Ombi maalumu kwa Rais Magufuli juu ya Nape, Polepole na Makongoro Nyerere

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,184
2,000
Mkuu wa nchi yangu na mwenyekiti wa chama dume africa nzima, kwanza naupongeza uongozi wako uliotukuka,

Mheshimiwa kupitia maoni ya watu mbali mbali kutoka kwa watu kwanza wanakukubali kwamba ni jembe kali mno,

Mkuu watu wana maombi matatu muhimu

1.Kuhusu Nape Nnauye

Mkuu wa nchi pamoja na mapungufu ya kibinadamu aliyonayo bwana Nape Nnauye lakin ana mazuri yake , tu najua kila binadamu ana mapungufu yake lakin tunakuomba umsamehe Nape na kumpa angalau kazi ndani ya chama , Anaweza kuwa katibu mkuu mzuri ambaye naona anaweza kukaribia viatu vya Kinana,

Kwanini Nape awe katibu mkuu?

A.Anaijua ccm kiundani na anajua kazi za chama kisiasa,
B.Kasi yake ni kubwa mno kiutendaji
C. Amepikwa vizuri na mzee kinana na ziara nyingine wamekuwa wote akiwa mwenezi,
D. Hana kashfa ya rushwa anachukia Rushwa toka moyoni,


2. Humphrey Pole pole
Mheshimiwa rais bwana pole pole hamkumtendea haki kumpa uenezi ,yeye kazi ya uenezi haiwezi , humphrey ni mtu wa facts na.ukweli wakati uenezi unahitaji propaganda zaid ya ukweli, na rafu za s siasa haziwezi pole pole,

Kazi inayomfaa pole pole ni ukatibu, ubalozi, au kazi nyingine kama uratibu au ukuu wa wilaya ni kijana mzuri katika mazingira yanayohitaji fikra pevu za ukweli mtupu na facts,
Naomba umfikilie katika ubalozi au kazi nyingine, lakin si unenezi siasa za rafu na propaganda haziwezi,
Nafasi yake izibwe na livingstone lusinde mbunge au Magoiga SN anaweza sana au kuna jamaa anaitwa raia mpenda haki,

3. Makongoro Nyerere
Huyu kaka kakupigania sana wakati ukipiga kampeni na kazi anaiweza tunaomba umpe kazi akusaidie katika gurudumu la maendeleo,

Hakuna ambaye hajui uwezo wake na usmart wake,

Mheshimiwa nawakilisha
 

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
6,919
2,000
Polepole hataki KATIBA MPYA tena eti sasa anataka UKATIBA hahahahah, Sasa huo UKATIBA utakuwepo bila ya kuwepo kwa kitu mlichokubaliana kama Taifa kuwa hiki ndicho KATIBA?.

By the way nimetafuta msamiati " UKATIBA" kwenye kamusi ya kiswahili fasaha lakini halimo!, huu ni ushahidi wa wazi kuwa Polepole anajiundia maneno yake mwenyewe na kutuaminisha kuwa ni kiswahili wakati siyo!!
 

mkwawa complex

Senior Member
Dec 15, 2016
184
250
KUMPENDEKEKEZA L/LUSINDE KWA NAFASI YA UKATIBU MWENEZI,HAPO UMECHEMKA.HIYO NAFASI INAHITAJI PROPAGANDA LAKINI LAKINI KWA UMAKINI NA AKILI NYINGI(WATANZANIA WA SASA WAMEELIMIKA).LUSINDE ANATUMIA NGUVU NYINGI BILA MAARIFA.
 

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,274
2,000
KUMPENDEKEKEZA L/LUSINDE KWA NAFASI YA UKATIBU MWENEZI,HAPO UMECHEMKA.HIYO NAFASI INAHITAJI PROPAGANDA LAKINI LAKINI KWA UMAKINI NA AKILI NYINGI(WATANZANIA WA SASA WAMEELIMIKA).LUSINDE ANATUMIA NGUVU NYINGI BILA MAARIFA.
Nguvu nyingi bila maarifa...nilidhani hiyo ndio sera mpya ya CCM. Fikiria risasi 38 kumtoa uhai mzalendo moja tu anayeitwa Mh. Tundu Antiphas Lissu! Watu kama Lusinde ndio hazina ya CCM ya awamu hii...akili kidogo lakini ubabe ubabe mtindo moja. Slow slow bahati mbaya hana ubabe na akili yenyewe mwendo wa kono kono ya kubabaisha bila busara..
 

jabulani

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
4,285
2,000
Nape ni jembe kwenye kampeni atatufaa sana chadema. Vingunge wanaochukizwa na ccm hawatahama kwa pamoja watakuja mmoja mmoja kimkakati.
 

NAREI

JF-Expert Member
Mar 10, 2017
1,700
2,000
chakubanga(pole pole) abaki kwenye nafasi yake ili 2020 alete vifact vyake uchwara CHADEMA tuweze kumnyonyoa vizuri.

NAPE tutamsajili na atakuwa katibu mwenezi wa CHADEMA 2020.
Ukatibu wenezi mkimmpa nape halafu makene awe ana lamba viatu vya lowasa kwenye kampeni.
 

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,752
2,000
chakubanga(pole pole) abaki kwenye nafasi yake ili 2020 alete vifact vyake uchwara CHADEMA tuweze kumnyonyoa vizuri.

NAPE tutamsajili na atakuwa katibu mwenezi wa CHADEMA 2020.
Nape kwa kweli ni kifaa sana .
Namkubali sana .
Ni mkweli, jasiri, muwazi na mpenda haki.

Kwa sasa ndani ya CCM hakuna kijana wa enzi ya sasa wa kulinganishwa na Nape enzi zake akiwa UVCM.
Ni jembe kweli kweli. Siasa anaijua sana na msomi pia.

Kutoka Moyoni hua namiubali sana Nape. Hana kinyongo cha kisiasa zaidi ya kuhubiri kile anachokiamini na kukataa kwa nguvu zote kila asichokiamini.
Huyu kada halisi wa imani ya CCM ile ya mwaka 1977.

CHADEMA wakifanikiwa kumsajili huyu kada kwa kweli watakuwa wamebakiza usajili mdogo wa baadhi ya wanasiasa ndani ya CCM ili ikamilishe usajili na kusubiri kifo cha CCM kati ya 2020 na 2025.

Ni bora CCM ikafia 2020 mana bado itakua na watu wa kuizika lakini ikilazimusha kusogeza mbele siku zake za kufa mpaka 2025 basi wakati huo haitapata hata mtu wa kuhudhuria kwenye mwisho wake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom