ya leo tunajadili mada ya mdau Mzee Mwanakijiji kuhusu suala la kuufunga mjadala wa Urais tukiilinganisha na Mawazo ya Mhadhiri Dr. Ayoub Rioba anayeutazama mjadala wa umri wa urais kama Mjadala uliopoa Njia. Makala hiyo ilichapishwa na Gazeti la Mwanahalisi.


Wakuu hiyo kifaa hapo kwenye red imerudi mtaani? Ha ha ha ha ha! Mbona kimya kimya?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom