Kiwi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 1,054
- 990
Heshima kwenu wanajamvi,
Nina ombi ama rai ambayo ningependa ifanyiwe utafiti na ikiwezekana iwekwe kwenye historia ya mapambano yetu ya ukombozi.
Ninapendekeza CHADEMA iweke siku maalum kwenye kalenda zetu, iwe siku ya kuwakumbuka wote wale waliopoteza maisha yao kwenye harakati za kumkomboa maskini wa Tanzania kutoka kwenye makucha ya wakoloni hawa weusi wadhalimu wanaotuangamiza kila kukicha. Ni wazo tu naomba muwe huru kulijadili na hata kuliacha kama mnaona halina tija. Ili kufanikisha hili ningeomba iwekwe orodha ya wote waliotangulia mbele ya haki na kama inawezekana hata picha zao na historia fupi za maisha yao. Tunao wengi, na kwa jinsi serikali yetu inavyoendelea kubanwa na badala ya kutafuta ufumbuzi inavyoendeleza vitisho na ubabe ninafikiri bado hatujafika mwisho wa safari yetu, ingawa tunakaribia...
Wapumzike kwa Amani mashujaa wetu! Tunaweza kuapa tu ya kuwa tutawaenzi, na damu yao itakuwa chachu itakayoongeza vuguvugu la mabadiliko katika nchi yetu!