On Magufuli na Odinga: CHADEMA wapo sawa!

MOds Unganisha hii thread na hii hapa iliyotolewa Desemba,7 .Uzuri mkutano wa ODM/CORD ulirushwa Live na Citizen,Nationtv na Magufuli alitoa mbwembwe nyingi sana, na MC alimtambulisha kama muwakilishi wa CCM na siyo Serikali na ndiyo maana mimi nikiweka mada hiyo.
[h=2]CCM ya Muunga Mkono Raila Odinga Urais Kenya ,Yawakilishwa na Magufuli Mkutano wa Uteuzi[/h]
 
Wewe ni mngonjwa kweli hujui kuwa Maghufuli ni waziri wa serikali ya Tanzania tamko la Maghufuli ni tamko la serikali kama sio CCM athari zake ni kubwa, hebu fikiria endapo Serikali ya Kenya ikachukuliwa na Uhuru Kenyeta je Tanzania tutaficha wapi soni zetu, ua unataka kujenga uadui na jirani zetu???

 

Kwahiyo huko hotelini alikuwa akiifanyia CDM kampeni ya uchaguzi upi?? hapa tunaongelea suala la Waziri wa Tanzania kupanda kwenye jukwaa na kumpigia debe mgombea wa nchi nyingine. Hapo lazima ukubali kuwa kuna maswali mengi magumu yanayohitaji majibu sahihi na sio utetezi huu wa kitoto
 

Hapo kwenye red; kama kweli ndilo lilikuwa lengo la safari yao (kuungwa mkono na SERIKALI YA KIGENI) hilo ni kosa kubwa na serikali yetu kama ILIUNGA MKONO itakuwa imefanya kosa kubwa. Si ajabu Odinga na ODM wana haki ya kutafuta upande wa kuwaunga mkono kutoka TZ baada ya kuona wapinzani wao wanaungwa mkono na serikali yetu.

Hii peke yake inaanza kuleta msuguano baina ya nchi jirani; imagine Odinga akishinda uchaguzi itakuwaje? EA Community itakuwa imefikia mwisho. Au baada ya serikali na CCM kuona wamebugi step kuwaunga mkono akina Ruto wakaona wa-neutralize kwa kumtuma Magufuli kwa Odinga? May be this is the case.

Hapo kwenye
navy; kila nchi ina sheria na taratibu zake. Si ajabu Malawi na kwingineko wanasiasa au viongozi wa kiserikali kutafuta au kutoa support za kisiasa wanasiasa wa kigeni inaruhusiwa; japo ni nchi chache mno zinaweza kuwa na utaratibu huo.

Kumbuka Komba sio kiongozi wa kiserikali zaidi ya kuwa "mpiga filimbi" wa CCM ambaye walimtumia kum-support rafiki yao Bakili Muluzi. Hata kwa hili dogo (la Komba na TOT) baada ya Muluzi kuondoka madarakani, je, unaona matokeo yake? Kinachoendelea hapo Ziwa Nyasa nadhani wote tunakifahamu; kwa nini tusiamini kina uhusiano na mambo haya ya kuingilia siasa za ng'ambo?

Hata Marekani inapotaka kuingilia siasa za kigeni hutafuta "kuungwa mkono" na jamii ya kimataifa kabla ya kufanya hivyo; sisi tunaingia kichwa kichwa na "umasikini" wetu.

ALL in ALL, sio sahihi sisi kutuma au kualika VIONGOZI WA KISERIKALI kwenda au kutoka ng'ambo kwa ajili ya masuala ya kisiasa na hasa inapokuwa ni siasa za majukwaani. Imagine umwone Kagame au Museveni jukwaani akimnadi mgombea wa CCM. Hii ni hatari!
 

- Tunaishi kwa kuongozwa na Sheria za Jamhuri, Magufuli ni Waziri Masaa 24/7, kwenda kwake kwenye kampeni za siasa za Taiafa lingine kunatakiwa kutolewa maelezo ya kina na Chama chake in this case CCM, angeuliwa akiwa huko unafikiri ni familia yake tu ndio ingehitaji maelezo kutoka Serikali ya Kenya? Au Taifa zima la Tanzania lingehitaji maelezo?

