Ombi maalumu kwa Mheshimiwa Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi maalumu kwa Mheshimiwa Kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwafrika wa Kike, Mar 4, 2008.

 1. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Jakaya Kikwete,

  Hongera sana kwa kuteuliwa kuwa kiongozi wa muungano wa Afrika kwa kipindi kijacho. Hongera pia kwa kufanikisha upatikanaji wa amani kwa majirani zetu Kenya. Hongera pia kwa kumualika raisi wa Marekani George Bush kutembelea Tanzania. Hongera pia kwa net za mbu ambazo Bush ametoa kwa watanzania. Hongera pia kwa kumtoa Mramba kwenye Baraza lako la mawaziri.

  Pamoja na hongera na sifa zote hizi, pamoja na email zangu zote zilizopita ambazo nimekuwa nakuandikia (ingawa nimekuwa sipati majibu toka kwako au kwa wasaidizi wako), nimeamua kukuandikia hii email nyingine ambayo pia nitaiweka kwenye mtandao mtukufu wa JF (kama ushahidi) kama ombi maalumu kwako kushughulikia hili suala la bei ya umeme.

  Mheshimiwa Kikwete, inawezekana kuwa huna taarifa ya hili ila ni kweli kuwa bei ya umeme imekuwa juu sana kiasi kwamba hali ya maisha ya watu inazidi kuharibika na kuelekea kwenye matatizo makubwa kifedha. Bei ya umeme kwa wastani kwa wengi wa wakazi wa Dar es salaam ni zaidi ya asilimia 50 ya kipato chao cha mwezi. Hii ni hatari sana hasa inapowafikisha wananchi kwenye mjadala wa kuamua kama wanunue chakula au walipie gharama za umeme.

  Baadhi ya washauri wako wa uchumi wamesingizia sera za soko huria kama kigezo cha kutoingilia kati suala la umeme, na bei ya mafuta, sementi, usafiri nk. Naomba nikuhakikishie (kama kweli hukujua hili) kuwa hata hapa Marekani, rafiki yako Joji imebidi aingilie kati suala la mortgages baada ya kuona kuwa uchumi wa nchi unaporomoka na mabenki yanafilisika. Kuna wakati ambao inabidi serikali iingilie kati biashara binafsi ili kunusuru maisha ya wananchi wake wa kawaida.

  Safari yangu niliyofanya Tanzania mwezi december, niligundua kuwa hata dawa ya mswaki ni ghali Tanzania ambako bei ya kufanya kazi ni rahisi kuliko marekani (dola 6 vs dola 2). Sitakuuliza kuwa uingilie kati ili kushusha bei ya dawa ya mswaki au dawa ya sementi, mafuta, usafiri nk. Lakini mheshimiwa Raisi, kwa vile bado uzalishaji na usambazaji wa umeme uko chini ya serikali, ni vizuri ukaingilia kati na kuwaokoa wananchi wako na hii dhahama.

  Bado sijui kwa nini serikali inayalipa makampuni ya IPTL, Kiwira, Richmond na Dowans, Songas, nk mapesa yote haya kuzalisha umeme na bado unakuwa ghali hivi (kuna taarifa kuwa haya yote yanalipwa wakati hayazalishi chochote). Naomba pia nikukumbushe kuwa rafiki ya Joji na serikali yake wanakatisha mikataba ya makampuni mbalimbali na serikali (mfano boeing na contract yake ya kutengeneza ndege za kijeshi nk) kila mara inapogundulika matatizo katika mikataba na utekelezaji wake.

  Chondechonde Kikwete, najua kuna mengi huwezi kufanya lakini hili la umeme ni muhimu sana kwa maslahi ya watanzania wengi.

  Asante sana!
   
 2. M

  Masaka JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 437
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wengine nao kwa kutaka sifa za bure. Wewe matatizo ya umeme Kikwete ameyakuta na unataka afanye nini sasa. Unamtaka Raisi wa nchi aingilie hata upangaji wa bei ya umeme? Kisha kesho utasema kuwa apunguze bei ya bia au nini? Hata ukijifanya kutumia lugha ya heshima hutasikilizwa na pumba zako hapa!
   
 3. B

  Binti Maria Senior Member

  #3
  Mar 4, 2008
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Sasa hapa mwenye pumba ni nani? Yaani wewe unaona umeme sio tatizo kubwa halafu bado unafikiri una akili?! Watu kama nyie mnahitaji elimu maalumu ya uraia, tena wewe unahitaji one to one tuition kuhusu elimu ya siasa maana inaonekana una matatizo sio madogo!
   
 4. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2008
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Tulimchagua ili atatue matatizo yaliyokuwapo wakati ule tukitegemea yeye ndiyo mkombozi. sasa kama hawezi kuyashughulikia kwa sababu aliyakuta then lazima kuwepo maswali mengi na iwapo tu wewe ndiye msemaji wake.

  Suala la umeme kama lilivyo la Mafuta ama kwa ujumla wake NISHATI ndiyo eneo nyeti sana linalogusa maisha yetu ya kila siku kupitia mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali na ndiyo maana Mwafrika wa kike ametuma ombi maalum kwa Rais. sasa inawezekana Rais akaona pumba au akaona kuna Hoja kwenye hiyo email hiyo ni juu yake mwenyewe.
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wewe ndo una pumba tupu, tena za mtama, zisizofaa kuandikwa hata katika magazeti ya Uhuru na Mzalendo.

  Umeme ni jambo very Sensitive katika nchi yeyote linalogusa kila sekta ya uzalishaji.

  Rais Kikwete akitatua tatizo la umeme hakutakuwa na haja ya kuingilia kati bei za bidhaa nyingine.
  Tatizo lako ni kwamba unayaona mambo katika umoja na upekee wake.
  Kwako nauli ya dala dala haina uhusiano na bei ya umeme.
  Bei ya nyanya sokoni tandale pia haina uhusiano na bei ya umeme.


  Acha kuishi kwa mafungu ndugu yangu, maisha ambayo viongozi wengi wa SISIEMU wanaishi.

  Tumia akili yako kufikiri na kutafakari mambo kuliko kukurupuka na kujadiri hoja kwa mazoea au kwa kutumia vichwa vya watu wengine.
   
 6. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sasa kama Rais wa nchi hausiki na matatizo ya wananchi kama bei ya umeme, unategemea kazi yake itakuwa ipi? Ni vyema ungesoma hoja kwanza kuona kama kuna cha maana kuliko kuhangaika na nani ameandika hoja hii ndugu yangu!
   
 7. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Njia rahisi ya ktekeleza hili ombi sio lazima kuibana TANESCO ipunguze bei bali ni kwa serikali kutoa ruzuku ambayo itaingia moja kwa moja TANESCO. Hili linawezekana iwapo mikataba yote ya makampuni ya kuzalisha umeme yaliyoingia na TANESCO itafanyiwa tathmini na kurekebishwa/kuvunjwa. Pia zile pesa za mafisadi nadhani zinaweza kusaidia kidogo. Ni maoni yangu tu, I stand to be corrected! Nawasilisha hoja.
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #8
  Mar 5, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,426
  Trophy Points: 280
  sioni tatizo kwa email ya mwanamama mwafrika...ila jibu ulilotoa MASAKA ..linatoa picha ya wasaidizi WAKIRITIMBA wa rais ..amabao wanalipiwa umeme pale kwenye vibanda vya mbwa magogoni au knyama...na wala hawajui kama tanzania kuna LUKU.....

  masaka ameshindwa kuelewa DHAMIRA..Ya barua kuwa ni moja..INFLATION RATE NI KUBWA KUTOKANA NA TATIZO LA GHARAMA ZA UMEME KUBWA ZINAZOTOKANA NA MIKATABA MIBOVU..pamoja na gharama ndogo za wafanyakazi...hilo nalo halihitaji uungwaji mkono wa rais....

  kama maoni ya masaka hata kama si msaidizi yanawakilisha kundi hilo...na watu kama hawa hata kama wana phd...kama za dr gama..nadhani wanazidiwa na watoto na wajukuu zetu wenye elimu ya msingi....kule mikindani na kwingine..shwn!!!!
   
 9. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sio Makosa yako nadhani ni uelewa mdogo wa kuchanganua mambo, kwani kazi ya Raisi ni nini? hata ikiwa Bia pia anatakiwa kuiangallia, kitu chochote kinachopangiwa Bei ndani ya Bajeti ya Taifa, lazima kiangaliwe na ikiwezekana kitolewe maelezo kama kimekaa vibaya

  Pole sana, kasome kwanza kazi ambazo wananchi wamemtuma Raisi kufanya ni zipi, alafu uje tena
   
 10. K

  Keil JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2008
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Masaka,

  Umeme huo ndiyo uliomng'oa EL, Karamaji na Dr. Msambaa na bado kuna wengine wengi watafuata baada ya hao vigogo kuachia ngazi. Bado unaona kwamba umeme ni kitu kidogo.

  Eti matatizo ya umeme ameyarithi/ameyakuta, ina maana hata Richmonduli nayo aliikuta? Hata kama tatizo ulilikuta ina maana huwezi kutafuta njia ya kujitoa kwenye hilo tatizo?

  Kama umesoma vyema maelezo ya MwK, ameainisha impliedly kwamba mikataba inayohusu umeme ni chanzo cha kupanda kwa bei ya umeme. MwK anauliza kwanini hayo makampuni yaendelee kulipwa wakati hayazalishi umeme? Mikataba hiyo mibovu ndiyo chanzo cha kupanda kwa bei ya umeme kila siku. Ndiyo maana TANESCO wanalalamika kwamba hawana uwezo wa kujiendesha kutokana na mzigo mzito na mikataba bomu ya IPTL, Songas, Aggreko, Richmond na mingineyo inayogusa sekta ya umeme.

  MwK hajaishia kutoa kilio tu, bali kaenda mbali zaidi kwa kutoa pendekezo, kwanini mikataba hiyo isivunjwe? Ndiyo maana katoa mfano wa serikali ya US kwamba huwa inavunja mikataba pale kasoro zinapojitokeza.

  Sasa pumba ziko wapi? Nadhani tunatakiwa kusoma kwa makini post ya mtu kabla ya kujibu hoja.

  Kwa maoni yangu JK ana uwezo wa kupunguza bei ya umeme kama kweli ana dhamira ya kufanya hivyo na kwa kuanzia angeanza na Richmond/Dowans ambayo kuvunja mkataba wake ni rahisi zaidi. Baada ya hapo aingie kwa Kiwira ambaye pia ni rahisi maana kama wakileta jeuri Mkapa na Yona itabidi wapande kizimbani kwa kutuingiza mkenge kwenye kampuni yao. Kosa la Mkapa na Yona ni kutumia madaraka vibaya kwa kuwa hatujui hata kama walifuata taratibu kwenye process nzima ya kujiuzia/kujimilikisha Kiwira.

  Mikataba mingine ya akina IPTL, Aggreko na Songas nayo inaweza kuwekwa kwenye darubini na ikachambuliwa kuona kama upenyo wa kuachana nayo. Bado hayo nayo ni magumu kuyafanya?

  Kwa hiyo JK has a role to play akiwa kama Rais. Kwa kuwatumia wasaidizi wake hayo yote aliyoyasema MwK yanawezekana!
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  mwafrikawakike,

  Ahsante sana kwa barua yako nzuri. Masuala yako uliyoshauri tutayashughulikia na tutakujulisha kupitia JF.

  KNY/ JK
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0


  Mukubwa Mwafrika Wa Kike,

  Kwanza heshima mbele, halafu pili ninaomba kukuunga mkono kwa barua yako kwa mtukufu rais wetu, hizi hapa juu ni point muhimu sana kwa rais kuzitafakari, maana sio siri kwamba sasa umeme ni karibu 50% ya mishahara ya wananchi walio wengi, bdo usafiri na chakula na mengineyo, na pia ni kweli serikali inaweza kuingilia kati matatizo ya uchumi ndio maana sasa hivi USA kuna rebate checks za taxes ambazo ni aneconomic act iliyochukuliwa na rais wa huko katika kujaribu ku-stimulate uchumi ambao ume-stall kwa sasa hivi, ni matumaini yangu kuwa Mkuu Darasalama ataufikisha ujumbe kwa rais akama anavyoahidi hapa.

  Ahsante Mkuu.
   
 13. M

  Mabbyjr Member

  #13
  Mar 5, 2008
  Joined: Aug 19, 2007
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli wewe ni Masaka. Tafsiri ya neno hili kwa lugha fulani huko kanda ya ziwa inamaanisha VICHAKA lakini sina hakika wakati unachangia hii hoja ulikuwa kichakani. Nakubaliana na one of the members hapa kuwa uelewa wako unaweza ukawa mdogo. Mambo mengine si lazima uende darasani ili ujue jinsi ya kuyachambua. Suala la Umeme ni muhimu sana katika taifa lolote dunia. Au wewe ulitegemea Mwafrika wa Kike aseme NISHATI ndipo ungeona kuwa linakufaa wewe. Sasa kama hutaelewa NISHATI na UMEME vina uhusiano gani basi ni kweli unahitaji ONE on ONE TUITION tena ya kusimamiwa na fimbo pembeni kama enzi hizo za MISINGI 7.
  Na hata kama tatizo hilo kalikuta ina maana Rais hawezi kushughulikia matatizo ambayo serikali yake imerithi kutoka kwenye serikali iliyopita??????? MASAKA MASAKA MASAKA jamani mbona haya mambo ni rahisi kuyaelewa? Mbona kamuondoa FISADI pale BOT na wakati huo alimkuta???!!! Jamani hilo nalo unahitaji darasa kuelewa!!! Lakini hata hivyo naamini hapa JF utapata darasa ila nina wasiwasi kama utaelewa mapema na vilivyo maana hakutakuwepo na mtu wa kukushikia KIBOKO au kukushikisha masikio through makalio kama hutaelewa.
  Hongera African Lady kwa ujumbe mzuri kwenda kwa Mheshimiwa SANA.
   
 14. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Pumba zingine Bw hata mashine ya kuchambua micros haiwezi kuchambua pumba kama hizi. Huyu Masaka ana aina fulani ya breki za akili sasa zime-jam, no more movement. Mateso yote tunayopata Watanzania kwa miaka mingi kiasi hiki yeye anaona ni kawaida (order of the day) Watanzania tuzidi kumshauri Rais wetu aingilie kati bei hii inayotuumiza hatimaye tutafanikiwa.
   
 15. Shukurani

  Shukurani JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 253
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nafikiri Masatu siyo mtanzania,japo jina lake lina asili ya visiwa vya ukerewe au kule majita. Masatu hizi ni pumba na kutokuelewa nini kinaendela nchi hii,hata kama nia yako ni kuleta ubishi na upambavu usiokuwa na akili. Kama kuna kitu amabcho kinasumbua wengi hapa kwetu ni hili suala la umeme.Masatu hebu fikiria 154Million tunalipa kwa richmond kila siku bila kupata umeme wowote toka kwa kampuni hii,hili siyo tatizo?Je hatuhitaji rais kuingilia hili?Je tutaendelea mpaka lini kulipia kampuni hizi hewa na zisizozalisha umeme? Masatu nasikitika sana ninapoona watanzania wachache wanadelea kuwa wajinga kiasi hiki kama wewe masatu. Sitoshangaa kuona Masatu ni miongoni mwa wale wanaowaona viongozi wao kama ni malaika vile. JK hili liko wazi lazima lifanyiwe kazi,tunasubiri majibu baba.
  Masatu shame on you
   
 16. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Jamani msameheni tu huyo Masaka, maana hata kwenye hizi teknolojia za computer Pentium I siyo sawa na Pentium IV. Inawezekana akili yake ina Pentium I "processor", hivyo inabidi afanye "upgrade" kwenda Pentium IV au zaidi.
   
 17. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkulu FMES,

  Hii issue ya umeme imekuwa noma na inabidi kwa kweli mkuu wa kaya aingilie kati. Wazee tusaidieni huko kufikisha mambo kama haya kwa sababu nina wasiwasi na Rweyemamu kama anafikisha hizi email tunazoandika kwa Kikwete!
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  mwafrikawakike,

  Ahsante sana kwa barua yako nzuri. Masuala yako uliyoshauri tutayashughulikia na tutakujulisha kupitia JF.

  KNY/ j
   
 19. C

  Chief JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2008
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Wewe ndio unatoa Pumba za mtama.
   
 20. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Kikwete,

  Wiki moja imepita sasa na bado nasubiria jibu (email au tamko) lako kuhusu hili. Watanzania wanaumia na hali inazidi kuwa mbaya kama huna taarifa hizi.

  Chonde chonde Kikwete........ nchi inakuangalia wewe ufanye the right thing katika hili.

  Thanks!
   
Loading...