- Mengine muwe mnatumia akili kidogo tu kuliko Uchama kipofu na ishu kama hizi ndio sometimes zinakuwa ni abuse of power!!

Es!
 

- Unajua I thank God kwamba nina msimamo so huwa sisumbuliwi na hizi, wewe unasema Few Years back na wengine wamesema Few Years back nilikuwa Chadema, unaona the contradiction? Ndio maana huwa siawasikilizi sana ninasimama na what I stand for, in this case kama hakuna maelezo ya kutosha kutoka kwetu CCM, automatically inakuwa ni Abuse of power nitamtafuta Kinana mimi mwenyewe on this!

Es!
 

Kimantiki mwanzoni nilidhani viongozi wa kisiasa na kiserikali kuonana kikazi na wenzao wa nje si tataizo bali tatizo ni kushiriki katika kampeni za kisiasa za nchi nyingine wakati wa uchaguzi tena kwa uwazi.

serikali nyingi na vyama vya kisiasa vingi vina wagombea wanaowaunga mkono nje ya nchi lakini si kwa uwazi bali kisirisiri.
 
Lakini pia tuvuke mipaka zaidi tusiangalie kisiasa tu lakini pia tuangalie kijasusi!!!!!!!!!!!

Kama Taarifa za kijasusi zinaonyesha kuwa Tanzania itakuwa salama chini ya Odinga ni sahihi kwa serikali yetu kuwa na mgombea tunayemuunga mkono katika uchaguzi wa Kenya. Tatizo ni ujasusi huo kutumia mbinu za wazi kwenye kampeni za siasa za Kenya.
 
- Kiboko cha nani? Taifa tunawalipa kutusaidia CCM na this is one of their responsibility, unamsifia mtu kwa kufanya wajibu wake?

Es!


Kwa hiyo msha jiharalisha kuwa ni watawala wa nchi hii siyo??

Tatizo lenu nyie watoto wa vigogo mnafikiri CCM itatawala milele na ndiyo maana wazazi wenu wako busy kuwalithisha vyeo.................. Yana MWISHO haya................... Tafuteni ushauri kwa KABURU South, maana walikuwa na mawazo kama yenu!!!
 
nashukuru kwa ufafanuzi mkuu.kwa hiyo ccm ipo upande wa raila odinga!
Nape njoo utupe ukweli basi!
 

Endapo ni kweli Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyau alimuunga mkono Romney dhidi ya Obama na baadaye Obama aliposhinda wameendelea kushirikiana basi hii inaonyesha kuwa wenzetu wamekomaa nimesikia Netanyau akimpongeza Obama kwa kumuunga mkono katika suala la Wapalestina. Lakini pia tuliwahi kushuhudia katika uchaguzi wa kwanza na wa mbili aliyekuwa waziri wa Mambo za nje wa Marekani Collin Poweri (republican) akimuunga mkono Obama wa chama cha Demokratic
 
Hili swala kama hawataki kujibu kwa utaratibu naona CDM kupitia wabunge wake akiwamo Mhe Wenje walipeleke swala hili bungeni majibu yatapatikana hukohuko!!!!

 

Hii point yako ya mwisho nakubaliana na wewe kabisa. Sasa nini cha kufanya, ni kwamba inatakiwa wabunge watunge sheria kali dhidi ya chama chochote kitakachofanya hivyo. Lakini kuanza kuwashambulia watu selectively sidhani kama ni sahihi. Kwa sababu watu wa pande zote upinzani na chama tawala wamekuwa wakijinasibu sana na washirika wao wa nje.
 
Mkuu,
Tanzania under CCM ki-vitendo hakuna mipaka ya uongozi ndiyo maana siyo ajabu hata wananchi wasio makini wanashindwa kutofautisha kati ya utendaji wa vyama na serikali.

CCM wangeweza kutofautisha hilo ingewasaidia sana, haya mambo ya chama kushindwa kukemea watumishi wa serikali wanaoboronga ndio inawaharibia. Kama chama kingekuwa kinaisimamia serikali kingeweza kujitenga na kashfa nyingi za ufisadi maana umetokea serikalini lakini kutetea makada wake kunakigharimu na hakiwezi kujitenga na uchafu huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…